MOI: Tutakuwa na kambi maalumu ya uchunguzi kwa watoto wadogo wenye matatizo ya mifupa na viungo

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
133
226
Kufuatia taasisi ya Tiba na Mifupa (MOI) kupokea kwa wingi watoto wenye matatizo ya muda mrefu ya mifupa na viungo, wameamua kundaa kambi maalumu ya uchunguzi kwa watoto wadogo changamoto hiyo ili kuwafanyia uchunguzi bure na kubaini magonjwa yanayowakabili.

Hayo ameyasema leo April 25, 2024 Dr. Antony Assey Mkurugenzi wa upasuaji wa mifupa na tiba ya majeraha MOI, amesema magonjwa hayo ni matatizo kwenye viungo mbalimbali kama magoti,nyonga,viwiko na uti wa mgongo.

"Tupo kwenye maandalizi ya kambi maalumu ya uchunguzi wa watoto wadogo wenye matatizo ya mifupa na viungo, inayotarajia kufanyika hapa kwenye taasisi yetu ya Moi tarahe moja Mwezi wa tano kuanzia asubuhi saa mbili asubuhi."amesema Dr. Antony

Ameongeza kuwa "Lengo la Kambi hiyo ni kutafiti na kubaini magonjwa yanayowakabili watoto wadogo, magonjwa yanayohusina na mifupa yao pamoja na viungo, magoti,nyonga, viwiko na uti wa mgongo"

Amesema kuwa sababu ya kufanya kambi hiyo, ni kwamba wamekuwa wakipokea watoto wengi wanaokuja na matatizo ya muda mrefu kutokana na sababu mbalimbali jambo ambalo ni changamoto, hivyo amedai kuwa kati ya sababu zinazopelekea matatizo hayo kuwa ya muda mrefu ni watoto wengi kucheleweshwa kuanza kupatiwa huduma kwa kufikishwa kwenye vituo stahiki vya afya.

Kutokana na hali hiyo amedai kuwa MOI wameona waje na kambi hiyo ili kutoa fursa ya kubaini matatizo hayo kwa watoto watakaofika, ambapo huduma hiyo itakuwa bure kwa kuwafanyia wahusika uchunguzi kisha kuwaweka kwenye utaratibu wa kupatiwa matibabu kulingana na uchunguzi wa kitaalumu utakavyobaini.

Akifafanua zaidi Meneja wa Idara ya Upasuaji Mifupa kwa Watoto MOI,Dr. Bryson Mcharo, amesema kuwa wameandaa kambi hiyo ambayo wanaamini itawasaidia watoto wenye changamoto za vioungo na mifupa hususani kwenye Jiji la Dar es Salaam pamoja na mikoa jirani.

Pia amebainisha wazi kuwa MOI ambayo inalo jukumu la kutoa huduma hizo inaendelea kusogeza huduma kwa wananchi kupitia Kambi hiyo pamoja na kushirikiana na hospitali nyingine katika kutoa huduma bora kwa ukaribu.

Aidha Dk. Bryson Mcharo Meneja wa idara ya upasuaji mifupa kwa watoto amesema wamewaita watoto wa mkoa wa Dar es salaam na Mikoa ya karibuni ambao wana matatizo hayo ni wakati mzuri wa kufika hospitalini hapo kupata matibabu

Kwa upande wake Emannuel Lema Dk.Bingwa mbombezi wa upasuaji wa mifupa ya watoto MOI amesema kuwa matatizo ya aina hiyo mtoto anaweza kuzaliwa nayo au mwingine akayapata baada ya kuzaliwa, miongoni mwa tatizo ambalo amelitaja kama kuwa wamekuwa wakikumbana nalo ni watoto wanaozaliwa na miguu kifundu, ambalo amedai kuwa chanzo kinaweza kuwa ni kutokana na upungufu wa baadhi ya vitu kwenye uzazi, hivyo akasema kuwa wanashauri mtu kupewa ujauzito ni muhimu miezi mitatu kabla akazingatia elimu inayoweza kumuepusha na matatizo mbalimbali mtoto anayetarajia kumpata.

Screenshot_20240425-201420_1.jpg
Screenshot_20240425-201129_1.jpg
 
Back
Top Bottom