ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,413
50,231
Mbunge wa Konde (ACT Wazalendo), Mohamed Said Issa ameitaka Serikali kurejesha upya utaratibu wa watu wote wanaoingia Zanzibar kuwa na hati ya kusafiria.

Akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Rais Makamu wa Rais kwa mwaka 2024/25 leo Jumanne Aprili 24,2024, Issa amesema lengo ni kuvilinda visiwa hivyo.

“Kwa nini waliweka pasipoti (hati za kusafiria) visiwa vile vinahitaji kulindwa, mimi sikubaliani na suala la kutovilinda visiwa saa hizi. Sasa hivi Zanzibar imejaa watu na tunavyoendelea hawatakuwa na sehemu ya kuishi,”amesema.

Issa amempongeza, hayati Abeid Karume kwa kujenga maghorofa yale (hakusema yako wapi) kwa kuwa alitaka Wazanzibar wote wakae humo, kwa sababu aliona ardhi ni ndogo sana.

“Sasa hivi ukienda pale Zanzibar utakuta viwanja vimechukuliwa, miti imekatwa, kulikuwa na zao la mikarafuu haliko tena, imebakia Pemba tu na kule Pemba linakwenda kuisha minazi hakuna sasa hivi tunaagiza kutoka Mafia ,”amesema.

Amesema jambo hilo sio zuri na hata ajira za watalii hawapati tena Wazanzibar wanaofanya kazi hizo ni wageni.

Pia soma

=====My Take
Serikali puuzeni huu ushauri Ili mwisho wa siku tuwe na Tanzania Moja japo ana hoja na asikilizwe na kujibiwa Kwa hoja.


View: https://www.instagram.com/p/C6IZ13IqXEa/?igsh=MWdhYmZ2cXhua2RyZg==

Majibu ya Serikali Kupitia Waziri wa Masuala ya Muungano Suleimani Jago akimjibu Mbunge hii hapa 👇👇

View: https://www.instagram.com/p/C6I5bsgNu5f/?igsh=Y3c0YnF5MXdhNGI1
 
Huyu Mbunge sijui ana umri gani! Wazanzibar walijaribu hilo miaka ya nyuma Wabunge wa Tanganyika wakasema nao waje kwa Passport. Wazanzibar waliondoa utaratibu ndani ya siku 7. Mwalimu Nyerere alisikia akaacha Bunge liwakaange!

Mbunge huyo aliyechaguliwa na watu 2,500 anasema watu wamejaa Zanzibar hakuna ardhi! Huyu sijui ana elimu gani. Anayeuza Ardhi kwa Wataliano ni Hussein Mwinyi. Visiwa vyote vimeuzwa.

Pili, huyu Mbunge wa watu 2,500 anatamani Zanzibar ya watu Laki 3 hajui kwamba population ni takribani 2 Milioni na 1.4 Milioni kwa takwimu wanaishi Tanganyika

Tungefurahi sana wakirudisha utaratibu wa Passport! Tena ikiwezekana wiki ijayo

JokaKuu Mag3 Pascal Mayalla
 
Mimi ningekuwa Rais ,Kwanza task ya Kwanza wale wote waliokuja bara baada ya Uhuru nawaambie mrudi kwenu natoa mwaka mmoja kila mtu awe ameshaondoka, na kinyume chake aliyeko Zanzibar baadae ya Uhuru Rudi ulikotoka, task ya pili kila taifa liwe na Uhuru wake na sio kama Sasa Tanganyika tunafanywa mbeleko zao,

Task ya tatu anayetaka kuja bara awe na passport ya kumruhusu kukaa Kwa sheria za kimataifa na anayetaka kwenda Zanzibar na yeye itabidi awe na passport yake Kwa sheria za kimataifa.

NB undugu utakuwepo kama ilivyo Msumbiji naTanzania au ENGLAND NA SCOTLAND tumechoka kuibiwa .
 
Mbunge wa Konde-ACT Wazalendo ambae anatokea Zanzibar ameitaka Serikali kurejesha utaratibu wa kuwa na Passport Kwa watu wa Bara wanapenda Zanzibar...
Nyerere sijui alitoka wapi na hawa mapumbavu!!

Imagine akili ya aina hii ndo iko magogoni inatawala nchi!! Haki TZ kuna maiti zinazotembea maana kama hata wasio na visogo wanatutawala na bado tumelala huku tukibishania Simba na yanga tumekwisha!!

Afrika ilikua bado sana kujitawala kwa picha ya hawa wapumbavu.
 
Mimi ningekuwa Rais ,Kwanza task ya Kwanza wale wote waliokuja bara baada ya Uhuru nawaambie mrudi kwenu natoa mwaka mmoja kila mtu awe ameshaondoka, na kinyume chake aliyeko Zanzibar baadae ya Uhuru Rudi ulikotoka...
Hawawezi kurudi wanaomba vibalo vya ukaazi na kufanya kazi au biashara
 
Back
Top Bottom