Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo anashikiliwa na Polisi, anyimwa dhamana

inaumiza sana ukiiwazia, na kuisikia, lakini wamekuja watu wengi kuijaza hii thread na sumu mbaya. naogopa nchi yangu inakoelekea
 
Zamani kulikuwa hakuna udikteta uchwara,zmani hakuna alietamani malaika waje wazime mitandao,zamani tulikuwa tuna bunge live,zamani mikutano ya siasa haikufutwa.......kwa hyo usituletee hadithi zenu za lumumba wanafki wakubwa nyie mnataka msifiwe tu.
Walidhani hapa ni bunge live
 
Halafu bado mnadhani mtaendelea kujificha kwa anuani bandia, kwa upuuzi kama huu,! Unaposhindwa kumheshimu rais wa Nchi yako unayeweza kumpa heshima ni nani ? Katika maisha yako??
Biblia inasema tiini mamlaka iliyo kuu sabbu hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu. !!! Halafu kwa kebehi na dharau zenu mnataka Nchii iendelee kuwaangalia tu,! Kwa kisingizio cha uhuru wa maoni na kukosoa.!
Haiwezekani na halitawezekana.
Unataka tumweshimu yy tu kwan yy amemheshimu nani. TOKA ZAKO HAPA
 
- Tunajenga Taifa so wananchi mchana mzima wanatakiwa kuwa kazini sio kuangalia Bunge live, hayo mengine ya kwako na ni nonsense!

le Mutuz
Mkuu,

Kwa nini matangazo ya bunge yalikuwa mubashara "in the first place"? Je, ni kweli kwamba matangazo hayo kuwa mubashara yalichangia kushuka uchumi wetu au watu kuacha kutimiza wajibu wao makazini na maeneo mengine?

Kaka ...
 
Mjinga mimi au wewe. Ukipiga kelele JF kuwa sheria hairuhusu then what? Ni hatua gani mnatakayochukua? Au mnataka kufarijiana nyuma ya keyboard.

Wenzenu vitu kama hivi kama wanaona vimekosewa hatua ya kwanza ni kwenda kuomba tafsiri ya mahakama then zingine zinafuatia.

Alipoteuliwa Naibu Spika Tulia mlikuja na hoja kama hizi then what? Kwahiyo mkishatoa malalamiko hapa then watu wakachangia imeisha.

Nyinyin ndio wajinga. Sehemu serikali ilipokosea ndio mtaji wa vyama vya upinzani. Ila kwa wapinzani nyinyi serikali ikikosea basi ni gia ya kusutana baada ya ku take proper actions

Sina haja ya kubishania ujinga.
 
Maelezo yako ni mazuri kwako. ukabila wako hauna nafasi Tanzania. Tunaweza kuendelea kama taifa hata tusipozingatia haya mawazo yako yako ya Kikabila.
Ukweli uko palepale kuna tofauti kati ya kuropoka na Freedom of speech.
Max yuko ndani kukutea watu kama wewe.

Be peacefully, obey laws.
Tunaamini haki itapatikana kwa Max Melo, MUNGU mwenye HAKI atamsimamia.
Tunaelezwa JamiiForums.com haina uwezo wa kumtambua kila mtumiaji wa mtandao huo kwasababu ya mfumo wanaotumia ama mtumiaji mhusika aamue mwenyewe kutoa utambulisho unaofahamika kwa wengine kama kutumia jina halisi. Tumeona wengi wanatumia majina ambayo si halisi ukiwa wewe Jick na wengine wengi. Kwa mfumo huo, mtu anayejisajili halazimiki kutoa particulars ambazo zinaweza kum-link mhusika (by using real names, phone numbers etc.) ndiyo maana wengi wanaamua kutumia majina ambayo si halisi. Lakini tukumbuke kuwa watumiaji wengu wa mtandao huu ni watu tofauti wakiwepo viongozi nyeti katika serikali ambao pengine anadhani hana sehemu ya kusemea, analazimika kuja JF. Hata wale ambao wanatumia majina halisi inaaminika kuwa nao wana accounts zisizo na utambulisho unaofahamika pia.
Haya yanatokea kwakuwa watu wanakosa uhuru wa kuongea, kwani hata kama kinachozungumzwa si cha kweli kwani shida iko wapi..?? Toka mbele kanusha with facts! Ndivyo mataifa yote yanavyofanya kazi, hii inatufanya tuzidi kurudi nyuma zaidi. Serikali kuhangaika na JF na kutumia nguvu nyingi ni kukosa maarifa ya kufanya kazi. JamiiForums iko miaka mingi mno, why leo yanatokea haya?? Non-sense kabisa!
 
Wakuu,

Taarifa mpya ni kwamba, Mkurugenzi wa JamiiForums, Maxence Melo mpaka muda huu bado anashikiliwa na polisi na hajafikishwa Mahakamani kama sheria inavyotaka.

Alifanyiwa mahojiano jana usiku kwa muda mrefu na faili lake limechukuliwa linapelekwa kwa DPP mchana huu.

Bado mashtaka halisi yanayomkabili hayajawekwa wazi.

Taarifa zaidi kukujia...
 
Eeeh, Mola wetu, kila ajae kwa shari, waijua yake siri, ivunje yake dhamiri asiweze kusimama! wote natuseme amin!
 
Wakuu,

Taarifa mpya ni kwamba, Mkurugenzi wa JamiiForums, Maxence Melo mpaka muda huu bado anashikiliwa na polisi na hajafikishwa Mahakamani kama sheria inavyotaka.

Alifanyiwa mahojiano jana usiku kwa muda mrefu na faili lake limechukuliwa linapelekwa kwa DPP mchana huu.

Bado mashtaka halisi yanayomkabili hayajawekwa wazi.

Taarifa zaidi kukujia...
Aluta Continua!

Kaka ...
 
Melo yuko salama..wala hakuna jambo jipya kaitwa kuhojiwa tuu.
Lakini walio sababisha kuitwa kuhojiwa ni wale waleta habari za uzushi ambazo serikali inalazimika kuhangaika kuzikanusha kila leo...
sheria ile ya mitandao ina ipa mamlaka polisi kupata taarifa za mtu kutoka kwa mtu na inawezekana hata kuchukua vifaa husika...
Melo yuko salama salimini.
Mpaka leo bado anahojiwa?
 
Melo ushauri wangu ukishatoka hamishia kazi zako Kenya, nenda kafungue ofisi na kazi zifanyike pale, ili tuwe tunafunguka sawasawa, hapo utapigwa zengwe mpaka basi,
 
Kama taifa, tunayumba na kupotea mwelekeo sana. Mungu wa rehema kawajaze viongozi wetu hekima na busara katika haya yanayotukumba kama taifa. Kazuie ombwe la uongozi ktk taifa letu ili hatimaye maoni na tuhuma ziibuliwazo na wananchi zikasaidie serikali kuchunguza watuhumiwa na kuwashughulikia badala ya mtoa/ mwibua taarifa.
 
Back
Top Bottom