Mkazi wa Arusha amwambia Makonda: Mtoto wangu amelawitiwa, Askari Polisi hawanisaidii na wananipa vitisho

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,941
12,234
Mkazi wa Muriet Jijini Arusha akielezea changamoto aliyokutana nayo akidai Mtoto wake amelawitiwa na baadhi ya Watu huku Askari kadhaa wa Murieti wakimzungusha kupata haki yake licha ya vipimo vilivyofanyika katika Hospitali ya Murieti na Mount Meru kuthibitisha ukatili aliofanyiwa mwanaye.

Ameeleza hayo wakati wa Mkutano wa Wananchi kuelezea kero zao ulioandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda kwenye Ofisi za Mkuu wa Mkoa, Mei 10, 2024 na kuongeza kuwa kuna kesi nyingi za ulawiti Muriet hasa zinazohusu Watoto na hakuna hatua zinzochukuliwa kama mzazi wa mhathirika hana hela.

Baada ya maelezo hayo, Makonda akasema “Mkuu wa Wilaya wa Arusha Jiji na OCD wa Arusha Jiji ninawapa Saa 24, watafute wahalifu na hatua kali za kisheria zichukuliwe, Askari waliotoa kauli ambazo si nzuri niwajue majina, OCD hakikisha ulinzi wa huru dada, RMO kote alikofanyiwa vipimo Mtoto nataka ripoti na Mtoto apewe Dawa aweze kupona.”
 
Nchi ishakua failed state, watu wa ngazi za chini hawawajibiki na wamejaa rushwa, kesi kama hizi ilitakiwa polisi wazimalize, wakuu wa mkoa wafanye majukumu makubwa ya kuleta chachu za maendeleo


Imagine mkuu wa mkoa ndo analetewa kesi za ardhi, watu kulawitiana, sijui wengine wagonjwa, wizi wa magari n.k. Pity issues ambazo mamlaka za chini walitakiwa kushughulikia
 
Mmmh.
hivi,kesi ya ulawiti inaweza chukuliwa kwa uzito mdogo hivi kama mtu kaibiwa bufa?.
Ngoja tujue upande wa pili.
Yule mama aliyeangua[ga] kilio kuwa anataka kuzulumiwa nyumba ya mmewe,magufuli akaagiza ngazi huska wafuatilie ilo jambo..kumbe yule mama ndiye anataka kuzulumu nyumba halali ya watoto wa marehemu mme wake.
 
NAAAM MATOKEO YA AWAMU DHAIFU
UTENDAJI HAKUNA, MATOKEO HAKUNA
NI MWENDO WA MASIFA, PONGEZI, KUJIPENDKEZA TU, MAMA HIVI MAMA VILE.
 
Back
Top Bottom