Mjadala: Je, ni kwanini gari hupoteza nguvu? Je, unawezaje kutatua tatizo hili?

Tafuta fundi acheki sensa nilishakutana ugonjwa hu kwenye suzuki v6 nilipoteza zaidi ya milioni 1 badae ikaja kugundulika ni sensa nikatibu kwa sh120000 unaweza ukakuta ghafla inapoteza nguvu na ikirudi kama inastuka kuwa makini sana unapoiendesha
Kaka nimepata tatizo Kama lako kwenye suzuki swift nimebadilisha pump, coil lakini bado tatizo lipo
Ulikuta sensor gani imekufa
 
Naombeni kujua shida nini, gari kama hiyo inapoteza nguvu. ukiwa kwenye mwendo ghafla unakutana na hali ya gari kukosa nguvu mfano wa kuzibwa pumzi au wewe unakanyaga mafuta na mwingine anakanyaga break.

naomba kujua inasababishwa na nini na utatuzi wake ni nini?

Gari ni Nissan HardBody
Engine ZD30 Turbo.
Kwenye gari hasa Nissan ikikosa nguvu unasikia kama imezibwa pumzi shida inakuaga kuziba kwa Exhaust Masega unaweza kubadilisha sensor zote usipokua makini na tatizo likabaki pale pale na hata ukipima inaweza isishtakie hiyo shida ya kuziba exhaust Masega mpaka umpate fundi makini wa kuskilizia gari
 
Back
Top Bottom