Mitandao ya Tanzania ni ya hovyo mno, Tigo, Vodacom, Airtel internet ni takataka tu. Wanatuibia pesa zetu

Wakuu, kwenye Internet service yenye speed ya uhakika na bila wizi wizi wa data (data hewa), nijiunge na kampuni ipi? kati ya hizi tatu:

✓ TIGO POSTPAID
✓ HALOTEL M2M
✓ AIRTEL SME

Matumizi kusudiwa: Online Studies with live tutorials and downloads.

Cc: Mwl.RCT , Chief-Mkwawa , BROKE BOYS , OKW BOBAN SUNZU

-Kaveli-
Jiunge Halotel M2M, imeboreshwa zaidi maana ime specialise kwenye internet tu. Speed inakuwa bora zaidi.
 
Niko mpakani huku natumia Safaricom ,hawana huu ujinga, Safari Com hawezi fanya uhuni kwa Wakenya watakinukisha dakika sifuri. Tanzania tatizo wanaona raia ni mazeta, ndio maana wanafanya watakavyo
Kwa upande wa Tanzania sio Mitandao tu hata Bank loan wanaibia raia yaani nawaza kuhama nchi hii kwa muda hadi hali itakapotengemaa. Yaani viongozi ni kama mazombie yapoyapo tu.

Kuna wkt nawaza hivi ?au ndio maana mange anawatukanaeee? Yaani waziri yupo tu
 
Hivi ile pocket AIRTEL router ya 4G (Inauzwa TSH 50,000), ina UNLIMITED package? SIM card yake inakubali na kwenye smartphone?

Cc Kang

-Kaveli-
 
Huduma za Internet kwa mitandao ya Tigo, Voda na Airtel kwa Tanzania ni mbovu mno.

Mtu unaweka bundle lakini mpaka inaisha unakuta hujatumia ipasavyo kutokana na kukatika katika kwa huduma husika.

Muda mwingi network hakuna hata ikiwa ni maeneo ya mjini kabisa.

Hivi wahusika mnajielewa kweli??

Kwanini mnachukua pesa zetu halafu mnatoa huduma mbovu.

Acheni wizi kwa watanzania, mnachukua pesa bila kutoa huduma za kueleweka.

Karibu halotel 🤕
 
Kuna laini za internet zipo vizuri sana ata bando lake linachelewa kuisha mno zinaitwa M2M. Mcheki jamaa 0615269508

Wadau wanasema hizo laini za M2M hazina UNLIMITED DATA PACKAGE. Zina bando la kupimiwa.

-Kaveli-
 
Back
Top Bottom