Milton Mahanga: Naomba niweke wazi, nilikuwa sitaki lakini mmezidi CCM. Acheni kunirubuni kwa fedha nirudi chama chenu

Huyu sio yule Mahanga akiwa mbunge alitapeli wananchi wa jimbo lake mpaka wakampeleka mahakamani? Na kutokana na hizo tabia za kitapeli Waziri wa Ujenzi wakati huo alikataa kumrudishia uenyekiti wa NBMM? Au anadhani waTZ tumesahau? Kwani kwenye kura za maoni CCM kugombea ubunge Mahanga si alishindwa? Sasa alijiuzulu au alikataliwa na wanachama? Na hao wanaomtaka arudi CCM ni kwamba hawajui mwenyekiti wa taifa ndiye aliyekuwa waziri wa ujenzi na kumnyima uenyekiti wa NBMM? Au wanadhani naye kasahau?
 
Manunuzi yakishazoeleka na kuleta uasi uliosababishwa na manunuzi mwisho ni aibu. Mubutu kilichomwangushaga ni siasa kama hizi za matumizi ya fedha.
 
Je wakipiga tunch ile nyumba ya kifahari ambayo haijamalizika pale regent estate , utaendelea kukataa??
 
Kwani hili nalo ni jipya Kwako? Jiulize ushahidi wa Nassari Uko wapi? Zaidi sana mtuhumiwa amepandishwa cheo.
Sad sad,
Vita dhidi ya Rushwa ni just a theoretical war, but practically tunajidanganya aisee
 
Kachoka kuona mijitu mizima kila wakati kumbembeleza eti njoo ccm mambo yatakuendea vizuri. Wanadhani yeye ni dhaifu na kahaba wa kisiasa kama kina MOTOCHINI? Lazima aweke tahadhari asije kuchukia bure akawalamba makofi makada wenu bure! marabuk!!
Ukoo wake tu walisha msahau
hajulikani
Ccm aje kufanyanini!
 
bodi ya manunuzi imeusika na wakusanya kodi wamekata makato yao...? au huku VAT na kodi zingine haziusiki ??
 
Maisha yangu yote nimeishi kwa misimamo yangu na imani zangu. Nilitoka CCM tarehe 02/08/2015 na nikaacha uwaziri kukiwa na miezi mitatu mbele na kuacha mishahara na marupurupu ya miezi hiyo mitatu, nikaacha "mkono wa kwaheri" wa mwisho wa mawaziri na nikarudisha "shangingi" la serikali siku hiyo hiyo ili kujiunga na CHADEMA.

Nilifanya hivyo kwa sababu hiyo ndiyo ilikuwa imani yangu, msimamo wangu na dhamira yangu. Sikushawishiwa na mtu yeyote na huwa sishawishiwi bila mimi kuamini. Naishi kwa ninachokiamini kwa dhati! Hivyo hakuna kinachoweza kunishawishi kubadilisha imani na dhamira yangu ile ya tarehe 02/08/2015. Siyo njaa yangu, siyo ahadi ya fedha na wala siyo ahadi ya cheo. Na siyo hata vitisho vya aina yoyote. HAKUNA!

Hivyo acheni kutuma watu wenu, rafiki zangu na ndugu zangu kunishawishi! HUWA SISHAWISHIKI! Na imani yangu, utu wangu na msimamo wangu huwa haina bei. Kamwe sitarudi CCM ng'o! Acheni kuhangaika!
Ha ha ha ameamua kutangaza kuwa naye anatamani dau.
Mtafuteni Makongoro..waziri aliyewahi kuruhumiwa na Chadema kuweka sanduku la kura kwapani na kukimbia nalo, aliyewahi kutuhumiwa na ccm kuwa waziri mzigo.
 
kwani wanakuitaji unaushawishi mkubwa sn ktk jamii?ah ah ah ntawashangaa ccm kama na wewe wanakufata
 
Waweke dau zuri mezani ulambe, hela za kuhamisha wanazo wanakosa tu za kuongezea maslahi watumishi wa umma
 
Back
Top Bottom