Mkoba wa Mama
Senior Member
- May 5, 2021
- 115
- 46
UTANGULIZI.
Ninashauri uundwe mfumo maalumu utakao beba taarifa zote muhimu za wananchi kuanzia pale mtu anapozaliwa mpaka kufariki. Mfumo huu uwe wa kielektroniki utakaosimamiwa na mamlaka zinazohusika na mambo ya uraia, ili usaidie upatikanaji wa taarifa zote muhimu za wananchi katika sehemu moja na kwa urahisi zaidi.
MAELEZO MUHIMU.
Mfumo huu utakuwa ukiwezesha mamlaka husika kuiingiza taarifa za mtu baada ya kudhibitisha taarifa hizo ni sahihi na ni za mtu aliye kusudiwa.
Taarifa za mtu zitakuwa zikitumwa na taasisi mbalimbali (mfano hospitali, shule, vyuo, baraza la mitihani, NHIF, NIDA, polisi, mahakama na taasisi nyingine) katika mamlaka itakayo kuwa ikisimamia mfumo huo, taarifa hizo zitahakikiwa kama ni sahihi kabla ya kuingizwa katika mfumo.
Kwa maana hiyo kila mwananchi atatengenezewa akaunti yake maalumu itakayo kuwa na taarifa zake zote na kupatiwa kitambulisho kitakachokuwa na namba ya akaunti hiyo. Akaunti hiyo iwe na vipengele mbalimbali kama vile sehemu ya taarifa za elimu, afya, ajira, uraia, anuani na makazi, na vipengele vingine.
Mwananchi atakuwa na uwezo wa kuingia katika akaunti yake kwa kutumia namba maalumu na ataona taarifa zake zote, lakini hatokuwa na uwezo wa kubadili taarifa hizo yeye binafsi. Iwapo baadhi ya taarifa za mtu zitakuwa sio sahihi na zinahitaji marekebisho, basi mhusika atawasiliana na mamlaka husika na kutoa udhibitisho wa taarifa sahihi na mamlaka watahakiki taarifa hizo na baada ya hapo taarifa zake zitarekebishwa.
Mfumo huu utawezesha mamlaka husika kuingiza taarifa zilizotumwa na kuthibitishwa kutoka katika taasisi mbalimbali za umma, mfano baada ya kuzaliwa, hospitali alipo zaliwa mtoto watatuma taarifa kwa mamlaka husika na mtoto huyo atatengenezewa akaunti na taarifa zake zitaingizwa (tarehe na mwaka wa kuzaliwa, mahali alipozaliwa, jinsia, taarifa muhimu za wazazi wake na taarifa nyingine muhimu ambazo hukusanywa pale mtoto anapozaliwa).
Taarifa zitakuwa zikiboreshwa/kuhaririwa kadri mtu anavyozidi kukua na kupiga hatua nyingine katika maisha. Mfano mtoto atakapo sajiliwa shule, shule aliyo sajiliwa mtoto itatuma taarifa za mwanafunzi huyo kwa mamlaka husika na hivyo kuingizwa kwenye akaunti ya mhusika maana tayari akaunti ilishaundwa mtoto alipozaliwa (mwaka alioanza shule, umri, shule anayosoma, mzazi/mlezi anayehusika na usimamizi wa mtoto na taarifa nyingine muhimu).
Mtu atakapo hitimu katika ngazi yoyote ya elimu, taarifa zake zitaingizwa kwenye akaunti yake (mfano, shule/chuo alipohitimu, mwaka wa kuhitimu, fani/masomo aliyosoma, matokeo yake na taarifa zote zinazohusika).
Vivyo hivyo mtu atakapo ajiriwa/ kujiajiri. Iwapo ataajiriwa, basi mwajiri wake atatakiwa kutuma taarifa zote sahihi (mfano, aina ya ajira, mkataba, mwaka alioajiriwa, na taarifa nyingine muhimu zinazohusu ajira hiyo). Na ikitokea mtu amejiajiri, basi itambidi atume taarifa sahihi kwa mamlaka husika na mamlaka wajithibitishie kabla ya kuingiza taarifa hizo katika akaunti ya mhusika (mfano aina ya shughuli anayofanya, mahali anapofanya shughuli zake, mtaji wake na vitu vingine muhimu).
Lakini pia mfumo huu utawezesha jeshi la polisi na taasisi nyingine za usalama na haki, kutuma taarifa za mtu yeyote atakaye kutwa na hatia/kosa kwa mamlaka husika ili taarifa ziingizwe katika akaunti ya mhusika na zibaki katika kumbukumbu (mfano, aina ya kosa, mahali alipotenda kosa hilo, mda/mwaka aliotenda kosa, sababu, madhara yaliyosababishwa na kosa hilo, aina ya adhabu aliyopewa na taarifa zote muhimu zinazohusiana na mashtaka).
Ikitokea mtu amefariki, taarifa za kifo zifikishwe kwa mamlaka husika ili kuwezesha kuingizwa katika akaunti ya yule aliyefariki (mfano, tarehe na mwaka aliofariki, mahali kifo kilipotokea, sababu ya kifo na vitu vyote muhimu).
Mbali na taarifa hizo, mfumo huo pia utubeba taarifa mbalimali, taarifa hizo ni kama vile hali ya ndoa, umiliki wa mali, kitambulisho cha taifa, leseni ya udereva, bima ya afya, cheti cha kuzaliwa, kitambulisho cha taifa na viambatanisho vingine. Hivyo mtu atatengenezewa kitambulisho na namba moja tu, na atatumia kitambulisho na namba hiyo kuona taarifa zake zote na kwa shughuli nyingine zitakazo hitaji kupata taarifa zake.
Kwa mfano kama mtu amejiunga na bima ya afya, akifika hospitali atatoa kitambulisho chake, wataingiza namba yake mtandaoni na taarifa zake zote zinazohusu bima zitaonekana, vivyo hivyo hata katika maeneo mengine, mfano dereva amekamatwa barabarani na askari, atawapatia kitambulisho chake, wataingiza namba yake mtandaoni na wataona taarifa zake zote zinazohusiana na leseni.
NINI UMUHIMU WA MFUMO HUU.
Kwanza kabisa utawezesha serikali kuwa na taarifa sahihi, halali na za uhakika za wananchi wake, hivyo kupunguza udanganyifu wa taarifa na taarifa za kughushi ambazo baadhi ya watu hutumia katika baadhi ya mambo ikiwemo kupata ajira au kupata nafasi ya kufanya kitu fulani.
Kuwezesha serikali kupata takwimu mbalimbali kwa urahisi zaidi sehemu moja, hivyo kupunguza baadhi ya gharama na mda mrefu wa upatikanaji wa takwimu, hivyo kurahisisha shughuli mbalimbali za serikali hasa katika kuwahudumia wananchi, takwimu hizo ni kama vile; hali ya vizazi na vifo, hali ya elimu, idadi ya walio ajiriwa na kujiajiri, uhalifu na takwimu nyingine muhimu.
Kupunguza usumbufu wakati wa kuajiri/kuajiriwa.
Hapa mwajiri ataweza kuingia mtandaoni na kuangalia akaunti ya mtu anayetaka kumuajiri, hivyo ataweza kuona taarifa zote anazohitaji kuziona. Hii itapunguza usumbufu wa watu kutembea na makaratasi wakitafuta ajira na kupunguza gharama za watu kuandaa na kutuma vyeti vya elimu na taaluma wakati wa kutuma maombi ya kazi, pia kuondoa udanganyifu wa kutumia cheti cha mtu mwingine.
Faida nyingine, ni wakati wa zoezi la sensa ya watu na makazi, serikali itaweza kupata taarifa zote muhimu za wananchi katika mfumo huo na kwa urahisi zaidi.
Kupunguza gharama ya uandaaji wa nakala ngumu za vitambulisho na vyeti mbalimbali, lakini pia usumbufu pale mtu anapopoteza kitambulisho au cheti hivyo kumgharimu fedha na mda wa kufuatilia nakala nyingine.
Lakini pia kupunguza wingi wa vitambulisho na vyeti ambavyo watu hupewa na taasisi mbalimbali ili kuwawezesha kupata huduma mahala fulani.
HITIMISHO.
Ili kuwezesha mfumo huu unahitaji wataalamu wa teknolojia ili kuuandaa, kuuendesha na kuuwezesha kufanya kazi kwa ufanisi bila kuingiliwa na mtu au taasisi yoyote ile. Hivyo serikali itumie wataalamu waliopo kuandaa na kuendesha mfumo huu.
Ahsanteni.