Mbunge wako na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wanafika eneo lako kushughulikia Kero au ndio wamepotea hadi Uchaguzi ujao

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,449
8,267
Tunaelekea mida ya kuanza kuwaona Waliotuomba Kura 2019 na 2020 wakitaka nafasi za Ubunge na Wenyeviti wa Serikali za Mtaa wakijipitisha tena kama vile walikuwepo.

Vipi hapo kwako Kiongozi uliyemchagua anashughulika na Kero zenu au ndo hata hujui alipo?
 
Hivi hawa wenyeviti wa mtaa si wale ambao hawakupigiwaga kura?

Hawa hatawasipofanya kazi hakuna wa kuwalaumu kwani hakuna aliyewachagua zaidi ya Marehemu.

Mbunge wa hili jimbo ninaloishi alikuwa anafanyafanya vikao/ kwenye kata jimboni kwake na kuna mshkaji namfahamu alikuwa kama mwandishi wake wa kumsaidia kurusha habari zake mitandaoni alikuwa ananipa ratiba za mikutano na ishu zilizokuwa zinajadiliwa Kwenye hiyo mikutano jamaa alikuwa analipwa laki2 Kwa mwezi.

Sasa tokea huyo mbunge kuteuliwa kuwa waziri na samia Kwenye mabadiliko aliyofanya hajaonekana wala simsikii tena kwenye kata na yule mshkaji wangu aliyekuwa msaidizi wake kazi na mbunge hamna yupo anapiga ishu nyingine za uandishi wa habari binafsi
 
Tunaelekea mida ya kuanza kuwaona Waliotuomba Kura 2019 na 2020 wakitaka nafasi za Ubunge na Wenyeviti wa Serikali za Mtaa wakijipitisha tena kama vile walikuwepo.

Vipi hapo kwako Kiongozi uliyemchagua anashughulika na Kero zenu au ndo hata hujui alipo?
kiongozi, ana chapa kazi kwa weledi na bidii sana hapa mtaani, na ametuunganisha sote katika umoja, pamoja na viongozi wa aina mbalimbali, na tusonga mbele kwa pamoja, na kwakweli uelekeo ni mzuri sana tunapoelekea uchaguzi serikali za mitaa baadae mwaka huu2024, na uchaguzi mkuu mwaka ujao2025....

Mambo ni mazuri, matumaini ya wanainchi ni makubwa mno, na matarajio ya maendeleo ni ya uhakika zaidi tuendako.... :DisGonBGud:
 
Tunaelekea mida ya kuanza kuwaona Waliotuomba Kura 2019 na 2020 wakitaka nafasi za Ubunge na Wenyeviti wa Serikali za Mtaa wakijipitisha tena kama vile walikuwepo.

Vipi hapo kwako Kiongozi uliyemchagua anashughulika na Kero zenu au ndo hata hujui alipo?
Wa kwetu sisi ni much appreciation kwake kwasababu anafika na anajitahidi kadiri ya uwezo wake, kuna wengine huwa wanagombea kwasababu nafasi ziko wazi ila kwenye suala la utendaji ni sifuri, kwa mamtiki hiyo tunatakiwa kupata siyo ilimradi wagombea! Bali wagombea wenye weledi wa kuongoza. Na kama tumeshindwa kabisa kuminfluence na kumpa support mtu ambaye ana kipawa cha uongozi na tukampa uongozi kwasababu ya mali anazomiliki matokeo yake ndo kama haya wanarudi wakati wa uchaguzi tu, na huu muda mwingine wanatumia kufanya mambo yao binafsi.
 
Back
Top Bottom