Mbunge Kwagilwa Nhamanilo Akichangia Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi Bungeni Jijini Dodoma

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,994
961

MBUNGE KWAGILWA NHAMANILO Akichangia Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi Bungeni Jijini Dodoma

"Nampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwasababu anakwenda kuweka historia kubwa Tanzania kama Rais aliyefanya Mapinduzi makubwa kwenye eneo la Reli. Serikali inatarajia kutengeneza mtandao wa Reli ya kisasa SGR unaokaribia Kilomita 4572 ambao utagharimu karibu Shilingi Trilioni 20+ na tayari Serikali ya CCM imeshalipa Shilingi Trilioni 10+ kwaajili ya kazi zilizokwisha kamilika" - Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo, Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini

"Yapo mambo lazima tuyarekebishe wakati tukikaribia kwa zoezi (Operation) za Treni ya SGR kutoka Dar es Salaam - Makutupola wakati tukiendelea kukamilisha vipande vilivyosalia. Lazima tufanye usafiri na usafirishaji kuwa wa kisasa kwa kuifungamanisha SGR na miundombinu mingine ya usafiri"

"Zipo Taasisi ambazo Lazima zifanye kazi usiku na mchana kama TANROADS, TARURA, Halmashauri za Miji ambapo Reli inapita na Bandari. Kituo cha SGR Morogoro Lazima tuwe na barabara nzuri ya kufika kwenye Kituo ijengwe kwa kiwango cha lami na kujenga miundombinu ya mabasi ili wanaoshuka wapate usafiri mwingine. Vivyo hivyo Kituo cha Kilosa na Ngerengere. Mradi ufanane na thamani yake"

"Mradi wa SGR Lazima tuufungamanishe na sekta za uzalishaji kama Kilimo, Mifugo, Madini, Utalii na Viwanda. Tusijenge SGR kwa kutazama mizigo ya nchi jirani pekee yake. Wizara za uzalishaji zione ni namna gani zitaifanyia SGR inayojengwa na Watanzania. Uwezo wa Treni ya SGR itakuwa na uwezo wa kusafirisha Tani Milioni 17 kwa kiwango cha chini na kiwango cha juu itasafirisha Tani Milioni 25 kwa mwaka"

"Lazima tuweke mkazo kwenye uhusiano wa SGR na utunzaji wa Mazingira. Kwenye ujenzi kuna kitu kinaitwa Hard Part Engineering Design ndicho tunaangalia Environment Impacts Assessment ndiy watu wanajenga Reli. Kitu muhimu kwenye miundombinu ya Reli ni Soft Part Engineering Design inayohusu kutunza Mazingira na kutunza Mradi ili udumu"

"Mwaka 2012, Katikati ya Misagala na Kilosa kwenye Reli ya zamani ya MGR palijengwa daraja miaka 12 iliyopita, kutoka Daraja lilipo mpaka maji ya mto ilikuwa ni Mita 20 lakini leo udongo umetoka milimani umeshuka kwenye mto, mto umejaa tope ambapo mvua ikinyesha kubwa maji yatajaa kwenye Reli. Tusiruhusu hii ikatokea kwenye SGR. Tuweke Sera nzuri ya kulinda Mazingira na miradi ya SGR ikiwezekana iwepo asilimia kadhaa inayotoka kwenye mapato ya SGR ikasimamie Mazingira"

"Ukarabati wa Reli ya Ruvu - Tanga na Tanga - Arusha, hii ni Reli pekee iliyopo mikoa ya Kaskazini kwa maana ya Tanga, Arusha, Manyara na Kilimanjaro. Ni Reli iliyobeba uchumi mkubwa. Ruvu - Tanga ni KM 268 na Tanga - Arusha ni KM 438 lakini Serikali haiifanyii Ukarabati Reli hii. Tuna Viwanda vya Saruji Tanga, ambayo ikisafirishwa kwa Reli inapunguza gharama za usafirishaji kwa asilimia 40, tungeokarabati Reli hii leo tusingekuwa tunalia na bei kubwa na Saruji"

"Ni jambo la ajabu sana ikifika wakati wa Christmas tunaanza kukarabati Reli kupeleka watu mikoa ya Kaskazini. Hii ni Reli ya Kubeba mizigo na siyo Reli ya kupeleka watu Christmas. Tumefanya uwekezaji mkubwa Bandari ya Tanga na sasa tunajenga Gati Namba 3 kwaajili ya Makasha ya Shehena (Container). Tukikarabati hii Reli itakuwa rahisi kubeba mzigo kutoka Bandari ya Tanga mpaka Bandari ya Kware kwa urahisi kwa kutumia Reli"

"Kinachotakiwa ni kuyaimarisha madaraja yaweze kubeba mzigo mkubwa. Tukaondoe Reli zilizochakaa (Mataluma tuweke mengine) ili Treni kwenye Reli iweze kutembea Mwendokasi wa Kilomita 60 kwa Saa moja. Hivi sasa inatembea Kilomita 20 kwa saa moja. Inatumia masaa 10 - 12 kutoka Tanga - Dar es Salaam"

"Mamlaka ya Bandari (TPA) ni lazima tuwawezeshe. Ipo sheria tulitunga inatwa The Treasurer Registrar Powers on the Functions Act. 370 ambayo inampa Hazina kupitia Msajili wa Mashirika uwezo wa kutoza makusanyo ghafi kutoka kwenye makampuni na Mashirika ya Umma asilimia 15. Kwa mapato ya ziada anapewa Msajili wa Hazina kutoza asilimia 70. Asilimia 15 ya Mapato ghafi na asilimia 70 ya mapato ya ziada yalikuwa yanatosha kabisa kwa Serikali kuchukua mapato kwenye Mashirika haya"

"Tuwaachie watu wa bandari (TPA) wakusanye mapato wao wenyewe lengo watengeneze BalanceSheet zao vizuri ili waweze kukopa na kuendeleza Gati mbalimbali. Hii itasaidia kuwapunguzia mzigo Serikali." - Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo, Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini
 

Attachments

  • maxresdefaultmnbvgt.jpg
    maxresdefaultmnbvgt.jpg
    111.7 KB · Views: 2
Back
Top Bottom