Mbona kama tatizo la wateja katika benki kupata noti pungufu wanapotoa hela linaota mizizi?

Mkuu, kuna bank ukianza kutoa kuanzia million hata 2 unapatiwa kibunda tayari kimeshapigwa rababendi. Hakihesabiwi kwenye mashine. Utahakiki wewe mwenyewe. Nafuu millioni 2.

Ukitoa kuanzia millioni 10 mpaka 20 mpaka 30 utaitwa ndani utapewa kibunda chako kimeshapigwa utepe wa BOT n.k

Au labda mimi sielewi. Unaweza ukaomba wakuletee mashine uzihakiki pale pale au inakuwaje?
Unamwambia zihesabu. Atafungua na kuhesabu hana mamlaka ya kukataa. Pale pameandikwa mteja hesabu hela zako kabla hujaondoka kaunta ni haki yako. Na akikwambia sogea wateja wemgine wahudumiwe muoneshe hilo tangazo kuwa uhakika kabla ya kuondoka kaunta.
 
Mwaka 2016 nipo Tanga kaka yangu alikwenda kukopa 12million sasa akabeba ule mzigo mpaka home,na wala hakuhangaika nao.

Sasa kesho akachomoa kibunda akanipa ili niende kwa wakala nimuwekee tigo pesa amtumie mtu,nami sikihangaika kihesabu.

Alcohol,nikampa wakala anahesabu zipo 750,000 badala ya million moja,nikarudi mpaka home nikamwambia huu mzigo haukuenea ikabidi tukaanza kuchambua lile bunda tumekuta 500,000 haipo,maana imekuwa million 11.5
 
Salamu Wakuu,

Nimegundua Suala la uaminifu bado ni changamoto kubwa sana hapa nchini

Hivi karibuni kumekuwa na malalamiko mengi ya watu kupatiwa fedha pungufu kila wakichukua hela kupitia kwa benki tellers

Katika mjadala unaondelea huko X inaonesha kuna benki ambazo zinahusishwa na tabia hii mbaya. Yaani kwao matukio ya aina hii ni kawaida kwao

Na mara nyingi imekuwa nguvu kwa mtu kugundua kama ameibiwa kwa sababu Watanzania ni wavivu wa kuhesabu hela zao mara baada ya kuwithraw

Swali langu ni je, kwa nini kama benki na tellers wenye tabia hii mbovu hawachukuliwi hatua?

Haya ni malalamiko ya mteja kutoka Mtandao wa X

"Hivi ni mimi tu nikienda bank kutoa pesa kuanzia 10M huwa nakuta pungufu ya noti? Mfano unakuta kibunda kimoja kina noti 96-97 badala y amia? Na imeshatokea zaidi ya mara nne. Kuna siku nikiwa Mafinga napakia mbao nilikuta kwenye kibunda kimoja kimepelea noti 13 badala ya mia, nikajua labda nimejichanganya.

"Leo tena nipo Mafinga napakia mbao nimetoa zaidi ya 12M, jioni nawalipa wenye mzigo kibunda kimoja nakuta kina noti 82 za elfu kumi badala y amia. Jamani inaumiza sana, sitaitaja ni bank gani lakini hii kitu inaniuma sana, kama haijawahi kukupata unaweza hisi ni ungo, ila omba sana isikutokee.

"Noti 97-98 nilikuwa nachukulia kaiwada, ila hii sasa Hapana kwa kweli.

"NB: Huwa natolea bank sio kwa wakala, mtu asije fikiria huwa natoa kwa wakala."
Hivi vijistori vya kutunga vya Twitter ndo unaichukua kama habari ya kureport hapa? Hauko serious bibi
 
Mwaka 2016 nipo Tanga kaka yangu alikwenda kukopa 12million sasa akabeba ule mzigo mpaka home,na wala hakuhangaika nao.

Sasa kesho akachomoa kibunda akanipa ili niende kwa wakala nimuwekee tigo pesa amtumie mtu,nami sikihangaika kihesabu.

Alcohol,nikampa wakala anahesabu zipo 750,000 badala ya million moja,nikarudi mpaka home nikamwambia huu mzigo haukuenea ikabidi tukaanza kuchambua lile bunda tumekuta 500,000 haipo,maana imekuwa million 11.5
Angetumia dakika 10-15 kuhesabu angeokoa 500,000/-. Tatizo watu kujifanya wamezoea hela.
 
Kuna mmoja pale NMB Uluguru branch, morogoro, kwenye bulk cash, mdada mmoja mweusi mbayaaa, zaidi ya mara mbili nikienda kuweka pesa lazima vibunda viwili au vitatu akwambie kuna hela angalau 80k zimepungua wakati pesa inahesabiwa kwa Bill counter dukani kabla haijapelekwa benki.

Nilianza kuwithdwal kidogokidogo within one month account ikabaki tupu.

Njia bora kwangu kwa sasa ni mobile money.
 
Kuhesabu 10M+ yote mbele ya Teller si utasababisha foleni juu ya foleni kama siyo mzoefu wa kuzifinya na mate yatakauka kinywani ubaki na makohozi.

Kipindi natumia NMB,kuwidraw zaidi ya 5M ilikuwa unaingia chamber kwa Meneja,sijajua kama ilikuwa matawi yote.

Nikiwaza uaminifu wa bank zetu kwa wasimamizi wa mirathi juu ya taarifa za pesa ambazo marehemu huacha kwenye account zao,nakosa furaha kabisa.

Bank haipaswi kuwa sehemu ya kutiliwa shaka kwenye suala la uaminifu.
 
Nimewahi kukutana na hii changamoto zaidi ya mara moja kwenye ile bank yenye blue blue
Mara ya kwanza ilipungua laki 1, yule teller alijua sitarudi. Akashangaa baada ya saa kadhaa narudi, but alinipa hiyo pesa na akasema niliondoka haraka nikasahau hiyo laki aliweka pembeni wakati pesa alizifunga pamoja, Ila nilielewa na sikutaka kumharibia maana alinichangamkia sana alipokua ananihudumia

Mara ya pili, ilipungua 20k, hii nikusamehe maana nilikuja kugundua baada ya siku kupita.

Mara ya tatu ni 30k ikaenda tena nayo ikawa ngumu kurudi sababu ilipita siku.
Mara ya nne....
Ni hii hii bank moja, sijawahi pata changamoto hii bank nyingine
Tatizo kuhesabu pesa hapo hapo dirishani ni ngumu sana
 
Back
Top Bottom