DOKEZO Mbeya: Wakili aelezea kilichotokea sakata la Mkurugenzi City Casino anayetuhumiwa kumnyanyasa kingono mke wa mtu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Suala la Mkurugenzi wa Kampuni ya City Casino raia wa Burgalia, Vasil Dosev Dimitrov kudaiwa kuwatishia kuwaua Wanahabari wawili waliokuwa wakifuatilia madai kuwa anatuhumiwa kumfanyia unyanyasaji wa kingono aliyekuwa mtumishi wake wakike ambaye pia ni mke wa mtu, uchunguzi bado unaendelea.

Tukio hilo lilitokea 8/04/2024, Usiku katika Kata ya Iyela Wilaya ya Mbeya Mjini mbapo inaelezwa Vasil alimchukua kwa nguvu mfanyakazi wake wa kike (RoseMary Martin Kijabilwa) na kwenda kumfanyia ukatili huo akipata msaada wa dareva wake katika hoteli moja maarufu hapa Jijini Mbeya.

MAELEZO YA POLISI
Wiki iliyopita, JamiiForums ilipomuuliza Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Abdi Isango alisema suala hilo lipo mikononi mwa Polisi na uchunguzi unaendelea.

Mei 15, 2024, alipotafutwa Kamanda wa Polisi Mkoa, SACP Benjamin Kuzaga akasema “Nilikuwa likizo, nipe muda nilifuatilie suala hilo.”

INADAIWA ASKARI POLISI WANATAKA SIMU ZA WAANDISHI WALIOTISHIWA
Upande wa pili Waandishi wa Habari waliotishiwa Maisha na mhusika, wameshafika Kituo cha Polisi Kati, Mbeya Mjini kutoa taarifa hiyo na kuambiwa upelelezi unaendelea.

Inadaiwa walitakiwa kuwasilisha sauti ambazo Vasil anasikika akiwatukana na kutoa vitisho, wakapatiwa lakini baadaye wakawaambia Waandishi hao kuwa wanatakiwa kukabidhi simu iliyotumika ili ikafanyiwe uchunguzi zaidi Jijini Dar es Salaam kwa madai kuwa Mbeya hawana teknolojia hiyo.

WAFANYAKAZI WA MKURUGENZI WA CASINO NAO WAMO
Baadhi ya Watumishi wa Vasil nao wamekuwa wakitumia ushawishi wao mara kadhaa kutaka kumalizana na Raymond na mkewe kimyakimya na mara kadhaa wamewataka wasifikishe suala hilo kwenye vyombo vya Habari.

Kuna sauti za Meneja wa Casino na Dereva wakisikika wakimtisha RoseMary kuwa hatakiwi Kwenda kushtaki kwamba yatamkuta makubwa, pia Dereva wa Vasil naye anasikika akimwambia Raymond kuwa watampa kiasi cha hela ili amalize suala hilo kimyakimya.

WAKILI WA RAYMOND AELEZEA
Alipotafutwa Wakili Ntegwa Mpinyagwa anayesimamia suala hilo upande wa RAYMOND anaelezea:

Mara ya kwanza nilipewa nafasi ya kutengeneza “Demand Notice” (Taarifa ya matakwa kutoka kwa mshtaki mtarajiwa kabla ya kufikia hatua ya kushtaki) na mteja wangu ambaye ni Raymond Valelian Mvande kuelekea kwa Vasil Dosev Dimitrov.

Mhusika tulimpa Siku 14 ili kuona kama anaweza kujibu chochote lakini hilo halikutokea, siku zikapita bila kupata mrejesho wowote na kilichokuwa kinafuata baada ya hapo ni kufungua kesi.

Baada ya hapo sikupata maelekezo kutoka kwa mteja wangu hivyo ndio maana sijafungua kesi mpaka sasa.

Maelezo ya mteja wangu ni kwamba alisema kuna kosa la ‘adultery’, kwa Kiswahili tunaweza kuita ‘kukamatana ugoni, kwamba huyu Vasil Dosev Dimitrov amemlazimisha kingono mke wa mteja wangu (RoseMary Martin Kijabilwa) na akataka kulipwa fidia kwa kosa hilo kiasi cha Tsh. Milioni 250.

Kama ingetokea upande wa pili (wa Vasil) angekubali mazungumzo basi yangefanyika.

Pia kama mteja wangu Raymond angekuwa na pesa akanilipa mchakato wa kuendelea na kesi ungefanyika.

Awali nilishiriki kuandika Demand kama msaada baada ya kuombwa na Karani ninayefanya naye kazi, sikuweza kufungua kesi bila malipo kwa kuwa huwezi kujua itachukua muda gani na inaweza kuharibu ratiba zangu.

MADAI KUWA AMEMZUNGUKA MTEJA WAKE
Sio kweli, nilizungumza na mteja wangu na kumwambia kama ana fedha ya kunilipa gharama za kufungua kesi tunaweza kuendelea, kwa kazi na kipato chake najua kunilipa ilikuwa ni suala gumu.

Kipato chake ni cha chini, nilimwambia alipe Tsh. Milioni 1 ili tufungue kesi lakini hilo likawa gumu kwake, labda kama anaweza kupata msaada wa kulipiwa taratibu nyingine zinaweza kuendelea.

Mimi nafanya kazi ki professional, siwezi kufanya kitu kama hicho, nimeshafahamu upande wake (mteja) siwezi Kwenda kuzungumza na upande wa pili, hilo haliwezi kutokea.
 
Back
Top Bottom