UZUSHI Mawingu yenye Mwonekano wa umbo la Yesu yaonekana Angani nchini Kenya

Baada ya tathmini, tumebaini kuwa taarifa hii ni ya uzushi
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Wakuu,

Nimekutana na Picha inayosambaa Mtandaoni imeniogopesha sana. Ni mawingu yenye mwonekano wa Yesu, ama kweli siku za mwisho zimefika.
1000023604.jpg
 
Tunachokijua
Aprili 7, 2024, Mwanasiasa wa Kenya, Mike Sonko alichapisha picha ya mawingu ikiwa na Mwonekano wa Yesu kwenye Mtandao wa X ikiwa na maneno yanayowataka watu waanze kutubu kabla hawajachelewa.

Kwa mujibu wa Sonko, picha hii ilikuwa imeonekana Aprili 6, 2024 soko la Oyuma, Kaunti ya Homabay.

Hadi JamiiCheck inaanza kushughulikia mada hii, ilikuwa tayari imetazamwa na watu zaidi ya 757,000 na zaidi ya maoni 1,400 yalikuwa yametolewa.

Ukweli wa Madai haya
JamiiCheck imefuatilia undani madai ya Sonko na kubaini kuwa hayana ukweli. Picha hii si halisi kama inavyodaiwa, imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya Akili Mnemba (AI).

Pia, utafutaji wa Kimtandao kwa kutumia Google Image Search umeeonesha kuwa pamoja na Sonko, zipo pia Akaunti zingine Mtandaoni zilizochapisha picha hii, mathalani hii, hii na hii.

Baadhi ya mambo unayoweza kutumia katika kugundua hili ni Kuangalia vivuli vya nyumba na watu, pamoja na mapungufu katika mwonekano wa watu 3 waliosimama upande wa kushoto wa nyumba yenye mabati ambapo mmoja hana miguu na mwingine hana kichwa.

Awali, Novemba 13, 2023, JamiiCheck iliwahi kutolea ufafanuzi jinsi Teknolojia ya Akili Mnemba (AI) inavyoweza kuiga uhusika kwa kuunda picha na sauti za watu wengine. Huu ni mfano halisi wa Matumizi ya teknolojia hiyo.
Kiuhalisia hakuna anaemjua yesu kwa sura kwahiyo epukeni matapeli,,, siku yenyewe yesu analudi wengi hawatamjua kabisa.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom