NADHARIA Matumizi ya Muda mrefu ya Dawa za uzazi wa Mpango husababisha kuzaa watoto wa Kiume wenye homoni za Kike

Taarifa hii ni nadharia tu, tumeitolea ufafanuzi kwa kadiri ilivyowezekana
Miaka ya hivi karibuni, matumizi ya dawa za uzazi wa mpango (Vidonge na Sindano) yameongezeka sana, hali inayozua wasiwasi wa usalama wake miongoni mwa watumiaji.

Baadhi wameonesha wasiwasi wao kuwa dawa hizi husababisha kupata watoto wa kiume wenye homoni nyingi za kike, au hata kupata watoto wa kike wenye kiasi kikubwa cha homoni za kike hivyo kuwafanya wakomae mapema kabla ya umri sahihi.

Mathalani, mdau mmoja wa JamiiForums.com amekiri kuwahi kusikia kuwa matumizi ya muda mrefu ya dawa hizi yanaweza kusababisha mama kupata binti ambaye akifikisha umri wa miaka 8 matiti yake yanaweza kuwa makubwa, yaliyolala.

1F6D63B3-752C-43D3-9C0B-D5B88F422561.png

Ukweli kuhusu athari za dawa hizi ukoje?
 
Tunachokijua
Ili matumizi ya dawa yoyote yenye kiambato hai (Active Ingredient) yaweze kuthibitishwa, Mamlaka ya Dawa na Chakula ya Marekani (FDA) ikishirikiana na Shirika la Afya Duniani husisitiza upitiwaji wa hatua 5 muhimu ambazo pamoja na malengo mengine, hupanga kupima ufanisi wa dawa husika, madhara ya muda mfupi na mrefu, dozi na uhifadhi wake.

Kupitia mchakato wa ufuatiliaji wa dawa au kifaa tiba kikiwa sokoni yaani Postmarketing surveillance ambao hulenga kupima madhara wanayopata watumiaji, Wazalishaji pamoja na Mamkala za Afya kwenye kila nchi hushirikiana kwa pamoja kufuatilia mwendendo wa athari ili kuboresha bidhaa, ikiwezekana hata kuondoa sokoni bidhaa husika ikiwa madhara yatabainika kuwa ni makubwa kuliko iliyotarajiwa.

Dawa za uzazi wa mpango zilizopo mtaani zimepitia hatua zote 5 zilizowekwa na FDA ikishirikiana na WHO, pia mchakato wa ufuatiliaji wa athari zinazowapata watumiaji unaendelea kwa kuwa ni zoezi endelevu.

Hadi sasa, hakuna taarifa zozote zinazoonesha kuwa matumizi ya muda mrefu ya dawa hizi husababisha kuzaliwa kwa watoto wenye changamoto za homoni mwilini mwao.

Kwa mujibu wa Mamlaka kadhaa za afya ikiwemo wazalishaji, WHO, FDA pamoja na tafiti mbalimbali, maudhi madogo yanayoweza kuonekana kwa kutumia dawa hizi ni-
  • Kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi na kutokwa na damu katikati ya mzunguko
  • Maumivu ya kichwa
  • Kiungulia
  • Kuwasha kwa matiti
  • Kuongezeka kwa uzito wa mwili
  • Mabadiliko ya kihisia na mihemko ya mwili
Madhara ya Muda mrefu
  • Kwa mujibu wa Taasisi ya Taifa ya Saratani (NCI), husaidia kupunguza hatari ya kuugua saratani ya Kizazi, Ovari na utumbo mpana. Lakini, NCI wanaonya kuwa huongeza nafasi ya kuugua saratani ya Matiti
  • Kwa baadhi, husababisha kuganda kwa damu hivyo kuongeza hatari ya kupatwa na kiharusi na mshituko la moyo
Kutokana na kukosekana kwa ushahidi wowote wa kitafiti unaothibitisha madai haya, JamiiForums imeshindwa kuthibitisha madai haya hivyo inayachukulia kama nadharia.

Dawa nyingi za uzazi wa mpango zinazotumika kwa muda mrefu hutengenezwa kwa utaratibu uliodhibitwa, unaoruhusu ufyonzwaji mdogo wa viambato hai unaotosha kukidhi mahitahi ya muda mfupi, ndio maana baadhi ya dawa hizi bila kujali zimetumika kwa muda gani, mwanamke asipotumia kwa wastani wa siku 3 pekee anaweza kupata ujauzito.

Kitendo hiki huashiria kuwa mwanamke husika hajakingwa vya kutosha, pia dawa iliyobaki ipo kwenye dozi ndogo isiyo na uwezo wa kuleta athari zozote kwa afya.
Miaka ya hivi karibuni, matumizi ya dawa za uzazi wa mpango (Vidonge na Sindano) yameongezeka sana, hali inayozua wasiwasi wa usalama wake miongoni mwa watumiaji.

Baadhi wameonesha wasiwasi wao kuwa dawa hizi husababisha kupata watoto wa kiume wenye homoni nyingi za kike, au hata kupata watoto wa kike wenye kiasi kikubwa cha homoni za kike hivyo kuwafanya wakomae mapema kabla ya umri sahihi.

Mathalani, mdau mmoja wa JamiiForums.com amekiri kuwahi kusikia kuwa matumizi ya muda mrefu ya dawa hizi yanaweza kusababisha mama kupata binti ambaye akifikisha umri wa miaka 8 matiti yake yanaweza kuwa makubwa, yaliyolala.


Ukweli kuhusu athari za dawa hizi ukoje?
Hilo LA kubadilika kwa hisia ni tatizo sn. Mwanamke hupoteza kabisa mvuto/hamu ya tendo LA ndoa.
 
Hakuna kitu kigumu duniani kama kuzuia uzazi,wanawake wanalijua hilo

Naamin sasa tumeumbwa ili tuijaze dunia
 
Jamii Doctors naomba msaada wenu nimekuwa nikisia kutumia vidonge vya kuzuia mimba vya P2 vinapelekea kuzaa mtoto mwenye hormones nyingi za kike.

Sasa baada ya kukutana na hili andiko mtandaoni nimechanganyikiwa kabisa.



Naomba kueleweshwa je ni kweli na kwa vipi?
Kwanza nikushauri tu usipende kutumia p2 hvo vidonge ni hatari sana hususan kama hujaanza kuzaa bado tumia calender, au weka kitanzi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom