Mashindano ya uvuvi ni balaa

Mundele Makusu

JF-Expert Member
Sep 28, 2021
894
1,324
Katika Nchi ndogo iliyopo Ulaya iitwayo Montenegro, mashindano ya kumtafuta Mtu mvivu zaidi hufanyika kila mwaka na mwaka huu washindani saba wamejilaza kwenye mikeka wakipambania kombe hilo katika jitihada za kuvunja rekodi ya awali ya saa 117 iliyowekwa mwaka jana katika kijiji cha mapumziko cha Brezna na Mshindi atapewa Euro 1000 (Tsh. milioni 2.68).

Sheria za mashindao hayo zinasema kusimama wima au kukaa kunachukuliwa kama ukiukwaji wa sheria hizo na sababu za kutolewa mchezoni hivyo Washiriki wanatakiwa kujilaza wakati wote lakini Washiriki wanaruhusiwa kuwa na dakika 10 kila baada ya saa nane za kwenda chooni.

Washindani wanaweza pia kusoma, kutumia simu zao za mkononi pamoja na laptop zao, shindano hilo lilianzishwa miaka 12 iliyopita ili kusaidia kuondoa sifa maarufu ya Watu wanaotokea maeneno hayo kuwa ni wavivu, Washiriki saba wamejilaza chini kwa saa 463 kufikia jana.

Mshiriki Filip Knezevic (23) kutoka Mji wa Mojkovac, amesema ana uhakika wa ushindi na kunyakua tuzo ya euro 1,000 “Tuna kila kitu tunachohitaji hapa, kampuni ni nzuri, wakati unakwenda haraka”

View attachment 2744006

#HII IMEENDA
 
Back
Top Bottom