Marekani: Mwanamichezo kutoka Afrika Kusini apigwa risasi na Polisi na kufariki

STRUGGLE MAN

JF-Expert Member
May 31, 2018
8,638
16,569
Hasira zaenea baada ya polisi Marekani kumuua mwanamichezo wa Afrika Kusini.

Kifo cha mchezaji wa mpira wa rugby wa Afrika Kusini, Lindani Myeni akiwa mikononi mwa polisi huko Honolulu, Marekani, kimeibua ghadhabu na hasira kali miongoni mwa watu wa Waafrika Kusini.

Kumefanyika maandamano ya kulaani mauaji hayo huku wananchi wakitaka haki itendwe. Mwanamichezo huyo ambaye hakuwa na silaha, alipigwa risasi na polisi tarehe 14 mwezi huu. Msemaji wa Chama tawala nchini Afrika Kusini ANC Pule Mabe amelaani vikali mauaji hayo, akitoa wito wa kufanyika uchunguzi wa kina kuhusu mauaji hayo.

Amesema ANC inaamini kuwa serikali ya Afrika Kusini itafanya kila kinachowezekana kupata ripoti kamili kutoka kwa mamlaka za Marekani kuhusu mazingira yaliyosababisha kifo cha Bw. Myeni akiwa mikononi mwa polisi.

Aidha wafuasi wa chama cha tatu kikubwa zaidi Afrika Kusini EFF wamefanya maandamano nje ya ubalozi wa Marekani mjini Pretoria kupinga mauaji ya Myeni.

Kiongozi mwandamizi wa EFF Ngopile Mhlongo amesema serikali ya Marekani imejengeka katika misingi ya ubaguzi wa rangi au apatheidi na imekuwa ikimhujumu mtu mweusi kote barani Afrika

Habari zinasema, Myeni aliuawa wakati wa makabiliano na polisi wa Hawaii, ambao wanasema walichukua hatua baada ya kupigiwa simu ya tukio la wizi. Mke wake mwendazake amesema atafungua mashtaka dhidi ya polisi kwa kitendo hicho cha jinai.

Ukatili na unyama usio na mpaka wa polisi wa Marekani dhidi ya watu wenye asili ya Afrika ulimulikwa zaidi kimataifa baada ya mauaji yaliyofanywa na polisi mzungu, Derek Chauvin dhidi ya raia mweusi wa nchi hiyo, George Floyd hapo tarehe 25 Mei mwaka jana katika mji wa Minneapolis kwenye jimbo la Minnesota.

4by03f88446a7b1v3q5_800C450.jpg
 
Marekani ni taifa kubwa kulinda haki na utu wa binadamu, hata kilichofanyika ni sehemu ya kulinda haki za binadamu, acheni wazilinde.
 
Waafrica bana ni vibaka afu wakiuliwa wanapiga kelele fanyeni kazi... kama ubaguzi hatusikii Willy Smith kauliwa au Rebron James huyo Froyd alikuwa Teja na kibaka mzoefu Imefikia hata Media zinaogopa kuwaanika vibaka
 
Watu mmnajifanya mnajua kuliko kawaida, mmnajua gang za Waitaliano, walatino, wazungu zipo kibao huko America but still mweusi ndio anaonekana muovu zaidi.

By the way, taarifa inajitanabaisha kabisa huyo ni mcheza Rugby wa South Africa, Hawaii atakuwa alikwenda kula bata sasa kumuhusisha na maGang ya wamarekani wapi na wapi,....tatizo lipo Marekani, raisi wao mwenyewe amekubali, sasa nyie watu wa Tandale kwa tumbo mnapata wapi huu ujasiri wenu wa kuropoka utopolo?...
 
Mtu hadi leo bado analaani tukio lile shambulizi kwa Lissu ila akisikia matukio kama hayo huko America anasema watu weusi ndio wakorofi.
 
Marekani ni taifa kubwa kulinda haki na utu wa binadamu, hata kilichofanyika ni sehemu ya kulinda haki za binadamu, acheni wazilinde.

Kumtoa Gaddafi madarakani ni kulinda haki za binadamu.
Na kwamba kiwango cha haki za binadamu nchini Libya kimekuwa bora kwa sasa kuliko kipindi cha Gaddafi.
 
Back
Top Bottom