Mara nyingine maisha ya ndoa ni Vita. Huyu jamaa sijui nimfanyeje?

Rabboni

JF-Expert Member
Apr 6, 2015
983
1,281
Nawasalimu sana Wakuu. Straight to the point.

Nimeoa takribani miaka 9 imepita sasa. Nikiri sijawahi kuwa na mgogoro mkuubwa kivile kwenye ndoa yangu. Zaidi ya zile confusion za hapa na pale.

Mke wangu anafanya kazi kwenye moja ya taasisi ya Afya, ya Serikali. Sehemu ambayo alianza kazi, miezi miwili tu! Baada ya kumuoa.

Namwamini sana wife wangu kwa kweli, ila kuna utata umeibuka over recently na ndio maana naandika hapa, kuongezewa hekima na Busara kutoka kwa wazoefu wa hii taasisi takatifu inayoitwa Ndoa.

Kuna jamaa anafanya kazi na mke wangu ila department tofauti na ninafahamu kuwa wanafahamiana tokea mwanzo as long as wamesoma pamoja, sema huyu jamaa alimtangulia wife kidogo. Na ni mtu tunayejuana ila hatuna mazoea kivile.

Shida inaanzia hapa huyu jamaa alimwomba wife, amsaidie pesa kidogo 1.5M kwa minajili yakumrudishia ndani ya siku chache na baada yakujieleza vizuri juu ya hilo hitaji lake wife hakuweza kumpatia yote so alimpa 900k, bila kunishirikisha akiamini jamaa hawezi kuacha kumrudishia.

Zikapita siku kadhaa, jamaa kimya, ikapita mwezi kimya. Ikabidi wife amuulize, jamaa akaanza kupiga chenga. Nakutoa sababu zisizo na maana tena. Hiyo pesa wife aliitoa kwenye akaunti yake, binafsi sikushtuka mapema.

Duuh, jamaa anaanza kumchombeza wife, kwa kumpiga sound za hapa na pale, mara anamwambia akitoka job aipitie hiyo pesa sijui lodge gani huko. Alijua kabisa wife hakunishirikisha kwenye ile pesa so hawezi kuniambia.

Juzi kati hapa wife alivyoona mizinguo inazidi ikabidi anipe picha kamili na misamaha mingi, simply kwasababu alimheshimu yule jamaa ambaye alikuwa anamwita Kaka.

Sijaamua kuingilia kati bado ila nimemwambia wife, awe serious kidogo hiyo pesa ipatikane, na nimeanza kumfuatilia huyu jamaa ili nimfahamu zaidi uwezo wake ili nijue nikiingilia kati nitampa adhabu gani.

Huu ni utapeli, kwa kweli. Nahitaji hekima na busara zenu juu ya hili jambo wadau.
 
Inawezekana walikuwa jamaa alikuwa anakula Apple lako sasa wife wako kakupa short stories . Inawezekana walikuwa wapenzi na walipeana hio hela kipindi ni wapenzi . pia huwezi kujua na wife wako hawezi kukuambia ukweli wote. Kuna kitu kikubwa kimejificha hapo inakubidi ufanye a research hata kwenye simu yake , workmates wake, class mates .pole pole ndio utasolve hio issue. Ukikurupuka utaumbuka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nimefurahi sana mpaka ulipofikia kusema mkeo kakuambia.ni uaminifu wa hali ya juu sana kwa mkeo.

Kutokukushirikisha sio tatizo kwa muktadha huo kwa sababu sio kwamba hakukushirikisha kwa sababu anataka kuchepuka nae laa,ila nadhani aliona ni jambo la mda mfupi tu na atarudisha.

Kikubwa ni kwamba mkeo muaminifu ndo mana akakupa mchongo mzima ulivyo.

Nachokushauri.

onana na jamaa kiustaarabu sana umuambie kwamba wewe na mkeo mlipanga mumkopeshe hizo pesa na ukazipata mbona huzirudishi?

Kwa sababu huyo jamaa anadhani kwamba kitendo cha mkeo kumkopesha hizo pesa basi ndo anafikiria ameshapendwa na anahisi anaweza kumlah kiulaini.

Na huwenda hakuwa na shida ila tu alitaka kuprove kwamba anatakwa na mkeo au laa.hivyo alijua akipewa atakuwa anatakwa na mkeo akinyimwa hatakiwi.hivyo hapo kapewa pesa na amejihakikishia kwamba anapendwa sasa anataka kuenda katika hatua ya pili ya kumlaaahhh.

Sasa kama anafahamu kwamba wewe hujui hilo deni lenu basi hiyo anachukua kama defence kwake ya kumzungusha shemeji yetu.si anajua wewe hujui na anajua kwamba mkeo akikuambia utamhisi vibaya kwa namna fulani,na hapo ndo anajihakikishia na kujisemea "hatomuambia mumewe hivyo hata nisimlipe hamna shida"

Onana nae wewe ili ajione bwege,aone kwamba mkeo alimchukulia kama amebanwa na shida tu na sio kwamba kazimiwaa,ajue kwamba kumbe mkeo alikaa na wewe mumewe mkajadili hilo jambo kinyume na ambavyo alikuwa anafikiria.

Then hapo msikilizie kwanzaa...asipolipa njoo fungua uzi tena tukuambie cha kufanya

N:B : mke kumuazima mtu pesa bila ya mume kujua huwa wanaume wengi tunahisi vibaya hasa aloazimwa akiwa mwanaume.ila kwa hilo usije kumhisi mkeo vibaya.
 
Inawezekana walikuwa jamaa alikuwa anakula Apple lako sasa wife wako kakupa short stories . Inawezekana walikuwa wapenzi na walipeana hio hela kipindi ni wapenzi . pia huwezi kujua na wife wako hawezi kukuambia ukweli wote. Kuna kitu kikubwa kimejificha hapo inakubidi ufanye a research hata kwenye simu yake , workmates wake, class mates .pole pole ndio utasolve hio issue. Ukikurupuka utaumbuka

Sent using Jamii Forums mobile app
Hilo la kula apple siyo rahisi mkuu, kwasababu jamaa inaonekana ndio anaanza kumfuatilia wife sasa.
Bahati nzuri wife alinionyesha conversations zao alipoanza kuifuatilia hiyo pesa.

Na hiyo hela ni nyingi kidogo, ambayo lazima ningeigundua tu.
Ingekuwa chini ya 300k ndio singeijua.
Na control vizuri mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzembe ni wewe ambaye unamruhusu mke wako kufanya maamuzi makubwa kama hayo bila kukushirikisha...
Inatakiwa umjengee tania ya kuwa anakwambia mambo ya muhimu kabla haafanya maamuzi..
Usimkataze kutoa msaada ulio ndani ya uwezo wake ila ahakikishe amekupa taarifa kabla hajatoa huo msaada..

Huyo jamaa uwezo wake ni mkubwa mdomoni pia inaonekana yupo smart kwani kumshawishi mke wako kutoa laki9 anamuazima kama shost yake sio jambo jepesi mzee
Umetumia busara kutokukurupuka,fanya uchunguzi wako kwa kina utapata majibu kwanini jamaa anamzungusha kulipa hiyo
 
Kiafrika afrika ni 0.0001 ℅ ya mwanamke (tena mke wa mtu ndoani miaka 9!!!) kukubali kumkopesha mwanaume pesa yote hiyo kimya kimya bila hata kumshirikisha mumewe halali kbs wa ndoa. Kama bado hajat*mbwa basi muda si mrefu anaenda kutiwa na huyo jamaa yake.
Nisingeambiwa mkuu.
Naheshimina sana na mke wangu.
Huyu jamaa alimwaminisha kumlipa on time. Na wife aliona haina shida.
Amenieleza kila kitu tena kwa ushahidi.
Namwamini mke wangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanini asikushirikishe tangu mwanzo alipokopwa hiyo hela? aje kukushirikisha baada ya mdeni kumzungusha!

Ni jambo jema na zuri sana kumuamini mkeo, japo sidhani kama yeye anakuamini, huenda ndio sababu hakutaka kukushirikisha kabla ya kuigawa hiyo hela yake.
Hata mimi nilihoji hilo swali kwa wife...
Aliniambia tu nilimwamini Sana kaka Niko!
Na ile haraka yake, akaona haina haja ya kunishirikisha as long as alimwamini.
Mistake yake ni ile kutosema hata baada ya kumpa, hilo kosa amelikiri na kuomba msamaha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usiskilize maneno ya wale wanaokuambia mkeo alikuwa na mahusiano.
Kuna mambo kwenye ndoa ukiingiza wasiwasi mwingii basi ndoa hainogi na inakuwa haina amani.
Nisingeambiwa mkuu.
Naheshimina sana na mke wangu.
Huyu jamaa alimwaminisha kumlipa on time. Na wife aliona haina shida.
Amenieleza kila kitu tena kwa ushahidi.
Namwamini mke wangu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usifatilie hiyo pesa yao wala usimsaidie kudai. Huo ni uzwazwa. Ni tabia mbovu sana ya wanawake kufanya deal kimya kimya wakishaharibu ndio wanarudi kuomba msaada. Kisa tu ile kujiona anatumia hela zake mwenyewe.

Kuna 1 alinunua kiwanja, kiwanja kina mgogoro na kesi imefika mahakamani ndio anamwambia mumewe.

Basi ujue kuna siku mkeo atafanya jambo kubwa zaidi ya hilo.

Wewe mwambie live kuwa hufuatilii ujinga wake. Ila fuatili mienendo yake. Asijekuliwa bure.
 
Usifatilie hiyo pesa yao wala usimsaidie kudai. Huo ni uzwazwa. Ni tabia mbovu sana ya wanawake kufanya deal kimya kimya wakishaharibu ndio wanarudi kuomba msaada. Kisa tu ile kujiona anatumia hela zake mwenyewe.

Kuna 1 alinunua kiwanja, kiwanja kina mgogoro na kesi imefika mahakamani ndio anamwambia mumewe.

Basi ujue kuna siku mkeo atafanya jambo kubwa zaidi ya hilo.

Wewe mwambie live kuwa hufuatilii ujinga wake. Ila fuatili mienendo yake. Asijekuliwa bure.
Labda akamlie New York ama London

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwanaume ni mnyonge kama nyoka ukimmwagia mafuta ya taa au petroli.
Huyo mkeo bado ni mtu sahihi tu na endelea kumuamini. Kilichotokea hapo mtu yeyote huweza kufanya ikiwa tu yule mfanyiwa kuaminiwa kutokana na ahadi zake. Na inapotokea yale yasiyotarajiwa ndipo busara na ushauri huitajika. Pia mkuu tambua kuwa lingekuwa kosa zaidi km mkeo angechukua pesa zako kisha kumpa huyo jamaa.
Suala la unyoka kwa wanaume ni kuwa hawatakiwi kuaminiwa kwa asilimia 40. Ikiwa huyo mwanaume si baba yake, kaka yake au ndugu yake wa damu. Vinginevyo vilio km hv havitokauka.
 
Back
Top Bottom