SoC04 Maonyesho ya Kijeshi yajikite zaidi kwenye kuonyesha uvumbuzi wa silaha na vifaa vya kivita

Tanzania Tuitakayo competition threads

1idea

Member
Aug 18, 2022
11
10
Imekuwa ni jambo la kawaida kila mara zifanyikapo sherehe za kitaifa (Sherehe za Uhuru, Muungano na Mapinduzi ya Zanzibar) kuambatana na maonyesho ya kijeshi. Maonyesho haya yamekua yakionyesha mbinu kadha wa kadha wanazotumia wanajeshi wakiwa vitani. Ni jambo la kuvutia na kusisimua sana machoni kwa watazamaji hasa tuonapo wanajeshi na makomandoo wetu walivyo imara na shupavu kukabiliana na adui.

Umekua ni utamaduni mzuri sana wa kijeshi, lakini kuna vitu/ubunifu zaidi unakosekana kwenye maonyesho haya jambo ambalo limenipa shauku ya kuzungumzia upande wa sekta hii nyeti sana kwenye nchi yoyote duniani. Mambo yafuatayo yamenifanya bila hiyana kuweka kambi ya muda kwenye jambo hili.

Jambo kubwa kabisa ni kwamba dunia inabadilika
Kubadilika kwa dunia kunatokana na ukuaji wa kasi wa teknolojia. Kama dunia inabadilika nasi pia inaidi tubadilike tusitegemee kuna siku mabadiliko yatarudi nyuma la hasha.

Tunashuhudia kwenye maonyesho mengi ya kijeshi nchini ni marudio ya mambo mengi yaliyowahi kufanyika nyuma. Matukio kama ya uokoaji wa mateka, utulizaji wa vurugu, kushuka kwenye ndege na kamba, kupigana, kulala juu ya misumari, kupasuliwa tofali kifuani, kupasua tofali kwa kichwa/ngumi na mengineyo mengi yamekua yakirudiwa mara kwa mara.
Hii inaashiria maonyesho haya yameegemea sana kwenye kuonyesha ukakamavu wa mwili na mbinu za kukabiliana na adui ana kwa ana kuliko uvumbuzi wa kijeshi uliofanyika.

Lakini zama zimebadilika, kipindi cha nyuma vita nyingi villikua vya kupigana ana kwa ana, zama hizi watu hawapigani tena ana kwa ana, nchi zinarushiana makombora bila ya wanajeshi kutoka nje ya mikapa ya nchi yao (mfano Iran walichofanya kwa Israeli). Kwa maana hiyo majeshi mengi yamewekeza kwenye teknolojia ili kuvumbua zana nzito za kivita na namna ya kujikinga na zana nyingine za kivita.

Jambo lingine ni kukosekana kwa maonyesho ya vifaa/silaha za kivita zilizoundwa na jeshi lenyewe.
Kwenye maonyesho mengi yaliyopita, vifaa na silaha zinazotumika kwenye maonyesho zinaonekana ni silaha kutoka nje. Bunduki,ndege na magari vyote ni kutoka nje, hii inaonyesha jinsi gani tulivyo nyuma kuitumia teknolojia kuvumbua na kutengeneza vyakwetu.
Kutokana na hayo basi tubadilike, tubadilike kwa kufanya nini? Tubadilike kwa kuendana na teknolojia, tupambane tusibaki sana nyuma, tupambane kuvumbua vyakwetu.

Tuanze kwa kuvumbua vya kwetu, tutakavyojivunia navyo. Maonyesho ya kijeshi yajikite kwenye kujivunia uvumbuzi wa kijeshi upande wa silaha na vifaa vya vita.

Sio lazima kuanzia mbali, bali ni vyema kuanza na chochote. Maonyesho haya yatufanye tuwe na shauku ya kuona maonyesho ya sasa wamevumbua/wametengeneza nini? Au wameboresha kitu gani walichovumbua kwenye maonyesho yaliyopita.

Jeshi linaweza likaanza kwa kutengeneza vitu vidogo kama bunduki, hata zisipokua na uwezo mkubwa watakapoendelea kufanyia marekebisho huenda zikawa na nguvu zaidi hata ya zilizopo na zinazotumika.

Jambo hili ni jambo linalowezekana kwakua tumeshuhudia kama sio kwa kusikia baadhi ya raia nchini waliokamatwa na bunduki(gobole) walizotengeneza kienyeji. Kama imewezekana kwa raia wa kawaida kutengeneza bunduki bila shaka itawezekana kwa wanajeshi kuziboresha na kuziongezea uwezo zaidi.

Pia jeshi la anga lijikite kwenye uundaji ndege zisizo na rubani (drones) zenye uwezo wa kubeba mizigo na makombora madogomadogo. Hizi ndizo silaha za kisasa zinazotumika miaka ya sasa, lakini pia ndege hizo zinauwezo wa kupeleka misaada ya chakula na silaha iwapo kuna waliozingirwa na adui bila kuhatarisha maisha ya watu wanaoziongoza.

Jeshi lijikite pia kwenye kuonyesha wanyama waliopewa mafunzo ya kijeshi na wenye uwezo wa kusaidia kwenye uwanja wa vita. Wanyama kama mbwa na panya ni miongoni mwa wanyama ambao ni rahisi sana kuelewa wanapopatiwa mafunzo na wataalamu.

Mfano mwepesi tu kupitia panya Magawa, ambaye alikua ni panya mbobezi kutoka tanzania mwenye uwezo wa kugundua mabomu yaliyotegwa ardhini. Kutoakana na uwezo aliokua nao panya huyu aliweza kubaini mabomu mengi yaliyotegwa ardhini nchini Cambodia. Jambo hili lilimfanya atunukiwe medali ya dhahabu na shirika la matibabu ya wanyama la uingereza PSDA kwa kzi aliyoifanya. Hii inaonyesha ni kwa namna gani wanyama wakipatiwa mafunzo wanaweza kua na uwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi na haraka kuliko hata mwanadamu na vifaa vyake.

Ingawa mwanzo ni mgumu, lakini ikiwekwa nia kwenye jambo hili huenda siku za mbeleni wanajeshi wetu wakawa na uwezo wa kuunda silaha nzito za kivita iwe ni bunduki, mabomu, makombora, magari, meli na hata ndege za kivita. Jambo ambalo litaipa heshima jeshi letu na kupunguza kutegemea silaha nyingi na vifaa kutoka nje.

Tukitazama nchi zenye nguvu kubwa kijeshi duniani, Marekani, Urusi na china zimewekeza zaidi kwenye kuvumbua na kuunda silaha zao wenyewe jambo ambalo linachangia kwa kiasi kikubwa kuongeza nguvu zao kijeshi.

Kinachotakiwa ni serikali kuongeza bajeti kwenye sekta ya ulinzi. Na pia kusambaza wataalamu wa kijeshi kwenye nchi mbalimbali zenye uwezo mkubwa kijeshi kwa ajili ya kupata ujuzi. Hii itasaidia kupata ujuzi kutoka nchi mbalimbali na wataalamu hao watakapo ungana watajua wa pakuanzia.

Pia kuunda kamati tofauti tofauti za utafiti wa kijeshi, zitakazokua na wataalamu wabobezi. Hii itazisaidia kila kamati kujikita kwenye jambo lao moja, kulifanyia utafiti na kuja na uvumbuzi au maboresho kwenye jambo hilo.

Kwa kuhitimisha napenda niwapongeze jeshi kwa majukumu yao wanayofanya ya kulinda amani nchini na nchi jirani. Lakini kiujumla maoni haya ni kupenda kuona jeshi la Tanzania linafika mbali zaidi upande wa uvumbuzi na ubunifu wa vifaa vitumikavyo vitani ikiwemo silaha. Jeshi litakapoweza kujihudumia kwa baadhi ya silaha na vifaa itakua ni jambo la kufurahisha na kujivunia kwa nchi na pindi watakapowasilisha kwa raia kupitia maonyesho ya kitaifa.​
 
Jeshi letu livumbue nini kaka wakati siasa ishapenya hadi huko.

Chimbuko la sayansi katika mataifa mengi huanzia ndani ya majeshi - la kwetu ni gwaride mwanzo mwisho.

Tunahitaji kuwa na jeshi la kisasa - Jeshi linalovumbua Silaha mpya za kisasa kama Drones, missiles nk pia tuanze mkakati walau wa kurusha Settelite yetu kwa ajili ya mawasiliano yetu ya kijeshi. Suala la kujenga mtambo wa nyukilia pia tuanze tukitumia Urani tuliyopewa na Muumba.
 
Majeshi yooooote, yajikite kikamilifu katika uchumi.

Tuliambiwa na Hayati kwamba tupo katika vita ya kiuchumi mara kwa mara. Hapo ndipo tuwekeze nguvu kubwa sasa.

Majeshi ya na mitaji na nguvukazi ya kutosha kuweza kuadapt teknolojia na kutumia teknolojia kujenga uchumi.

Lakini wasiishie hapo tu wakishaiboresha wanaileta kwa wananchi ikishakuwa imesahilishwa kwa kutumika mwananchi wa kawaida. Rejea ARPANET hadi kuwa intaneti.

Military science, military intelligence ziwape kazi za kutafiti na kuendeleza (R n D) wasomi wote waliopo huko vitengoni. Sifa kitengo basi tunataka kila kitengo kituletee kitu kinachoistahilisha sifa yake.

Sio kuanzia mbali kwa suala la vitengo. Tunaweza hata kuanza na bendi za jeshi zituletee wimbo wa kitaifa hata kila baada ya miezi 3 - 6. Ambao sio kwa ajili ya vibe tu, bali uwe na ujumbe wa ajenda za kitaifa mfano, viwanda, ulinzi, uwajibikaji, kanuni, utaifa tukishindwa vyote basi tuburudike na chenja muruaaaa toka majeshini😅.

Wasiishie nyimbo, waje na kwenye filamu. Maana hata huyu mwananchi mleta mada anaweza kuwa ameandika haswa kwa mwitikio wa vitu alivyoshuhudia katika nchi nyingine kwa mtindo wa 'kiburudani' zaidi. Labda ameona muvi za FIGHTER au Operation Valentine akayashuhudia 'maonesho' ya stealth fighters/bombers kwenye video basi akatamani na anapoiona nchi yake ikionesha angalau ikaribie huko. Basi ni wakati wa Militaries kuanza kuhusishwa katika script na hadithi za muvi zetu. Jeshi liigize pia muvi zake kujenga morali. Tufuatilie hata namna Von Goebbel wa Hitler alivyozitumia media kupelekea ushindi kimedani na kisiasa.

Hamjawahi kufikiri hizi muvi zoote kwa nchi nyingine hutumika kama sehemu ua maonesho CO propaganda za nchi husika. Tujiulize sisi watanzania je tunachokiishi nchini ni kulia na kutangaza mateso ya mapenzi au nini?
 
Inashangaza kuona mwanajeshi wa tz anabeba beg la kilo 70 limejaa mawe sa inasaidia nini vitani?
Bado tupo nyuma sana, bado tunaendelea kuamini kua mwanajeshi ni kuvumilia mateso, na ndio maana utaona siku ya maonyesho wanajitahidi kuonyesha mazoezi magumu.
 
Jeshi letu kivumbue nini kaka wakati siasa ishapenya hadi huko.

Chimbuko la sayansi katika mataifa mengi huanzia ndani ya majeshi - la kwetu ni gwaride mwanzo mwisho.

Tunahitaji kuwa na jeshi la kisasa - Jeshi linalovumbua Silaha mpya za kisasa kama Drones, missiles nk pia tuanze mkakati walau wa kurusha Settelite yetu kwa ajili ya mawasiliano yetu ya kijeshi. Suala la kujenga mtambo wa nyukilia pia tuanze tukitumia Urani tuliyopewa na Muumba.
Kweli kabisa inabidi tutambue zama zimebadilika
 
Bado tupo nyuma sana, bado tunaendelea kuamini kua mwanajeshi ni kuvumilia mateso, na ndio maana utaona siku ya maonyesho wanajitahidi kuonyesha mazoezi magumu.
Ww komaa na magumu yako watu wanakupiga na kidrone tu wakiwa sebuleni
 
Mkuu umeongea jambo ambalo ndilo linalofanywa na mataifa makubwa duniani na si kama mawazo haya hayapo ndani ya vitengo vya kijeshi kama FIELD ENGINEERING. Tatizo kubwa tulilonalo ni limited budget; hayo uliyoyasema yote yanaitaji FUND ya kutosha sasa kwa nchi yetu hii ambayo inategemea misaada ya kifedha kwaajili ya kuzirun baadhi ya wizara tu ni shida.
Kumbuka wenzetu wanafanya haya kwaajili ya kuearn military prestige in the world tangia kuwepo kwa kambi kuu mbili ya magaribi na mashariki. Kwasisi bado Sana na tutaendelea kuona maonesho yaliyobase katika ukakamavu na vitu vingine vidogo dogo less otherwise yafutwe tu
 
Mkuu umeongea jambo ambalo ndilo linalofanywa na mataifa makubwa duniani na si kama mawazo haya hayapo ndani ya vitengo vya kijeshi kama FIELD ENGINEERING. Tatizo kubwa tulilonalo ni limited budget; hayo uliyoyasema yote yanaitaji FUND ya kutosha sasa kwa nchi yetu hii ambayo inategemea misaada ya kifedha kwaajili ya kuzirun baadhi ya wizara tu ni shida.
Kumbuka wenzetu wanafanya haya kwaajili ya kuearn military prestige in the world tangia kuwepo kwa kambi kuu mbili ya magaribi na mashariki. Kwasisi bado Sana na tutaendelea kuona maonesho yaliyobase katika ukakamavu na vitu vingine vidogo dogo less otherwise yafutwe tuma
Sidhani kama pesa inayohitajika ni kubwa kiasi hicho unachowaza, sio lazima kuanza kwa kutengeneza silaha nzitonzito.

Hivi hata mafunzo kwa wanyama, kutengeneza bunduki na drones ndogondogo inahitajika pesa kubwa kiasi hicho?.
 
Mkuu kama mfumo wa ufanyaji kazi wa bunduki tu kama SAR, SMG kutoka China, Korea Kusini na Urusi tunajua na muda mwengine tunazifanyia repairing zinazoharibika lakini so far hatutengenezi zetu huoni kwamba ile hali ya utegemezi bado inatutafuna sana? Tutaweza fikia kutengeneza drones zinazobeba siraha au kufanya uchunguzi katika anga la adui bila kugundulika?
Above all yote yanawezekana pale tutakapokuwa na NIA kwanza then UWEZESHAJI hakika tutafika.
 
Imekuwa ni jambo la kawaida kila mara zifanyikapo sherehe za kitaifa (Sherehe za Uhuru, Muungano na Mapinduzi ya Zanzibar) kuambatana na maonyesho ya kijeshi. Maonyesho haya yamekua yakionyesha mbinu kadha wa kadha wanazotumia wanajeshi wakiwa vitani. Ni jambo la kuvutia na kusisimua sana machoni kwa watazamaji hasa tuonapo wanajeshi na makomandoo wetu walivyo imara na shupavu kukabiliana na adui.

Umekua ni utamaduni mzuri sana wa kijeshi, lakini kuna vitu/ubunifu zaidi unakosekana kwenye maonyesho haya jambo ambalo limenipa shauku ya kuzungumzia upande wa sekta hii nyeti sana kwenye nchi yoyote duniani. Mambo yafuatayo yamenifanya bila hiyana kuweka kambi ya muda kwenye jambo hili.

Jambo kubwa kabisa ni kwamba dunia inabadilika
Kubadilika kwa dunia kunatokana na ukuaji wa kasi wa teknolojia. Kama dunia inabadilika nasi pia inaidi tubadilike tusitegemee kuna siku mabadiliko yatarudi nyuma la hasha.

Tunashuhudia kwenye maonyesho mengi ya kijeshi nchini ni marudio ya mambo mengi yaliyowahi kufanyika nyuma. Matukio kama ya uokoaji wa mateka, utulizaji wa vurugu, kushuka kwenye ndege na kamba, kupigana, kulala juu ya misumari, kupasuliwa tofali kifuani, kupasua tofali kwa kichwa/ngumi na mengineyo mengi yamekua yakirudiwa mara kwa mara.
Hii inaashiria maonyesho haya yameegemea sana kwenye kuonyesha ukakamavu wa mwili na mbinu za kukabiliana na adui ana kwa ana kuliko uvumbuzi wa kijeshi uliofanyika.

Lakini zama zimebadilika, kipindi cha nyuma vita nyingi villikua vya kupigana ana kwa ana, zama hizi watu hawapigani tena ana kwa ana, nchi zinarushiana makombora bila ya wanajeshi kutoka nje ya mikapa ya nchi yao (mfano Iran walichofanya kwa Israeli). Kwa maana hiyo majeshi mengi yamewekeza kwenye teknolojia ili kuvumbua zana nzito za kivita na namna ya kujikinga na zana nyingine za kivita.

Jambo lingine ni kukosekana kwa maonyesho ya vifaa/silaha za kivita zilizoundwa na jeshi lenyewe.
Kwenye maonyesho mengi yaliyopita, vifaa na silaha zinazotumika kwenye maonyesho zinaonekana ni silaha kutoka nje. Bunduki,ndege na magari vyote ni kutoka nje, hii inaonyesha jinsi gani tulivyo nyuma kuitumia teknolojia kuvumbua na kutengeneza vyakwetu.
Kutokana na hayo basi tubadilike, tubadilike kwa kufanya nini? Tubadilike kwa kuendana na teknolojia, tupambane tusibaki sana nyuma, tupambane kuvumbua vyakwetu.

Tuanze kwa kuvumbua vya kwetu, tutakavyojivunia navyo. Maonyesho ya kijeshi yajikite kwenye kujivunia uvumbuzi wa kijeshi upande wa silaha na vifaa vya vita.

Sio lazima kuanzia mbali, bali ni vyema kuanza na chochote. Maonyesho haya yatufanye tuwe na shauku ya kuona maonyesho ya sasa wamevumbua/wametengeneza nini? Au wameboresha kitu gani walichovumbua kwenye maonyesho yaliyopita.

Jeshi linaweza likaanza kwa kutengeneza vitu vidogo kama bunduki, hata zisipokua na uwezo mkubwa watakapoendelea kufanyia marekebisho huenda zikawa na nguvu zaidi hata ya zilizopo na zinazotumika.

Jambo hili ni jambo linalowezekana kwakua tumeshuhudia kama sio kwa kusikia baadhi ya raia nchini waliokamatwa na bunduki(gobole) walizotengeneza kienyeji. Kama imewezekana kwa raia wa kawaida kutengeneza bunduki bila shaka itawezekana kwa wanajeshi kuziboresha na kuziongezea uwezo zaidi.

Pia jeshi la anga lijikite kwenye uundaji ndege zisizo na rubani (drones) zenye uwezo wa kubeba mizigo na makombora madogomadogo. Hizi ndizo silaha za kisasa zinazotumika miaka ya sasa, lakini pia ndege hizo zinauwezo wa kupeleka misaada ya chakula na silaha iwapo kuna waliozingirwa na adui bila kuhatarisha maisha ya watu wanaoziongoza.

Jeshi lijikite pia kwenye kuonyesha wanyama waliopewa mafunzo ya kijeshi na wenye uwezo wa kusaidia kwenye uwanja wa vita. Wanyama kama mbwa na panya ni miongoni mwa wanyama ambao ni rahisi sana kuelewa wanapopatiwa mafunzo na wataalamu.

Mfano mwepesi tu kupitia panya Magawa, ambaye alikua ni panya mbobezi kutoka tanzania mwenye uwezo wa kugundua mabomu yaliyotegwa ardhini. Kutoakana na uwezo aliokua nao panya huyu aliweza kubaini mabomu mengi yaliyotegwa ardhini nchini Cambodia. Jambo hili lilimfanya atunukiwe medali ya dhahabu na shirika la matibabu ya wanyama la uingereza PSDA kwa kzi aliyoifanya. Hii inaonyesha ni kwa namna gani wanyama wakipatiwa mafunzo wanaweza kua na uwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi na haraka kuliko hata mwanadamu na vifaa vyake.

Ingawa mwanzo ni mgumu, lakini ikiwekwa nia kwenye jambo hili huenda siku za mbeleni wanajeshi wetu wakawa na uwezo wa kuunda silaha nzito za kivita iwe ni bunduki, mabomu, makombora, magari, meli na hata ndege za kivita. Jambo ambalo litaipa heshima jeshi letu na kupunguza kutegemea silaha nyingi na vifaa kutoka nje.

Tukitazama nchi zenye nguvu kubwa kijeshi duniani, Marekani, Urusi na china zimewekeza zaidi kwenye kuvumbua na kuunda silaha zao wenyewe jambo ambalo linachangia kwa kiasi kikubwa kuongeza nguvu zao kijeshi.

Kinachotakiwa ni serikali kuongeza bajeti kwenye sekta ya ulinzi. Na pia kusambaza wataalamu wa kijeshi kwenye nchi mbalimbali zenye uwezo mkubwa kijeshi kwa ajili ya kupata ujuzi. Hii itasaidia kupata ujuzi kutoka nchi mbalimbali na wataalamu hao watakapo ungana watajua wa pakuanzia.

Pia kuunda kamati tofauti tofauti za utafiti wa kijeshi, zitakazokua na wataalamu wabobezi. Hii itazisaidia kila kamati kujikita kwenye jambo lao moja, kulifanyia utafiti na kuja na uvumbuzi au maboresho kwenye jambo hilo.

Kwa kuhitimisha napenda niwapongeze jeshi kwa majukumu yao wanayofanya ya kulinda amani nchini na nchi jirani. Lakini kiujumla maoni haya ni kupenda kuona jeshi la Tanzania linafika mbali zaidi upande wa uvumbuzi na ubunifu wa vifaa vitumikavyo vitani ikiwemo silaha. Jeshi litakapoweza kujihudumia kwa baadhi ya silaha na vifaa itakua ni jambo la kufurahisha na kujivunia kwa nchi na pindi watakapowasilisha kwa raia kupitia maonyesho ya kitaifa.​
Unazungumzia kuunda kitu kipya au kukopi ?

Tanzania kuwa watu wenye wishful thinking, hakuna brains za kuunda au kubuni vitu vipya zaidi ya kukopi mambo waliyobuni wengine.
 
Ubunifu na weredi uliopo sekta binafsi, ni mkubwa kuliko serikalini, mathalani, niliwahi, kufanya kqzi voda, tigo, Airtel, kule wahandisi, wanachapa kazi kwa weredi sana, kutatua changamoto za kila siku, pale ttcl,wafanye wasifanye,salary ipo tu, hata kampuni isipoingiza mapato, mishahara itatoka hazina!wakati kwenye sekta binafsi, kampuni isipopata mapato,hapo ni redundancy, hakuna bonus, nk,
Sasa may be jeshi lingekuwa binafsi, ubunifu ungekuwa mkubwa, kilicho pale jwtz,wakuu wote wanawaza jinsi ya kupiga maokoto kwa njia halari na haramu! Wizi tu, kukusanya ukwasi, architecture, majumba, nk, unakuta eti na mtoto wa mabeyo nae anakimbizna kutafuta ajira za takukuru! Kwanini asiwe na kampuni ya kuagiza siraha kwa, ajiri ya nchi za, Burundi, Rwanda, Zambia nk!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom