Maoni yangu; Ni afadhali utoe namba yako ya siri ya benki au simu kwa ndugu kuliko kuificha kama tunavyoambiwa na benki, faida hupata wao zaidi ukifa

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,295
21,430
Ule ushauri wa mabenki na makampuni ya simu kwamba Namba yako ya siri ni siri yako usimpe hata unayemwamini ni mbaya sana!

Ukitaka kujua ule ushauri ni mbaya fatilia mirathi ya ndugu ndipo utajua ulikuwa hujui!

Hata ukifuata taratibu zote za mirathi usumbufu uko palepale,

kwanza usumbufu unaanzia mahakamani utaambiwa Mara hakimu hayupo, Mara nani yuko likizo, Mara fomu zimeisha subiri zije, Mara faili limepotea, Mara yule hakimu kahamishwa hajakabidhi ofisi, Mara hakimu yuko semina subiri hadi arudi n.k

Ukienda bank/ au makampuni ya simu hawakupi cash msimamizi wa mirathi, Wanakwambia Pesa Zitapitia Akaunti ya mahakama!

Na usifikilie kila mahakama ina akaunti yake,No; yaani pesa ni hadi iingie kwenye akaunti kuu, ndipo iombwe, ebu fikilia huo mlolongo usiokuwa na maana yoyote!

Fikilia kama kuna watoto watakiwa kulipiwa ada au kuna mambo ya kifamilia!
Inakuwaje kama Hizo pesa zitachukua zaidi ya mwaka? Na mafaili kupotea potea?

HIVI KWANINI WASINGEWEKA UTARATIBU RAHISI KWAMBA BAADA YA KIKAO CHA MIRATHI, familia ifungue akaunti na pesa ziwekwe huko chap kwenye akaunti ya familia?

Kiukweli Ni afadhali Utafte ndugu au mtoto mwaminifu umtajie password yako, Vinginevyo kwa utaratibu wa Kibongo Hakuna kitu utapata!

Uwezekano wa pesa nyingi sana za watu wanaokufa hupotelea hukohuko NA HAKUNA ANAEJALI!

Kwasababu wakubwa wao wakifa, benk, taasisi za fedha zinawapelekea Mafao na pesa zote BILA USUMBUFU! Bila kujazajaza mafomu kama RAIA!

NAKUSHAURI Ni afadhali ufiche kadi, lakini usifiche password hata kwa ndugu yako mmoja! Huko pesa za simu ndo sana zinapotea kabisa hizo lakilaki maana wengi wanaona bora ipotelee huko kuliko kupotezewa mda wa kwenda rudi kila siku
 
Pole sana kaka amefariki lini ndg, ni kweli mfumo huo ni hovyo kabisa mahakama wanasumbua sana kwasababu ni kacctimu fulani hivi hivyo ukikutana na karani ananjaaa akakunga nahakimu mwizi mwezake umekwisha kinachofanyika hapo balaa tupo lakini ukikutana na hakimu mwaminifu atakwambia kila kitu cha kufanya

Kibaya zaidi ukutana na karani uchwara
 
Yaani mda ote mafaili yanapotea, au hakimu anasafili!
Sijui hata mishahara walipwaga ya nini!

Zamanni niliamini mahakamani wanajiliwa watu waaminifu sana
 
Hili nimeliona 100% kabisa ulivyosema... yaan kama huna moyo unaacha na hapo umehisi mwaka ila sisi ilichukua miaka miwili karibu na nusu, tulifanikiwa ila kwa mbinde sana
 
Ukiacha tu masuala ya pesa pia unakuta mtu alikuwa yuko na akaunti kwenye mitandao ya kijamii bahati mbaya anapofariki akaunti inabaki tu ila angekuwepo wakujua namba za siri angeifuta kabisa..

Vema mtu ukaandika vitu vyako vyote hasa namba za siri za maeneo mbalimbali kwenye karatasi ukahifadhi mahali ili siku yakitokea yakutokea basi watu wako wa karibu waendelee ulipoachia wewe..
 
Hili nimeliona 100% kabisa ulivyosema... yaan kama huna moyo unaacha na hapo umehisi mwaka ila sisi ilichukua miaka miwili karibu na nusu, tulifanikiwa ila kwa mbinde sana
Can u imagine miaka miwili unafuatilia laki laki si wengi husamehe?
Kwanza kuna sababu gani kuzungusha namna hiyo?
Kuna matukio ya kutisha sana yaani hata sijui huko maofisini watu huwa wanalipwa kufanya nini
 
Tusiishie kwenye account za benki na simu pia ata umiliki wa assets zingine tusifanye siri. Unaweza mwambia rafiki / ndugu unayemwamini.
 
Yaani mda ote mafaili yanapotea, au hakimu anasafili!
Sijui hata mishahara walipwaga ya nini!

Zamanni niliamini mahakamani wanajiliwa watu waaminifu sana
eneo walilotakiwa kua na watu watiifu ni mahakamani ila ndo wamejazana wezi balaa na kila kitu kinasukwa na makarani
 
Huu unaitwa uwizi uwizini, Siri sio nzuri, vitu vingi vinapotelea kwa watu wengine, kweli kabisa.
 
Ule ushauri wa mabenki na makampuni ya simu kwamba Namba yako ya siri ni siri yako usimpe hata unayemwamini ni mbaya sana!

Ukitaka kujua ule ushauri ni mbaya fatilia mirathi ya ndugu ndipo utajua ulikuwa hujui!

Hata ukifuata taratibu zote za mirathi usumbufu uko palepale,

kwanza usumbufu unaanzia mahakamani utaambiwa Mara hakimu hayupo, Mara nani yuko likizo, Mara fomu zimeisha subiri zije, Mara faili limepotea, Mara yule hakimu kahamishwa hajakabidhi ofisi, Mara hakimu yuko semina subiri hadi arudi n.k

Ukienda bank/ au makampuni ya simu hawakupi cash msimamizi wa mirathi, Wanakwambia Pesa Zitapitia Akaunti ya mahakama!

Na usifikilie kila mahakama ina akaunti yake,No; yaani pesa ni hadi iingie kwenye akaunti kuu, ndipo iombwe, ebu fikilia huo mlolongo usiokuwa na maana yoyote!

Fikilia kama kuna watoto watakiwa kulipiwa ada au kuna mambo ya kifamilia!
Inakuwaje kama Hizo pesa zitachukua zaidi ya mwaka? Na mafaili kupotea potea?

HIVI KWANINI WASINGEWEKA UTARATIBU RAHISI KWAMBA BAADA YA KIKAO CHA MIRATHI, familia ifungue akaunti na pesa ziwekwe huko chap kwenye akaunti ya familia?

Kiukweli Ni afadhali Utafte ndugu au mtoto mwaminifu umtajie password yako, Vinginevyo kwa utaratibu wa Kibongo Hakuna kitu utapata!

Uwezekano wa pesa nyingi sana za watu wanaokufa hupotelea hukohuko NA HAKUNA ANAEJALI!

Kwasababu wakubwa wao wakifa, benk, taasisi za fedha zinawapelekea Mafao na pesa zote BILA USUMBUFU! Bila kujazajaza mafomu kama RAIA!

NAKUSHAURI Ni afadhali ufiche kadi, lakini usifiche password hata kwa ndugu yako mmoja! Huko pesa za simu ndo sana zinapotea kabisa hizo lakilaki maana wengi wanaona bora ipotelee huko kuliko kupotezewa mda wa kwenda rudi kila siku
True! Mi mwenyewe mhanga wa hii kitu mpaka nimesalenda nimewaachia voda pesa ya mirathi
 
Kuna mzee mmoja mwanajeshi bahili huyo hajui kutumia smartphone anaweza kukuita umuelekeze namna ya kutuma pesa, kila kitu unamfanyia ila linapokuja swala la kuingiza namba ya siri hamuamini mtu. Mpaka tulivyomuwekea screen recorder ndio tukafanikisha kujua namba yake ya siri

Muhimu kua na backup kwa mtu ambaye unamuamini, hata kama sio mkeo basi mteue mwanao mpendwa ambaye atakua na access na hizo accounts
 
Sina siri, one of them knows my passwords.

Wote wanajua wanachoambulia kwangu, mmoja na nyumba yake alishaiuza. namjengea room moja huku nje,..... siri ya nini ndo mnapata bp kisa unalinda account na hela yenyewe ipo kiduchu
 
Kuna mzee mmoja mwanajeshi bahili huyo hajui kutumia smartphone anaweza kukuita umuelekeze namna ya kutuma pesa, kila kitu unamfanyia ila linapokuja swala la kuingiza namba ya siri hamuamini mtu. Mpaka tulivyomuwekea screen recorder ndio tukafanikisha kujua namba yake ya siri

Muhimu kua na backup kwa mtu ambaye unamuamini, hata kama sio mkeo basi mteue mwanao mpendwa ambaye atakua na access na hizo accounts
Kabisa yaan
 
Back
Top Bottom