Manula ajaribu mitambo wakati Simba ikimuua Dar City goli nyingi

CAPO DELGADO

JF-Expert Member
Aug 31, 2020
7,617
16,712
ASUBUHI ya Jana Simba imecheza mechi ya kirafiki dhidi ya Dar City kwenye uwanja wake wa Mo Simba Arena, Bunju - Dar es Salaam na kuibuka na ushindi wa mabao 5-1, huku kipa wake Aishi Manula akirejea langoni.

Mchezo huo ni wa kwanza kwa Manula msimu huu kwani kabla ya hapo alikuwa nje ya uwanja akiuguza majeraha ya nyonga aliyoyapata Aprili 7, mwaka huu kwenye mechi ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (ASFC), dhidi ya Ihefu katika Uwanja wa Azam Complex.

Katika mchezo wa jana, Manula alianza langoni Simba akicheza kwa dakika 40, kabla ya kufanyiwa mabadiliko na nafasi yake kuchukuliwa na Hussein Abel ambaye naye bado hajapata muda wa kutosha kucheza ndani ya kikosi hicho tangu asajiliwe mwanzoni mwa msimu akitokea KMC.

Kurejea kwa Manula ni taarifa njema kwa Simba na mashabiki wake kwani kabla hajaumia alikuwa ni kipa namba moja wa kikosi hicho na alipoumia Simba ilisajili jumla ya makipa watatu, lakini hakuna hata mmoja aliyeonyesha kukamatia nafasi hiyo.

Simba ilianza kwa kumsajili Mbrazili Jefferson Luiz, lakini ilidaiwa alipata majeraha wakati timu ikiwa katika maandalizi ya msimu huu nchini Uturuki na kuachwa, kisha ikamsajili Abel ambaye hajacheza mechi ya mashindano na pia ikamsajili Mmorocco Ayou Lakred.
(KIPA WA MCHONGO WA MO)
kupiga ma BILIONI ya super League

Ally Salim na Ayoub (mdaka panzi) ndio wamekuwa wakipokezana kudaka kwenye mechi za Simba katika msimu huu huku wote wakionyesha kushindwa kuvivaa vyema viatu vya Manula langoni.

Huenda Manula akaanza kucheza mechi ya mashindano msimu huu katika mchezo wa ufunguzi wa michuano mipya ya African Football League dhidi ya Al Ahly utakaopigwa Oktoba 20, mwaka huu katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mabao ya Simba leo dhidi ya Dar City yalifungwa na Shaban Chilunda aliyecheka na nyavu mara mbili huku Luis Miquissone, Willy Onana na Saidi Ntibazonkiza kila mmoja akifunga moja.
 
Khaaaaw yani clean SHEET hakuna kwa timu kama Dar city simnawachezea nusu uwanja
Ukuta wa yeriko umekuwa ukuta wa guest kila mtu ruhusa kuegemea
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom