SoC02 Mambo ya kuzingatia ili kuweza kutajirika kwa kuwekeza kwenye soko la hisa

Stories of Change - 2022 Competition
Jul 19, 2022
11
33
Muhtasari:

Dhumuni la nakala hii ni kuelimisha jamii kuhusiana na kanuni za kuzingatia ili kuweza kutajirika kwa kuwekeza kwenye soko la hisa. Pia, kutoa hamasa kwa vijana na wajasiriamali mbalimbali kukuza mitaji na utajiri kwa kuwekeza kwenye soko la hisa la Dar es Salaam.

1660447488963.png

(Nembo ya Soko la Hisa la Dar es Salaam “Dar es Salaam Stock Exchange” pamoja na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana “Capital Market and Security Authority” (CMSA). Chanzo: https://www.cmsa.go.tz/ , https://dse.co.tz/)

Utangulizi:

Hisa ni nini? Hisa ni sehemu ndogo ya biashara inayowakilisha umiliki wa mtu/kampuni katika biashara hiyo. Soko la hisa ni taasisi ya serikali inayowawezesha wananchi wote pamoja na raia wa kigeni kununua na kumiliki kampuni kwa kununua hisa zake. Soko la Hisa la Dar es Salaam lilianzishwa mnamo tarehe 19, mwezi Septemba, mwaka 1996 chini ya Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA).

Hisa za kampuni kadha wa kadha huuzwa na kununuliwa kwenye soko la hisa kila siku. Mfano wa kampuni ambazo hisa zake zinapatikana kwenye soko la hisa la Dar es Salaam ni; CRDB, Dar Es Salaam Stock Exchange (DSE), National MicroFinance Bank (NMB), Swissport (SWISS), Tanga Cement Company Limited (TCCL), na kadhalika.

1660447882328.png

(Picha ya nembo za baadhi ya makampuni yaliyosajiliwa kwenye soko la hisa. Chanzo: Hifadhi ya maktaba ya picha google)

Kanuni ambazo matajiri huzingatia kabla ya kufanya uamuzi wa kununua au kuuza hisa:

1. Uwiano kati ya bei ya hisa na thamani ya hisa (Price to Value Ratio).

Kuna tofauti kati ya thamani na bei ya hisa. Bei ni kile unacholipa ili kuwa mmiliki wa hisa. Bei ya hisa hutegemea ugavi na uhitaji wa hisa (supply and demand). Thamani ni kile unachopokea kama mwekezaji baada ya kununua hisa. Thamani ya hisa hutegemea ukubwa wa mali (assets) na madeni (liabilities) katika biashara. Lengo kubwa la mwekezaji makini ni kutafuta biashara zenye mali nyingi kuliko madeni. Thamani ya biashara hupimwa kwa kuchukua mali (assets) za biashara toa madeni (liabilities) ya biashara hiyo. Kinachobaki huitwa mali wavu (net worth). Ukigawanya mali wavu (net worth) ya kampuni kwa idadi ya hisa zilizouzwa na kampuni hiyo, utapata thamani ya kila hisa moja. Kama thamani ya hisa moja ni kubwa kuliko bei ya hisa moja, inashauriwa kununua. Kwanini? Kwa sababu ni sawa na kununua kiwanja chenye mgodi wa dhahabu ndani yake kwa bei nafuu. Thamani unayopokea ni kubwa kuliko bei unayolipia. Thamani ikiwa ndogo kuliko bei, maana yake utalipia fedha nyingi kupata kitu chenye thamani ndogo.

1660448356677.png
1660448614367.png

2. Uwiano kati ya bei ya hisa na mapato kwa kila hisa moja (Price to Earnings Ratio).
Mapato katika muktadha huu ni faida baada ya kulipa kodi na riba. Mapato kwa kila hisa moja hupatikana kwa kugawanya mapato baada ya kodi na riba kwa jumla ya hisa zilizouzwa. Jibu litakalopatikana (mapato ya hisa moja) litatumika kugawanya bei ya hisa moja. Jibu litakalopatikana likiwa dogo(chini ya tano) litaashiria kwamba bei ya hisa ni nafuu na mapato kwa kila hisa moja ni makubwa(fursa ya kununua). Jibu likiwa kubwa (zaidi ya kumi) litaashiria kwamba bei ya hisa ni kubwa sana na mapato kwa kila hisa ni madogo (fursa ya kuuza na kutengeneza faida).

1660448916139.png
1660448968740.png

3. Mavuno ya gawio (Dividend yield) .
Gawio ni faida inayoingia mfukoni mwa mwekezaji. Mavuno ya gawio hupatikana kwa kuchukua gawio kwa hisa, gawanya kwa bei ya kununulia hisa mara asilimia mia. Jibu (asilimia) likiwa kubwa huashiria kwamba, kampuni inatengeneza faida kubwa na bei ya kununua hisa ni nafuu sana(fursa ya kununua). Jibu (asilimia) dogo huashiria kwamba, faida katika biashara hio ni ndogo au bei ya hisa ni kubwa sana (fursa ya kuuza).

1660449241631.png

4. Utendaji na mwenendo wa biashara pamoja na mazingira ya biashara
Mwenendo wa biashara huweza kupimwa kwa kuangalia vigezo vifuatavyo; Je? bidhaa inayouzwa inamatumizi makubwa kwenye jamii?, bidhaa itaendelea kutumika majira ya mbeleni?, je ni biashara halali?,ina ubunifu wa kutosha kuzidi biashara shindani?, inajali maslahi ya wateja,wafanyakazi pamoja na wadau wengine katika biashara hio?, je kuna uongozi bora? na kadhalika.

1660449572687.png

🤑💰💸 HADITHI YA MWANAFUNZI ANAYELIPWA HUKU AKISOMA SHULE 🤑💰💸

Kijana huyu anafahamika kwa jina la nadharia “Ukwasi". Ukwasi alitamani sana kukuza mtaji wake kwa kuwekeza kwenye biashara zenye kutengeneza faida na ambazo hazitagharimu muda wake wa masomo. Ukwasi akaanza kufuatilia jinsi ya kukuza mtaji kupitia soko la hisa na kujifunza kwa MABILIONEA waliotajirika kwa kuwekeza kwenye soko la hisa kama Charlie Munger, Benjamin Graham na Philip Fisher. Baada ya kuweka akiba kwa zaidi ya mwaka mmoja, Ukwasi akanunua hisa za benki ya CRDB kwa Tzs 100 mwaka 2019, hisa za Tanga cement kwa Tzs 1,100 mwaka 2021 na hisa za Swissport mwaka 2022 kwa Tzs 1,120. Hivi sasa yupo chuo akifaidi matunda ya jasho lake huku mtaji aliowekeza CRDB ukiwa umekua kwa 390%, mtaji aliowekeza Swissport umekua kwa 82% na mtaji aliowekeza Tanga Cement umekua kwa 35%. Licha ya hapo kila biashara hizo zikitengeneza faida anapata gawio kila mwaka. Anasoma kwa raha mustarehee!!!

1660451005118.png
1660451118971.png

(Picha za katuni zinazoashiria ukuaji wa fedha za Ukwasi kutokana na jitihada zake katika uwekezaji kwenye soko la hisa. Chanzo: https://www.vectorstock.com/royalty-free-vector/cartoon-savings-value-growth-money-profit-vector-27455969 , Rich Businessman Sleeping On Money Bags Cartoon Clipart Vector - FriendlyStock)

Tulipomuuliza siri ya mafanikio yake alitaja kanuni zilizoongelewa kwenye nakala hii hapo awali. Pia aligusia tabia ambazo zimemsaidia kufikia mafanikio hayo. Hizi ni pamoja na kuweka akiba, kujifunza kuhusu uwekezaji kwa kusoma nakala kuhusu biashara na uwekezaji na kusikiliza matajiri waliofanikiwa kwa kununua hisa. Cha mwisho na muhimu zaidi, alizungumzia kuhusu umuhimu wa kumuomba Mungu na uthubutu wa kuchukua hatua. Ukwasi anaamini kwamba kanuni pamoja na tabia hizi zitaweza kuisaidia jamii kuweza kuwa matajiri kwa kuwekeza kwenye soko la hisa.
 
Attachments

  • 1660448291006.png
    1660448291006.png
    19.4 KB · Views: 98
Muhtasari:

Dhumuni la nakala hii ni kuelimisha jamii kuhusiana na kanuni za kuzingatia ili kuweza kutajirika kwa kuwekeza kwenye soko la hisa. Pia, kutoa hamasa kwa vijana na wajasiriamali mbalimbali kukuza mitaji na utajiri kwa kuwekeza kwenye soko la hisa la Dar es Salaam.

View attachment 2323359

(Nembo ya Soko la Hisa la Dar es Salaam “Dar es Salaam Stock Exchange” pamoja na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana “Capital Market and Security Authority” (CMSA). Chanzo: https://www.cmsa.go.tz/ , https://dse.co.tz/)

Utangulizi:

Hisa ni nini? Hisa ni sehemu ndogo ya biashara inayowakilisha umiliki wa mtu/kampuni katika biashara hiyo. Soko la hisa ni taasisi ya serikali inayowawezesha wananchi wote pamoja na raia wa kigeni kununua na kumiliki kampuni kwa kununua hisa zake. Soko la Hisa la Dar es Salaam lilianzishwa mnamo tarehe 19, mwezi Septemba, mwaka 1996 chini ya Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA).

Hisa za kampuni kadha wa kadha huuzwa na kununuliwa kwenye soko la hisa kila siku. Mfano wa kampuni ambazo hisa zake zinapatikana kwenye soko la hisa la Dar es Salaam ni; Cooperative and Rural Development Bank (CRDB), Dar Es Salaam Stock Exchange (DSE), National MicroFinance Bank (NMB), Swissport (SWISS), Tanga Cement Company Limited (TCCL), na kadhalika.

View attachment 2323360
(Picha ya nembo za baadhi ya makampuni yaliyosajiliwa kwenye soko la hisa. Chanzo: Hifadhi ya maktaba ya picha google)

Kanuni ambazo matajiri huzingatia kabla ya kufanya uamuzi wa kununua au kuuza hisa:

1. Uwiano kati ya bei ya hisa na thamani ya hisa (Price to Value Ratio).

Kuna tofauti kati ya thamani na bei ya hisa. Bei ni kile unacholipa ili kuwa mmiliki wa hisa. Bei ya hisa hutegemea ugavi na uhitaji wa hisa (supply and demand). Thamani ni kile unachopokea kama mwekezaji baada ya kununua hisa. Thamani ya hisa hutegemea ukubwa wa mali (assets) na madeni (liabilities) katika biashara. Lengo kubwa la mwekezaji makini ni kutafuta biashara zenye mali nyingi kuliko madeni. Thamani ya biashara hupimwa kwa kuchukua mali (assets) za biashara toa madeni (liabilities) ya biashara hiyo. Kinachobaki huitwa mali wavu (net worth). Ukigawanya mali wavu (net worth) ya kampuni kwa idadi ya hisa zilizouzwa na kampuni hiyo, utapata thamani ya kila hisa moja. Kama thamani ya hisa moja ni kubwa kuliko bei ya hisa moja, inashauriwa kununua. Kwanini? Kwa sababu ni sawa na kununua kiwanja chenye mgodi wa dhahabu ndani yake kwa bei nafuu. Thamani unayopokea ni kubwa kuliko bei unayolipia. Thamani ikiwa ndogo kuliko bei, maana yake utalipia fedha nyingi kupata kitu chenye thamani ndogo.

View attachment 2323365 View attachment 2323366

2. Uwiano kati ya bei ya hisa na mapato kwa kila hisa moja (Price to Earnings Ratio).
Mapato katika muktadha huu ni faida baada ya kulipa kodi na riba. Mapato kwa kila hisa moja hupatikana kwa kugawanya mapato baada ya kodi na riba kwa jumla ya hisa zilizouzwa. Jibu litakalopatikana (mapato ya hisa moja) litatumika kugawanya bei ya hisa moja. Jibu litakalopatikana likiwa dogo(chini ya tano) litaashiria kwamba bei ya hisa ni nafuu na mapato kwa kila hisa moja ni makubwa(fursa ya kununua). Jibu likiwa kubwa (zaidi ya kumi) litaashiria kwamba bei ya hisa ni kubwa sana na mapato kwa kila hisa ni madogo (fursa ya kuuza na kutengeneza faida).

View attachment 2323367 View attachment 2323368

3. Mavuno ya gawio (Dividend yield) .
Gawio ni faida inayoingia mfukoni mwa mwekezaji. Mavuno ya gawio hupatikana kwa kuchukua gawio kwa hisa, gawanya kwa bei ya kununulia hisa mara asilimia mia. Jibu (asilimia) likiwa kubwa huashiria kwamba, kampuni inatengeneza faida kubwa na bei ya kununua hisa ni nafuu sana(fursa ya kununua). Jibu (asilimia) dogo huashiria kwamba, faida katika biashara hio ni ndogo au bei ya hisa ni kubwa sana (fursa ya kuuza).

View attachment 2323370

4. Utendaji na mwenendo wa biashara pamoja na mazingira ya biashara
Mwenendo wa biashara huweza kupimwa kwa kuangalia vigezo vifuatavyo; Je? bidhaa inayouzwa inamatumizi makubwa kwenye jamii?, bidhaa itaendelea kutumika majira ya mbeleni?, je ni biashara halali?,ina ubunifu wa kutosha kuzidi biashara shindani?, inajali maslahi ya wateja,wafanyakazi pamoja na wadau wengine katika biashara hio?, je kuna uongozi bora? na kadhalika.

View attachment 2323371

HADITHI YA MWANAFUNZI ANAYELIPWA HUKU AKISOMA SHULE

Kijana huyu anafahamika kwa jina la nadharia “Ukwasi". Ukwasi alitamani sana kukuza mtaji wake kwa kuwekeza kwenye biashara zenye kutengeneza faida na ambazo hazitagharimu muda wake wa masomo. Ukwasi akaanza kufuatilia jinsi ya kukuza mtaji kupitia soko la hisa na kujifunza kwa MABILIONEA waliotajirika kwa kuwekeza kwenye soko la hisa kama Charlie Munger, Benjamin Graham na Philip Fisher. Baada ya kuweka akiba kwa zaidi ya mwaka mmoja, Ukwasi akanunua hisa za benki ya CRDB kwa Tzs 100 mwaka 2019, hisa za Tanga cement kwa Tzs 1,100 mwaka 2021 na hisa za Swissport mwaka 2022 kwa Tzs 1,120. Hivi sasa yupo chuo akifaidi matunda ya jasho lake huku mtaji aliowekeza CRDB ukiwa umekua kwa 390%, mtaji aliowekeza Swissport umekua kwa 82% na mtaji aliowekeza Tanga Cement umekua kwa 35%. Licha ya hapo kila biashara hizo zikitengeneza faida anapata gawio kila mwaka. Anasoma kwa raha mustarehee!!!

View attachment 2323374 View attachment 2323377
(Picha za katuni zinazoashiria ukuaji wa fedha za Ukwasi kutokana na jitihada zake katika uwekezaji kwenye soko la hisa. Chanzo: https://www.vectorstock.com/royalty-free-vector/cartoon-savings-value-growth-money-profit-vector-27455969 , Rich Businessman Sleeping On Money Bags Cartoon Clipart Vector - FriendlyStock)

Tulipomuuliza siri ya mafanikio yake alitaja kanuni zilizoongelewa kwenye nakala hii hapo awali. Pia aligusia tabia ambazo zimemsaidia kufikia mafanikio hayo. Hizi ni pamoja na kuweka akiba, kujifunza kuhusu uwekezaji kwa kusoma nakala kuhusu biashara na uwekezaji na kusikiliza matajiri waliofanikiwa kwa kununua hisa. Cha mwisho na muhimu zaidi, alizungumzia kuhusu umuhimu wa kumuomba Mungu na uthubutu wa kuchukua hatua. Ukwasi anaamini kwamba kanuni pamoja na tabia hizi zitaweza kuisaidia jamii kuweza kuwa matajiri kwa kuwekeza kwenye soko la hisa.
Asante kwa maarifa haya. Mkuu hivi kwa uwiano wa bei ya hisa na thamani ya hisa za NMB ukoje?
 
Thank you bro …..Kwa kuelimisha Jamii yetu
 
UTT liquid fund unaongelea kile kinachoitwa UKWASI....hicho kipande kina sifa ya kukupa pesa kidogo kila baada ya mida flani..... sema ukuwaji wa bei ya kipande cha ukwasi ni mdogo kulinganisha na vipande ambavo havitoi faida bali inaviwekeza na kuvilimbikiza(compounding) tena kama kipande kinachoitwa UEWEKEZAJI
Shukrani kwa maelezo Yako mazuri, ni kweli almost Kila siku kunafaida kidogo inaonemana. Natakiwa nifanyie nini niweze kupata compound interest mfuko wa liquid . Kwa upande wa bond fund nao unaoparate vipi?. Nimfuko Gani unatengeneza compound interest? Na huo mfuko wa uwekezaji ndio upi?
 
Asante kwa maarifa haya. Mkuu hivi kwa uwiano wa bei ya hisa na thamani ya hisa za NMB ukoje?

Asane sana kwa swali zuri. NMB ni kati ya Benki zinazofanya vizuri sana Tanzania. Hili limethibitika kwa faida kuongezeka kwa 53% katika mihula miwili ya fedha. Hii imesababisha thamani ya hisa moja ya NMB kuongezeka na kufikia 2951. Bei ya leo ya sokoni ya hisa ya moja ya NMB ni Tsh 2800. Kwa mwekezaji yoyote anaetaka kutajirika atanunua hisa za NMB kwasababu thamani ni kubwa kuliko bei. ASANTE SANA. KARIBU.
 
Shukrani kwa maelezo Yako mazuri, ni kweli almost Kila siku kunafaida kidogo inaonemana. Natakiwa nifanyie nini niweze kupata compound interest mfuko wa liquid . Kwa upande wa bond fund nao unaoparate vipi?. Nimfuko Gani unatengeneza compound interest? Na huo mfuko wa uwekezaji ndio upi?

Asante kwa maoni na swali zuri sana. Fika ofisi za UTT, mtaa wa Ohio, Sukari House, ghorofa ya pili, watakupa maelekezo mazuri na ya kina zaidi. ASANTE. KARIBU SANA
 
Nondo haijajaa ongeza nondo mkuu,

Mfano faida na hasara za kuwekeza katika hisa ni zipi?

Ni kampuni gani nzuri kuwekeza katika hisa?

Gawio hupatikana vipi? Linakuakuaje hilo gawio unapatiwa vipi?

Kiasi cha kuwekeza kinaanzia shillings ngap?

Vipi hisa zikiungua zote na wewe unakua umepoteza pesa au inakuaje? Yaan km uliweka million hisa zote zikaungua ndio unakua umepoteza million au inakuaje?

Nimalize kwa kusema hisa ni uwekezaji hatarishi kuliko Dhamana,

Mfano wa Dhamana ni UTT, ukiweka unapewa gawio unawekeza kwa muda fulani na unajaza mkataba, unapewa gawio fulani kwa % then mkataba ukiisha let say miaka 5 unarudishiwa pesa yako huku ulishapata faida kwa pesa yako, mfano uliweka million 100 utapewa % mfano 88,000 kila mwezi baada ya miaka 5, unarudishiwa million 100 yako na huku miaka yote kila mwezi umekua ukipewa 88,000 kila mwezi

Hisa, ukiweka hisa kwenye kampuni kisha ikapoteza hisa zote na wewe unakua umepoteza pesa zako yaani umeziunguza kimoja, km uliweka million 10 au million 100 inakua imeungua kimoja hupati hata shilling 10, huwezi kwenda kudai tena hisa zako inabidi ununue upya hisa zingine kwenye kampuni nyingine,

Nimeeleweka?
 
Back
Top Bottom