Malawi yadai kuishtaki Tanzania kwenye Umoja wa Afrika(AU)

Shukrani ya punda ni mateke, hawa watu tunawahifadhi hapa kwa maelfu, halafu bado wanaleta madai yasiyokua na kichwa wala miguu. Tuwafukuze wote wakajifunze namna ya kuishi na majirani zao. Ungrateful people.
Mkuu halihitaji jazba,wanyasa wameoana na wamalawi,bidhaa nyingi kyela na nyasa zinatumika hadi malawi. Sioni sababu ya kuwafukuza hawa ndugu,ni kuhakikisha viongozi wenye mtazamo kama wa huyu bwege hawaioni ikulu ya malawi.
 
Hii nshu ya malawi ni siasa tu hapa. Kwanza hebu fatilieni vizuri Rais wa malawi ni nani, alikuwa akifanya nini kama professor hapo dar miaka ya nyuma, alikuwa na conection hipi na ile serkal ya kikwete. Nani alimfinance campain yake uko malawi. Aliwezaje kumshinda yule mama ( Rais wa malawi aliyepita) Ukipata majibu sahihi yaweke kwenye mabano jumlisha na siasa za propaganda za tanzania , jibu jiongeze mwenyewe.
 
Harambee iitishwe tuchange pesa na raslimali zingine tuwatwange, Hii ni field work imepatikana, ni fursa. Hembu kesho tu harambee ianze. HATA majogoo bila kupigana haya heshimiani. Zipigwe tu
Ukipigana na Malawi kuhusu ziwa Nyasa ujue unapambana na Marekani na Urusi ya Putin. Uko tayari?
 
Sababu 10 zinazoesha kwanini Malawi haina ubavu wa kupambana na Tz kijeshi ni hizi zifuatazo
1. Geographical position; Malawi wapo uwanda wa chini na Tz ipo uwanda wa juu ni rahisi kushambuliwa kijeshi ukiwa chini wkt mwenzako yupo huu.
2 Population; Kwa sensa ya mwk 2012 Wa Tz wapo 45m Wamalawi wap hawavuki Milioni 25, ukubwa wa jeshi ni direct proportional na idadi ya popn.
3. Malawi haina jeshi la wana maji Navy Tz wanajeshi imara la Navy
4. Umbali wa miji mikuu, nirahisi kombora la Masafa marefu kufika Lilongwe ukiwa boda umbali ambao kombora la Masada marefu litaishia Iringa



Mkuu umetoa point zilizo expire Israel ina watu wangapi ilivopiga waarabu kwa siku6?
Kombora zipi unazisemea?kun inter continentali ballistic missiles inafika hadi India ukipiga toka tz
3navy ya Tz ina vifaa gani na uimara wake nini?
Sababu 6zilizobaki mbona hutaji
 
Mkuu hilo ndo linalonishangaza. Hii ramani tumeichora kama inavyotakiwa iwe. Itabidi "watuformat" akili zetu zote ndo hilo lifanikiwe


Ni ngumu. Yaani toka naandikia kwenye vumbi kule kijijini mpaka leo niko nyuma ya keyBoard ya Mpakato naambiwa eti ile ramani niliyokaririshwa ilikuwa siyo mpaka sahihi siyo rahisi kumwelewa haraka mtu kiasi hicho-na kinyume na hivyo shule tutakuwa tulipotezeana muda na ingekuwa heri ningejiendea kufuga Mbuzi na ngo'mbe leo hii pengine ningekuwa kama Mengi,MO kwa kule kwetu.
 
Waachiwe tu,mbona tz ina maziwa makubwa tu kuliko icho ki-nyasa


Unaongea tu bila kufiria, je watanzania wa Mbamba Bay na Liuli ambao maisha Yao yote yanategemea ziwa hilo utawapa nini?
 
Hivi vita na malawi nayo kweli itaitwa vita? Mbona kwa JWTZ hii ni kazi ya siku mbili tu. Hata hatuhitaji kupeleka vikosi vya ziada huko...walio huko wanatosha. Sema tu sisi ni taifa ambalo linapenda amani.
Mbona Uganda hatukuwapiga kwa siku mbili? Usirahisishe mambo kiasi hicho.
 
Unaongea tu bila kufiria, je watanzania wa Mbamba Bay na Liuli ambao maisha Yao yote yanategemea ziwa hilo utawapa nini?
Sijaongea, nimeandika buana. Kwa hiyo unataka kuniaminisha kwamba bila hilo ziwa hao watu hawawezi kuishi? Huo ni uvivu wa kufikiri,Fursa zipo kamanda wacha kulemaza akili. Sina uhakika kama rasilimali za hilo ziwa zinawanufaisha hao wakaazi hisika inavyotakiwa.

Sent from my TECNO-Y4 using JamiiForums mobile app
 
Sijaongea, nimeandika buana. Kwa hiyo unataka kuniaminisha kwamba bila hilo ziwa hao watu hawawezi kuishi? Huo ni uvivu wa kufikiri,Fursa zipo kamanda wacha kulemaza akili. Sina uhakika kama rasilimali za hilo ziwa zinawanufaisha hao wakaazi hisika inavyotakiwa.

Sent from my TECNO-Y4 using JamiiForums mobile app


Ngoja nikuache Tu. Kwasababu nimeshaelewa upeo Wako uko vipi.
 
Ngoja nikuache Tu. Kwasababu nimeshaelewa upeo Wako uko vipi.
Kwani lazima tufanane mawazo, any way hata likitokea la kutokea nina uhakika mchango wako uyaishia humu jf..wa kuamua wataamua babu, usijifanye unaipenda sana tz maana ni unafiki tu na kutafuta sifa.

Sent from my TECNO-Y4 using JamiiForums mobile app
 
Je Ulikuja Kubadirishwa hapo katikati kabla hizi nchi hazijapata uhuru?
Je ule mkataba wa nchi zinazoshare vyanzo vya maji mpakani zote kuvitumia kwa pamoja sisi tumeusaini?, Je Wamalawi nao wameusaini?.

mimi nafikiri solution ni mahakama ya kimataifa tu kutatutua huu mgogoro, vita si lelemama

Wakuu nimefuatilia kwa kina posts zote kuhusu huu mgogoro. Hata hivyo kwa kiwango kikubwa wengi wanajielekeza zaidi kwenye vita badala ya njia za kidiplomasia. Ni wazi kuwa msimamo wa Malawi ni kwamba ziwa lote liko kwao isipokuwa ule upande wanapopakana na Msumbiji. Msimamo wa Tanzania uko wazi wala sihitaji kuurudia.

Katika hoja zao Wamalawi wanatumia Heligoland - Zanzibar Treaty kama mamlaka ya kuwapa ziwa lote. Watanzania inatupasa tujiridhishe kuwa ipo sheria yoyote ya kimataifa inayotupa uhalali wa hilo ziwa? Sheria ya Water Bodies inatumika tu in the absence of written agreement!

Kwenye preamble ya Heligoland - Zanzibar Treaty yapo maneno haya:

"This treaty temporarily settled colonial disputes between Germany and Great Britain. It recognized Tanganyika as a German colony; in return, the Germans abstained from further encroaching into British Kenya. The agreement ceded Heligoland, an island off the coast of Schleswig-Holstein in the North Sea, to Germany. Because the treaty appeared to abandon German colonial claims to much of east Africa, it unleashed a storm of nationalist protest at home."

Je, baadaye kulikuwa na Mkataba mwingine?

Article I(2) ya Heligoland - Zanzibar Treaty inasomeka hivi:

"To the south by the line that starts on the coast of the northern border of Mozambique Province and follows the course of the Rovuma River to the point where the Messinge flows into the Rovuma. From here the line runs westward on the parallel of latitude to the shore of Lake Nyasa. Turning north, it continues along the eastern, northern, and western shores of the lake until it reaches the northern bank of the mouth of the Songwe River. It then continues up that river to its intersection point with the 33rd degree of east longitude. The line continues along the river until its closest point with the border of the geographical Congo Basin as described in Article I of the Berlin Conference and marked on the map appended to its ninth protocol. From here the line runs directly to the previously described border, follows this to the point of intersection with the 32nd degree of east longitude, turns and continues directly to the meeting point of the northern and southern branches of the Kilambo River. It follows that river until it enters Lake Tanganyika.

The course of the planned border has been specified in accordance with the map of the Nyasa Tanganyika Plateau that was officially drawn up for the British government in 1889.
"

Kwa kuzingatia Heligoland - Zanzibar Treaty, ziwa lote liko Malawi.

Tunapojadili tujaribu sasa kuja na msimamo wa nchi yetu ukithibitishwa na sheria za kimataifa. Tunaweza kuamua kuingia vitani na huenda tukawashinda Wamalawi lakini hatutabadilisha kabisa mpaka huo hata kama tutawaua Wamalawi wote.

Msimamo wangu:
Hakuna haja ya kuingia vitani na jirani zetu Malawi, twende kwenye meza ya majadiliano, wakitushinda twende kwenye Mahakama ya Kimataifa. Endapo Mahakama hiyo itatoa maamuzi kwa kuwapa ziwa lote Malawi kwa mujibu wa Heligoland - Zanzibar Treaty basi tusipanic, tujipange upya na sisi turudi kwenye mahakama hiyo hiyo kudai ardhi yetu iliyopo Rwanda na Burundi kwa maana Heligoland - Zanzibar Treaty inatambua ardhi hiyo kuwa ni sehemu ya Tanganyika (German East Africa).

Heligoland - Zanzibar Treaty (1890) inapatikana hapa kwa wepesi wa rejea:

http://germanhistorydocs.ghi-dc.org/pdf/eng/606_Anglo-German Treaty_110.pdf

Say "No" to war and "Yes" to dialogue, ng'wabheja sana.
 
Watu wasichokijua ni kwamba, japo Tanganyika imezunguukwa na maji kibao kila kona, lakini umiliki wa hayo maji una utata sana, kwa mfano:

1) Maji ya Ziwa Victoria, Misri inadai share kubwa ya maji hayo kupitia mkataba wa kikoloni wa River nile.

2) Ziwa Nyasa, Wamalawi wanadai kuwa lote lao!

3) Bahari ya hindi, Haijulikani mpaka kati ya nchi ya Zanzibar na Tanganyika ni upi, lakini Zanzibar ina bahari yake.

Ziwa pekee lisilo na utata ni Ziwa Tanganyika!
 
Mkuu umetoa point zilizo expire Israel ina watu wangapi ilivopiga waarabu kwa siku6?
Kombora zipi unazisemea?kun inter continentali ballistic missiles inafika hadi India ukipiga toka tz
3navy ya Tz ina vifaa gani na uimara wake nini?
Sababu 6zilizobaki mbona hutaji
Duh sawa ww mwenyewe point za maana Ukiongelea Isreal uwe unafikiria na level ya technology waliyonayao, intercontintal ballistic missiles unaweza kuniambia nchi ngapi za Africa wanazo? Pia unafahamu vigezo vya kuangalia unapotaka kumshambulia adui yako au?
 
Duh sawa ww mwenyewe point za maana Ukiongelea Isreal uwe unafikiria na level ya technology waliyonayao, intercontintal ballistic missiles unaweza kuniambia nchi ngapi za Africa wanazo? Pia unafahamu vigezo vya kuangalia unapotaka kumshambulia adui yako au?


Mkuuu embu jaribu kusoma history ya vita kuna mambo mengi ya kushangazaa sana hao Malawi unaeza kuta wanatangulizwa mbele nyuma Tao Luna wenye mabavu japo kuwa kiukweli Malawi kama Malawi haiwezi kusimama na Tz
 
Nimesoma koment zao wengi wanaona Malawi iko powerful sana kijeshi kwamba wataipiga tz kirahisi kama vita itatokea. Hawa jamaa wametusumbua sana toka enzi za kamuzu banda nadhani ifike wakati sasa tufanye maamuzi magumu
Kwa hiyo unapendekeza nini kifanyike???????????????
 
Hakuna vita itakayopigwa,ramani ilicholwa na mkoloni na kesi ipo kwenye mahakama ya mkoloni tusubiri maamuzi Ya mkoloni.
 
Nimesoma koment zao wengi wanaona Malawi iko powerful sana kijeshi kwamba wataipiga tz kirahisi kama vita itatokea. Hawa jamaa wametusumbua sana toka enzi za kamuzu banda nadhani ifike wakati sasa tufanye maamuzi magumu
Tatizo kubwa ukianzisha vita na Malawi unaweza kujikuta upo vitani na mataifa makubwa kama Uingereza ambao wana interest na mafuta na gesi iliyopo ziwani lazima kufikiria sana kabla ya kuingia vitani
 
Back
Top Bottom