Maisha ni safari, usikate tamaa

kelphin

JF-Expert Member
Dec 24, 2019
9,198
14,698
Nitumie mfano harisi kwenye maisha yangu mwenyewe,

Hi ikupe mwanga wewe kuendelea kupigana kwenye hicho unachokifanya.

Tangia mdogo nlipenda sana mambo ya ufundi,hasa umeme na electonics kiujumla. Hata nyuzi zangu humu zimejikita zaidi kwenye mambo hayo.

Pengine nlikosa ada yakusomea mambo ya electronics au sifa za kujiunga na vyuo kupata elimu hiyo.
Ila kwakua nlikua na NIA thabiti nliendelea kujifunza kupitia smartphone yangu ya kipindi hicho(vodaphone).

Nlipenda sana mambo ya audio amplifiers,Nikapewa ushauri na baadhi ya watu kua niende ofisi moja iringa (jina kapuni) nkaombe kujitolea huku nikijifunza zaidi Walinikatalia!!

Hivyo kama wangenikubalia basi ingekua nikitoka chuo,basi nipite hapo kufanya kazi kadhaa jioni hadi walau saa3,4.

Hapo ndipo nlipoamua kutumia simu yangu kusoma na kutumia pesa kidogo (niliyopewa kama nauli na kula chuo) kununua components na kuanza kuunda circuits au Ramani za electonics (amplifiers)

IMG_6915.jpg

Hivyo nilinunua vero board moja na soldiering gun na soldering waya kiasi ya kuanzia.

Nlianza kuunda ramani ndogo bila ya mafanikio yoyote yale.

Zaidi ya yote nilikula hasara sana sababu ya makosa kadhaa ya ugeni wa kujifunza,

Nliharibu vitu kadhaa ikiwepo laptop yangu Samsung (NP300e5z) iPhone 3g yangu ya kwanza ndio ilitoa moshi mbele yangu

Yani una test mziki kama unapiga fresh kumbe waya wa umeme umegusana na ule wa kuleta mziki kutoka kwenye simu.

Na kwasababu sikua na fedha hi ilinibidi kusubiri hadi niwekeze tena fedha walau ifike 2000 nkanunue ic tena yakufanyia majaribio.

Kumbuka ic hizi nlikua nanunua palepale ambapo walinikatalia kwenda.

Kadri siku zilivyosogea nilizidi kujaribu na kuona matokeo + kwenye projects zangu.

Na kwa kudra za mungu nilianza kuletewa kazi kadhaa hapohapo nyumbani.

Hivyo nikitengeneza nikilipwa basi fedha hiyo naipeleka tena kununua components tena nyingine na nyingine.

Kwa upekee sana nashukuru mungu nlikuja kufahamu wapi nilikua naenda kinyume.

Na hapo ndio nkawa nmeweza kutengeneza circuits yangu ya kwanza.

IMG_6916.jpg


hi ilifanya kazi vizuri bila shida. Hivyo nkaendelea zaidi na zaidi hadi hapa nilipo. Japo nlikua siweki umeme mwingi(kadri ramani inavyoingiza umeme mwingi basi ndivyo inavyokua na nguvu

IMG_6919.jpg

IMG_6921.jpg
Hapa nikawa nimesha anza kuelewa kwa kiasi kipana.

Lakini hazikua kubwa sana

Hi mfano wa hizi subwoofer zitumikazo nyumbani.

Kwa baadae nikaanza zenye watts nyingi kwa matumizi makubwa.

IMG_6451.jpg

Hi ni moja kati ya nilizofanya hiv karibuni

IMG_6452.jpg

IMG_6454.jpg

IMG_6463.jpg

IMG_6770.jpg

Na hii ni most powered sababu inatumia umeme mwingi
Na pengine una redio yako imekufa labda na ulipenda irudi
Inasukiwa amplifier kisha inawekwa humo ndani na redio yako itarud kwenye hari yake
IMG_6774.jpg

IMG_6913.jpg

hapa tayari inafanya kazi. Siku moja nilipigiwa simu na mmiliki wa ile ofisi akinitaka nifike ofisini kwake,
Kidogo alistaajabu. Kama ni mimi. Alitaka nmfanyievkazi moja ,nikamwambia sawa ila kwa ghalama hizi’akaridhia akanilipa(pata kitu hapa) Niliendelea na naendelea kujifunza kila siku na kila wakati

Sababu inahitaji ghlama kubwa kulinda kile ulichonacho na kukiongezea thamani.

Siku zote Nataman nipate watu wa5 kwenye life yime yangu niwafundishewafikie hapo!

Shida ni kua wengi wao wanataka kutengeneza kile nlichofanya. Mwingine akisikiliza mziki wangu anataka kutengeneza kama mimi.

Mimi nataka mtu mwenye nia binafsi Aamue yeye binafsi. Ajitoe kwenye kujifunza

Sababu mimi nitakupa 1/10tu vingine utatakiwa kujifunza wew mwenyewe.

Keep it fighting. Until umefikia highest point kwenye maisha yako.

Ikiwa hujui unapoend , popote ulipo ni sawa
 
Sisi tulianza na radio ya gari kuibadilisha ikawa amplifire. Ila kwa sasa tuko kwenye hydropowercircuit tunapasuka vichwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom