Kaa la Moto
JF-Expert Member
- Apr 24, 2008
- 7,903
- 1,055
Kwa kuongezea hata wenje ni mjaluoMWEEN umecha mada umeingia kwenye mjadala usioujua wa kikabila. Kwanza naomba uelewe wajaluo wa Kenya au Uganda si wajaluo wa Tanzania. Wote ni wajaluo lakini wako nchi tofauti lakini hata kama umewaongelea wajaluo wa Kenya sitaacha uendeleze hizo fikra potofu.
Naomba kama kuna kabila lina historia ya kupigania Uhuru wa Kenya na Afrika Mashariki basi utakuwa mnafiki kubwa kuwaweka wajaluo kando.Wajaluo kwa tabia yao ni watu wasioogopa na hawapendi kuonewa hivo walikuwa watu wa kwanza kupambana na wakoloni. Kama kuna mjaluo walikuwa wasaliti ni mtu m1 m1 na si jamii nzima kama ilivyo wasaliti wa ufisadi leo wanaotoka kwenye kabila tofauti. Mau mau walikuwa wakikuyiu walokuwa wanapiga vita na wakoloni lakini si kwamba makabila mengine hayakuwa yakidai uhuru. Wajaluo waliongoza mapambano ya kiamani dhidi ya wakoloni mbali na Maumau. Kwanza uelewe Chama cha KANU kilichokuja kupata uhuru kilinzishwa na wajaluo na si Kenyatta. Kenyatta alikuja kupewa uongozi baadaye wa chama hicho.
Watu kama babake Raila; Oginga Odinga, Tom Mboya, Achieng' Oneko, Argwing Kodhek na wengine wajaluo wengi ni mashujaa w Kenya waliopigania kupatikana uhuru wakishirikiana na wakenya kutoka makabila mengine.
Nikutaarifu tu kwamba kama wajaluo wangekuwa wasaliti Kenyatta asingekuwepo kwenye uliongo wa siasa ila kwa busara za babake Raila na kwa uzalendo mkubwa alipotakiwa kuchukua uongozi wa Kenya wakati huo Kenyata yuko Gerezani alikataa kwamba Kenyata afunguliwe kwanza ndipo wapewe uhuru. Sijui ni watu wangapi wanaoweza kufanya uzalendo kiasi hicho.
Baada ya Kenyatta kuchukua madaraka hakukumbuka fadhila hizo na akaanza kuwatenga wajaluo, kuwaua na utawala wa kidekteta wa kutisha na kujilimbikizia mali huku akiinua kabila la wakikuyu na hapo ndipo ukabila ulipoanza. Mauaji kama ya Tom Mboya 1969, JM Kariuki na wengineo ni mifano.
Wakati wa Moi pia wajaluo walidhulumiwa kwa kiasi kikubwa mfano mauji ya Dr. Robert Ouko 1990 na hata wakati wa Kibaki Mauaji ya Profesa Odhiambo Mbai kwenye mapambano ya kupata katiba mpya.
walioongoza mapambano dhidi ya utawala wa kimabavu mpaka wakenya sasa wanajivunia nchi yao kwa kiasi kikubwa ni wajaluo na mpaka sasa kwao mapambano yanaendelea.
Tukirudi Tanzania wajaluo walichagua mbunge wa upinzani kwenye uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi 1995 na hata mwaka huu CHADEMA tu hawakujipanga kuchukua jimbo la Rorya lakini ni wazi ushindi ulikuwa ni wao. Watu wa Rorya nina imani wamemchagua Dr. Slaa kuliko Kikwete ni watu wa mageuzi kabla Mageuzi hayajaingia Tanzania. Kule watu hawapendi CCM na huo usaliti wa Maina ni wa wachache.
Hivyo MWEEN uwe makini kujadili makabila badala ya hoja ya Maina.