Mahakama yakazia sheria ya ushoga

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,820
4,572
Mahakama ya katiba nchini Uganda imetupilia mbali shauri lililowasilishwa Mahakamani kupinga sheria dhidi ya mapenzi kati ya Watu wa jinsia moja na kusisitiza kuwa sheria hiyo inalinda utamaduni na hadhi ya Watu wa Uganda.

DW ( @dw_kiswahili ) imeripoti kwamba Walalamikaji walitaja sababu mbalimbali wakitaka itupiliwe mbali ikiwemo kusema Bunge la Nchi hiyo halikufuata utaratibu stahiki katika kujadili na kupitishwa muswaada wa sheria hiyo na kwamba sheria hiyo ilipitishwa baada ya kujadiliwa kwa siku sita tu badala ya 45 kama inavyotakiwa.

Maamuzi ya mahakama ya katiba yenye kurasa 200 yamesomwa kwa muhtasari na Naibu Jaji Mkuu aitwae Richard Buteera akinukuu dondoo mbalimbali zilizowapelekea kufikia maamuzi hayo ambapo amenukuliwa akisema “tunakataa kutupilia mbali sheria hii kwa sababu kimsingi inalinda hadhi na utamaduni wetu ambao huzingatia familia kuwa taasisi muhimu kukuza jamii”.

Mawakili wa upande wa Walalamikaji wanaojumuisha hasa makundi ya jumuiya ya mapenzi ya jinsia moja maarufu kama LGBTQ wamepinga maamuzi hayo na kuwakosoa Majaji kwa kile wanachokitaja kuwa kujenga hisia za ubaguzi wakisingizia utamaduni na kusisitiza kuwa watawasilisha rufaa Mahakamani kupinga maamuzi hayo.
 
Hao wanasheria wa serikalini na mahakama mbona wanajipa kazi isiyo na kichwa wala miguu. Yaani wanakaa chini kujadili na vichaa juu ya wanachotaka, tangu lini mtu mwenye matatizo ya akili akaruhusiwa kuparticipate maswala ya mahakamani.
 
Kweli mkuu. Ni Kichaa pekee ndiye atapata hamu kula kinyesi
 
Hao wanasheria wa serikalini na mahakama mbona wanajipa kazi isiyo na kichwa wala miguu. Yaani wanakaa chini kujadili na vichaa juu ya wanachotaka, tangu lini mtu mwenye matatizo ya akili akaruhusiwa kuparticipate maswala ya mahakamani.
Kwa namna hii hata mtu akishtakiwa inakua fair
 
Back
Top Bottom