Maeneo maalum ya Uchumi yanayoungwa mkono na China barani Afrika yahimiza maendeleo ya Nchi za Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,023
1,047
VCG41N692496282.jpg

Na Fadhili Mpunji

Moja kati ya mambo ambayo China iliyataja mwanzoni wakati wa kuanzishwa kwa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC, ni kuanzisha maeneo maalum ya uchumi (Special economic zones- SEZs) ili kuhimiza uzalishaji wa bidhaa za viwanda, na kuzisafirisha katika masoko ya nje.

Hii ni moja ya njia ilizotumia China kuendeleza sekta yake ya viwanda, na kupata mafanikio makubwa tangu Agosti 1980 ilipoutangaza mji wa Shenzhen kuwa eneo maalum la kiuchumi.

Mara nyingi tunapotaja sababu za Afrika kuwa nyuma kiuchumi, kimsingi tunataja kuwa nyuma kwenye maendeleo ya viwanda. Nchi zote zinazotajwa kuwa na maendeleo makubwa ya kiuchumi duniani, ni zile zenye maendeleo ya viwanda, na zinatumia sekta hiyo kama kichocheo cha sekta nyingine. Baadhi ya nchi za Afrika zenye maendeleo kiasi, ni zile zilizoonesha mwelekeo kwenye eneo hili, au walau kuifanya sekta ya viwanda iwe sehemu muhimu ya uchumi.

Kutokana na ukweli huu, mwanzoni wakati baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) linaanzishwa, China ilieleza utayari wake wa kuzisaidia nchi za Afrika kwenye eneo la viwanda kwa kuanzisha maeneo maalum 50 ya viwanda. Lengo lake lilikuwa ni kutoa msukumo kwa maendeleo ya viwanda barani Afrika, ikiwa ni moja ya njia za kuendeleza uchumi, na hatua kwa hatua imekuwa ikitekeleza ahadi hiyo.

Kwa mujibu wa Shirika la Maendeleo ya viwanda na biashara la Umoja wa Mataifa UNCTAD, hadi kufikia mwaka 2019 kulikuwa na Maeneo Maalum ya Uchumi 237 katika nchi 39 za Afrika, na maeneo hayo mengi yako katika eneo la Afrika Mashariki, na China imekuwa na mchango mkubwa katika uwekezaji kwenye maeneo hayo.

Katika miaka ya hivi karibuni maeneo maalum ya uchumi wa Ethiopia ndio yamekuwa yakitajwa zaidi, kutokana na mafanikio yake makubwa mchango wake mkubwa kwa uchumi wa Ethiopia. Maeneo ya nchi hiyo kama vile Arerti na Mekelle, yana muundo unaofanana kiasi maeneo maalum ya uchumi ya China, kutokana na ushiriki mkubwa wa wawekezaji wa China kwenye maeneo hayo.

Pamoja na kuwa uwekezaji mwingi kwenye maeneo hayo unatoka nje ya Ethiopia, mbali na kuleta fedha zinazohitajika kuendeleza sekta ya viwanda, wawekezaji pia wanatoa mchango kwenye utoaji wa ajira na usafirishaji wa teknolojia. Kwa sasa nchini Ethiopia ni jambo la kawaida kuona wenyeji wakiwa kwenye mistari ya uzalishaji wakiendesha mitambo kutoka hatua ya kwanza hadi ya mwisho, wakitengeneza bidhaa zinazosafirishwa nje ya nchi. Lakini muhimu zaidi ni kuwa uzalishaji kwenye maeneo hayo licha ya kutumia nguvu kazi ya wenyeji, pia unahimiza matumizi ya malighafi za ndani.

Mara nyingi wataalamu wa mambo ya uchumi wa Afrika wamekuwa wakikosoa muundo wa uchumi wa Afrika kwa kuutaja kuwa ni ule “unaozalisha bidhaa zisizotumiwa na wenyeji, na wenyeji wanatumia bidhaa zisizozalishwa nchini kwao”. Kupitia Maeneo maalum ya viwanda, hali hii sasa imeanza kubadilika.

Tunaweza kuchukulia mfano wa simu maarufu ya TECNO ambayo shughuli zake za utafiti zinafanyika mjini Shenzhen, uzalishaji wake kwa sasa unafanyika nchini Ethiopia na Nigeria. Teknolojia ya kutengeneza simu hizo ni ya China, lakini nguvu kazi na malighafi zinazotumiwa kutengeneza simu hizo zinatoka Afrika. Na baadhi ya simu hizo zinasafirishwa hadi kwenye soko la mashariki ya kati.

Uzuri wa maeneo maalum yanayojengwa na China barani Afrika ni kuwa si kwa ajili ya makampuni ya China peke yake. Kwenye baadhi ya maeneo hayo kuna makampuni kutoka Marekani, Uingereza, Japan na nchi nyingine yakiwa pamoja na makampuni ya China na ya wenyeji.
 
Back
Top Bottom