Machinga wanapotoa Somo, Makamanda tunakwama Wapi?

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
28,180
36,171
Safari ya kudai haki haijawahi kuwa rahisi:



Wenye ajira kudhani wasio na ajira ni wapuuzi hiyo si sahihi.

Kwanini rais ang'ake kusikia tishio kwenye kuendelea na urais baada ya 2025?

Kwanini Makalla asiwe tayari kuachia ngazi na kwenda kujiajiri?

Kwanini yasipunguzwe maslahi serikalini kuwafanya watu waone haja ya kujiajiri zaidi na kutoka serikalini?

Hili likiwahusu vigogo wote wakiwamo Rais, Mawaziri, wabunge nk haliwezi kusaidia kupunguza makali kwenye jamii?

Makamanda hatuna la kujifunza kutoka kwa washupavu hawa?

Haki hupiganiwa na kupiganiwa kwake kwenye tija ndiyo huku katika mazingira tuliyomo.

"Shujaa ni yule anayefia kwenye uwanja wa kivita." Asema Chinga.

Angalizo:

Mfano wa gharama za shughuli kama hizi:



Zisingeweza kutumika kwa tija zaidi?
 
Makamanda wajifunze kitu? Hiyo ni ndoto ya mchana. Makamanda, hasa wafuasi wa mr #dishlimetilt, hawawezi kujifunza kitu maana wanaamini wanajua kila kitu!

Wenye misafara ya anasa kama hii:



Wakati hali nchini si hali, kama wanavyo tanabaisha machinga.

Mustakabala wa ku tilt kwa madishi yao unauongelea je ndugu mjumbe?
 
Yuko Pia anae ng'ang'ania uchairman hapo ufipa

Amekuingiza wewe gharama gani? Au ana kuhusu wewe vipi?

IMG_20211031_200534_701.jpg


Au ni chuki binafsi tu ndugu mjumbe?
 
Makamanda wajifunze kitu? Hiyo ni ndoto ya mchana. Makamanda, hasa wafuasi wa mr #dishlimetilt, hawawezi kujifunza kitu maana wanaamini wanajua kila kitu!
Wewe kiazi ikiwa tu akina mama wa Bawacha wakifanya jogging wanapelekewa defender 10 na Askari wenye silaha nzito za kivita sembuse kufanya vurugu. Najua mnachochea hivyo ili kukidhi kiu ya watawala ya kuifuta Chadema kuwa ni chama cha vurugu. Hatuingi hii mitego yenu ya kindezi.
 
Dogo nimekuelewa sana!

Unakuta Ummy Mwalimu anaitisha press kutangaza ajira 3000 katika population ya binadamu 60,000,000.

Halafu waandishi wa habari Wanamshangilia na kumpigia makofi.

Bila kuwa kemea watawala hawa katika yasiyo haki na usawa watadhani ni halali yao.

Shime waungwana:

1. mshahara na marupurupu yao si halali.
2. Gharama wanazotumia katika anasa zao kutokea katika jasho letu si halali.
3. Madege wanayonunua kwa cash, hiyo pesa isingeweza kutumika vyema zaidi kupunguza matatizo kama haya?
4. Vipi haya wanayosema kila siku ni siri za serikali?
5. Kwanini kusiwe na muda anaoruhusiwa mtu kuwa katika ajira ya serikali au umma?

Tufike mahali haya ya siri za serikali yasiwepo.

Siri vipi wenye nchi sisi?
 
Wewe kiazi ikiwa tu akina mama wa Bawacha wakifanya jogging wanapelekewa defender 10 na Askari wenye silaha nzito za kivita sembuse kufanya vurugu. Najua mnachochea hivyo ili kukidhi kiu ya watawala ya kuifuta Chadema kuwa ni chama cha vurugu. Hatuingi hii mitego yenu ya kindezi.

Pamoja na yote mkuu hatupaswi kutegemea huruma ya mtu awaye yote.

Haki haitapatikana kwa mujibu wa matakwa yao. Wala haki haitapatikana kwa mujibu wa sheria zao.

Kumbuka matakwa na sheria zao ni kuwa waendelee kudumu milele:

Katiba Mpya: Kulikoni Makamanda na ndugu Wananchi Kusita Sita?

Pana maeneo makamanda itabidi kukubaliana kupeana makavu na Bila kuangalia makunyanzi. Bila hivyo hatuwezi kutoboa.

Kuwa tayari kuyajaza magereza yao ni karata bora kabisa tuliyo nayo inayomtia adui kiwewe.

Chama si kuwa kwenye madaftari ya Mutungi peke yake. Huko hata TLP wapo.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Back
Top Bottom