Maboresho ya sekta ya elimu yanaendelea kwenye shule za kata

Apr 11, 2024
21
52
Mnamo Oktoba 2023, Nilifanikiwa Kuhudhuria Mahafali Ya Kidato Cha Nne, Ya Shule Ya Upili, Zavara.
9A646E45-58A0-4BED-8CFF-AC4F815ABD3C.jpeg


Katika Mahafali Haya, Mgeni Rasmi Alikuwa Mbunge wa Viti Maalumu Anayewakilisha Wafanyakazi, Mhe. Janejelly James Ntate, Ambaye Alihusia na Kuwatia Moyo Wanafunzi Waliohitimu Kidato Cha Nne. Alipokea Changamoto Za Shule. Aliahidi Kuipa Shule Ushirikiano na Kutatua Baadhi Ya Changamoto Hizo, Na Kuahidi Kuwa Changamoto Zingine Ataziwasilisha Kwa Mkurugenzi wa Jiji, Ili Yapate Utatuzi.

Lakini Pia Alikumbushia Mazuri Yanayofanywa na Serikali Ya Chama Cha Mapinduzi, Yakiwa Pamoja na Kuwawezesha Wanafunzi Kupata Elimu Ya Bure Kuanzia Ngazi Ya Msingi, Shule Ya Upili, Mpaka Kidato cha Tano, na Cha Sita. Hii Imekuwa Nafuu Ya Wazazi Kuwasomesha Watoto Wao Kwenda Elimu Ya Juu.

Binafsi, Uwepo Wangu Kwenye Mahafali Haya Yamenipa Maono Ya Kwamba Ufaulu Kwenye Shule Za Kata Unawezekana, Kutokana Na Uwepo wa Ufaulu wa Daraja la Pili na la Tatu, Kwenye Mitihani Waliyofanya Kidato cha Nne Shuleni Hapo, Ikiwemo Mitihani Ya Majaribio (MOCK) Iliyofanyika Shuleni Hapo. Hivyo Kuwepo Kwa Walimu Wazuri, Na Utayari wa Wanafunzi, Kutasaidia Kuchochea Ufaulu Mzuri na wa Juu ✍️.

Pia, Napenda Kumpongeza Mheshimiwa Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Kwa Kuendelea Kuitekeleza Ilani Ya Chama Cha Mapinduzi, Kwenye Suala Zima la Uboreshaji Sekta Ya Elimu, Kimiundombinu na Kadhalika, Ili Kuchochea Maendeleo Chanya Ya Wananchi 🇹🇿 na Taifa.
03C62707-D57F-4F40-8F73-1F7792F505F2.jpeg

#KaziIendelee
 
Elimu bila ajira wala maarifa ya kujiajiri hugeuka kuwa ujinga Kwa taifa!!

Graduate anakua boda boda anapata ajali anakufa bila kurejesha mkopo was HSLB !Elimu hii ya Sasa Haina maana kama haiajiri!!
 
Back
Top Bottom