M23 yaua wanajeshi 3 wa Tanzania huko Goma DRC

Halafu huwezi tumia lugha eti M23 wawaua wanajeshi 3 wa Tanzania,huko kuna jeshi la Tanzania +la South Afrika na wamekwenda kwa mwambuli wa SADC ingekuwa vyema kutumia neno kuwa Wanajeshi 3 wa kikosi cha Tanzania kinachowakilisha SADC kilichopo DRC wauwaawa

Kwahiyo hapo Watanzania wanakuwa hawajauawa au
 
Watambulike kama wacongo then waunde taifa lao na kujitenga na congo kama ilivyokua sudan na sudan kusini,nchi yao itaitwa nord kivu na ndio sehemu yenye utajiri mkubwa wa madini nchini congo,cha ajabu hilo eneo lina wakimbizi wengine wa kutokea rwanda wahutu wanajiita fdrl ila wahutu wanaamini wao ni warwanda,watutsi wa m23 wanadai wao wacongo sababu wazee wao walipokimbia rwanda during habyarimana regime wao wakazaliwa ndani ya ardhi ya congo,kule kigoma kuna warundi wapo camp toka utawala wa buyoya burundi,wamezaa na hadi wamejukuu wakiwa camp but awathubutu kudai u TZ
Aidha wewe ni mbumbumbu hujui unachokiongea, au unafanya makusudi kujifanya hujui. M23 inatokea kwenye kundi la wa Congo ambao wanaongea Kinyarwanda. Wanapatikana kwenye maeneo ya Kivu kaskazini na Kusini kwa zaidi ya miaka 400 sasa. Haya maeneo wanayoishi kabla ya mkutano wa Berlin ulioigawa Afrika yalikuwa ni sehem ya Kingdom ya Rwanda chini ya mfalme wa Rwanda (King Rwabugiri)huyu ndie alikuwa anatawala Kingdom ya Rwanda wakati huo 1845-1896 wakati wa ujio wa wakoloni, Himaya yake ilikuwa ni kubwa sana kwenye maeneo haya ya maziwa makuu. Eneo lote la Rwanda leo, eneo lote la kusini mwa Uganda(Kabale) mpaka Lake Edward, Eneo lote la Kivu kusini na Kaskazini, hapa pote waliishi Raia wake wakiongea Kinyarwanda. Ikumbukwe wakati huo hapakuwa na Congo wala Tanzania au Uganda, palikuwa na chiefdom ndogondogo tu, Lakini Rwanda ilikuwepo ikiwa ni Kingdom kubwa tu mara kibao ya Rwanda ya Leo. Wakoloni hasa hasa Wajerumani, Wabelgiji na Waingereza Waliikatakata hii Kingdom na kuifanya iwe ilivyo leo. Walikubaliana ku share mirima ya Volcano kwani walijua kwenye hiyo milima kuna Utajiri mwingi sana wa madini ya chuma. so kila mmoja alisqueez Kingdom ya Rwanda mpaka kwenye hii milima. Muingereza akapush upande wa Kaskazi na Mbelgiji akapush upande wa magharibi. Hii Milima amabayo inapatikana kaskazini mwa Rwanda maeneo ya Ruhengeri,Gisenyi,Goma/Rutshuru na Kikunguri Upande w Uganda Kabla ya Wakoloni ilikuwa inapatikana katikati mwa Kingdom ya Rwanda Mfalme Rwabugiri alikuwa akiitumia kama observation point yake. So haya maeneo yalipokatwa Raia waliokuwa ndani ya hii mipaka hawakuwa Wanyarwanda tena japo lugha yao ilibaki Kinywanda. Waliokatiwa uganda wakawa waganda, waliokatiwa Congo wakawa wa Congo. Sasa Viongozi wasiokuwa na sera ndio wanawatumia kisiasa kuleta machafuko ili waendeleze utawala wao. Lakini kwa kweli hawa watu kamwe hawawezi kuwa Wanyarwanda unles kama Mwalimu Nyerere alivyosema ukiwafukuza wafukuze na Ardhi yao, Sio uwafukuze halafu ubaki na ardhi yao. Kwa bahati mbaya sasa hiyo Ardhi yao is very rich in minerals and fertility.
 
Back
Top Bottom