Lema, Nassari kufunika kesho Arusha!!!

sweetlady

JF-Expert Member
Dec 24, 2010
16,947
8,409
Baada ya ccm kuambulia watu 23 kwenye mkutano wao wa leo maeneo ya uwanja wa stadium bar ... Mkutano ambao wananchi wa arusha wameufananisha na kikao cha send off....

Pole nyingi kwa Ole sendeka na Mary Chatanda manake wamekuwepo eneo la mkutano toka sa 5 asubuhi bila kuambulia watu wa kuwahutubia! Kilichoshuhudiwa ni wacheza ngoma wakikata mauno ili kuwavutia watu bila mafanikio....... Hii ndio Arusha bwana peoplessssssss ndio habari ya wakaazi wa arusha!!! Hii maana yake ni kwamba arusha bila ccm inawezekana / ilishawezekana!

Chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) kitafanya mkutano mkubwa kwenye uwanja wa Ngarenaro kesho kuanzia saa 10 jioni...... Wasemaji wakuu ni makamanda wetu wa ukweli Godbless Lema, Nassari Joshua, Nanyaro Ephata, Amani Golugwa pamoja na makamanda wengine wengi!

Kama kawaida kutakuwepo na makamanda watakaotupatia kwa ufasaha kinachoendelea kutoka eneo la mkutano (live bila chenga).......... Habari ziwafikie Mungi, Crashwise, Arushaone, Filipo, Ben Saanane, Fidel80, Erickb52, Masanilo na wengine wengi!

Kama kawaida arusha ni peoplessssssssss mwanzo mwisho!!

Nawasilisha!
 
Last edited by a moderator:
Hakuna Jipya watakalolileta kama kawaida yao, sana sana Mipasho tu, wananchi wa Arusha wameshawachoka hawa wahuni.
 
nimepita hapo stadium ccm wanakata mauno kama wanalalwa..

Arusha Mna wabunge wawili tu halafu mnajifananisha na CCM? Eti Arusha ni ngome ya CHADEMA...acheni kupotosha Umma, Najua LEMA na Nassary wameshajipanga kununulia vijana viroba ili wawashangilie wakati wanamwaga Pumba na matusi jukwaani!
 
Waulize viongozi wako leo jua lilivyowawakia pale stadium bar..... Walikuwa wanatia huruma sana..... Poor them !!!

Mmewatuma afu wamefeli mbayaaaaaa!
 
Hakuna Jipya watakalolileta kama kawaida yao, sana sana Mipasho tu, wananchi wa Arusha wameshawachoka hawa wahuni.

Wamewachoka kwa kuwachagua au? Maana ni juzi tu wamepanda majukwaani na kuchukua kata nne muhimu. Toa hoja na ushahidi kuhusu kuchokwa kwao. Vinginevyo unashinda msalani na kutabiri mambo ya barazani.
 
Maadui wa Chadema wanakesha mitandaoni na makamanda wa ukweli wanajenga Chama.

Hakunaga kama Lema Arusha!

Watakesha sana Molemo ila wakae wakijua kuwa sauti ya wengi ni sauti ya Mungu... Sisi bado tunawaombea waishi miaka mingi ili tutakapofanikiwa wajionee kwa macho!
 
Last edited by a moderator:
Wamewachoka kwa kuwachagua au? Maana ni juzi tu wamepanda majukwaani na kuchukua kata nne muhimu. Toa hoja na ushahidi kuhusu kuchokwa kwao. Vinginevyo unashinda msalani na kutabiri mambo ya barazani.
Mkuu umenikumbusha ushindi wa nne kwa beseni...
 
Watakesha sana Molemo ila wakae wakijua kuwa sauti ya wengi ni sauti ya Mungu... Sisi bado tunawaombea waishi miaka mingi ili tutakapofanikiwa wajionee kwa macho!

bi dada unaamanisha Mungu wa Tengeru au Mungu wa Machame?? ufafanuzi tafadhali
 
Last edited by a moderator:
Arusha Mna wabunge wawili tu halafu mnajifananisha na CCM? Eti Arusha ni ngome ya CHADEMA...acheni kupotosha Umma, Najua LEMA na Nassary wameshajipanga kununulia vijana viroba ili wawashangilie wakati wanamwaga Pumba na matusi jukwaani!

You're absolutely right man! Chadema is Kiroba OG
 
Watakesha sana Molemo ila wakae wakijua kuwa sauti ya wengi ni sauti ya Mungu... Sisi bado tunawaombea waishi miaka mingi ili tutakapofanikiwa wajionee kwa macho!

Kama walivyoumbuka jinsi Lema alivyowasambaratisha kwenye uchaguzi wa Madiwani.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom