Wabunge Lema na Nassari kuweka ushahidi hadharani kesho kuwa Madiwani walipewa rushwa kuhama CHADEMA kwenda CCM

jimmyfoxxgongo

JF-Expert Member
Jan 23, 2013
5,352
9,293
Wakuu amani ya bwana iwe nanyi,

Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amesema kesho Jumapili ataweka hadharani ushahidi wa tuhuma walizonazo kuhusu madiwani wa chama hicho waliojiuzulu wakisema ni kutokana na kuunga mkono utendaji wa Rais John Magufuli.

Lema na mbunge mwenzake wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari wamewatuhumu madiwani hao wakisema uamuzi wao unatokana na rushwa.

Hata hivyo, madiwani hao kwa nyakati tofauti wamekuwa wakikanusha tuhuma hizo.
Lema akizungumza na CHADEMANEWS leo Jumamosi, amesema wataweka hadharani ushahidi huo kesho kabla ya Jumatatu kuupeleka kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Pia nimekutana na hii katika ukurasa wa Instagram wa Mhe. Mbunge Joshua Nassari, akiandika

"Ni matumaini yangu kwamba Rais atachukua hatua kwa kile kitakachoanza kuonekana kesho. Tulisema Madiwani hawaungi mkono juhudi za Rais bali wanaunga mkono RUSHWA. Ushahidi hadharini kesho".


Kinachonishangaza ni kwanini Nassari amekuwa kama mzito hivi kuutoa huo ushahidi?

Au unataka yakupate ya kukupata utuambie kwamba ushahidi umepotea?

Mlisema ushahidi ni wa kimtandao kuna ugumu gani kuutoa muda wote huo

Au mnataka na ninyi mtafute wawape kidogo walichopewa

Hebu acheni kucheza na akili za watu wekeni hivyo vitu ili tujue mtetezi wa wanyonge na haki achukue hatua

Naamin mpendwa raisi wetu Mh Magufuli hataliacha hili alishasema na ameendelea kusema kwamba anachukia rushwa

Na ameonyesha baadhi ya mifano kweli kweli

NB:Hizo aya za mwisho nimeandika nilipomimina kitu kwenye glass
 
Kwa ufupi niseme chadema si chama cha demokrasia Kabisa mtu akihama nongwa!!! Mbona CCM walipohama keenda chadema hatukusema chadema imewahonga? Niseme wazi by all standars chadema kupitia mtu Kama lema kina perform below standard kutwa kelele zake Na malalamiko yake ya kitoto ya umbeya umbeya ya kuokoteza Hana la maana analosimamia. Shame on him. Nassari kaa mbali na Lema wewe ulishajijengea heshima kubwa. Kuungana vitu vya kuokoteza okoteza kutakuharibia credibility yako. You are not Of Lema Size. Siasa za kitoto mwachie mwenyewe
 
Aaangalie sana huyo dogo asije akakutana na Nissan nyeupe akiwemo kapero?
 
Hata wewe NASSARI na ujanja wako wote unaingia katika mtego "MBUZI" wa kitoto kama huo? pole sana!!!!
 
Back
Top Bottom