Kwanini watanzania wengi huwa hawakubali kuwa kuna watu wanafanikiwa kihalali?

Gulio Tanzania

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
2,283
4,890
Ni jambo la kushangaza kwa watanzania wengi sio watu kukubali pale mtu anavyofanikiwa kimaisha lazima mtu azushiwe jambo lolote ataitwa mchawi, tapeli, anafanya biashara haramu ukisamehewa kidogo utaambia unasaidiwa na familia ili ionekane uwezo wako ni mdogo kwamba hauna tofauti na wao watanzania wengi huwa hawataki kuamini kwamba Kuna watu wapambanaji
 
Watanzania tuna matatizo ya kiakili ambayo ni matokeo ya umaskini uliokithiri...

Hata ukinunua gari utasikia mkopo huo! Ukianzisha biashara mtaani basi wanaamini umeajiriwa mahali.

Kuna jamaa wilaya fulani kafanikiwa sana kwenye biashara ya Hardware, sasa waja wanazusha eti kuna kaka ake TRA ndo anampa hela, hivi kuna kaka wa kukupa hela mpaka utajirike kweli na bado aendelee kukupa tu?
 
Kuna mafaniko mengine ukiyafikiria haya make sense na ubaya zaidi hata walifanikiwa na wenyewe ni wabinafsi kuonyesha abc za mafanikio yao hapo ndo kila mtu atakuja na assumption zake .
 
Ni jambo la kushangaza kwa watanzania wengi sio watu kukubali pale mtu anavyofanikiwa kimaisha lazima mtu azushiwe jambo lolote ataitwa mchawi, tapeli, anafanya biashara haramu ukisamehewa kidogo utaambia unasaidiwa na familia ili ionekane uwezo wako ni mdogo kwamba hauna tofauti na wao watanzania wengi huwa hawataki kuamini kwamba Kuna watu wapambanaji
Kwasababu ni wajinga tu.

Ujinga uliokithiri ukachanganywa na umaskini mkubwa.
 
Kwa sababu kwa mazingira ya ujumla ya kibongo ni vigumu sana kufanikiwa kihalali
 
Back
Top Bottom