Kwanini Waafrika hatulimi matunda yetu ya asili?

Huku kijiji yapo baadhi mfano tope tope, maparachichi ya asili tokea enzi, mapera, strawberry za asili , kuna mengine nayajua kwa kilugha sijui kiswahili chake

sema wameshaleta miparachichi eti wanayaita ya kizungu, michungwa ya kizungu yaani full uzungu
Matunda yote uliyoyataja ni ya kigeni.
 
Hatuna matunda yetu ya asili yote yaliletwa na kina vasco da gama. Labda ndulele
Tikitiki la asili yalikuwa yale ya kijani,mzee wa denga sahv yamepotea kabisa
Kuna kipindi fulani nliyalima sana
Mkuranga maeneo ya mwarusembe ndani ndani huko
Na matango ya kienyeji yale

Ova
 
Hivi mtu unaanzaje kufanya kilimo cha Ngweda?, Ila ni tamu sana. Au basi tuseme mtu unaanzaje kulima Mabungo?. Matunda ya Afrika ni matunda pori tu. Badala ya shamba utajikuta unakuwa na pori la matunda
 
Hata ya kizungu yalianzia porini. Huko Asia watu wanalima ukwaju kwa wingi na hili tunda asili yake ni Afrika. Panda mibuyu, vizazi vyako vitakula miaka mia nane ijayo. Kuna mtu West Afrika anapanda mibuyu. Inachukua miaka mingi sana kuzaa lakini akiwa anasubiria matunda, majani machanga ya mibuyu anatumia kama mboga, yanatwangwa kama kisamvu, full vitamin C.
 
Hivi mtu unaanzaje kufanya kilimo cha Ngweda?, Ila ni tamu sana. Au basi tuseme mtu unaanzaje kulima Mabungo?. Matunda ya Afrika ni matunda pori tu. Badala ya shamba utajikuta unakuwa na pori la matunda
Mmea wa bungo hutambaa kama mpensheni, hivyo tunaweza yatoa porini mambo yakaenda,
Tafiti zinaonyesha hata mahindi yalitoka porini
 
Back
Top Bottom