Kwanini 'military takeovers' zimerudi kwa kasi Afrika?

Haya mambo yameanza tena kurudi hapa Africa hivi sababu ni kitu gani ? Mbona huko majuu hatuyasikii au kuyaona yakitokea ?
Hatuko huru,
watu wanadai uhuru.
viongozi wa Afrika wengi ni vibaraka

bado tumetawaliwa na wazungu

Wajukuu watakuja kusoma historia namna mapinduzi yaliyofanyika na kuleta uhuru

Watatushangaa sana Kwamba tulikuwa wazembe

Kizazi cha 2010 kikiwa na elimu hakiwezi kuvumilia hasa ujinga wa wazungu
Mikataba mingi ya hovyo itavunjwa
 
It might happen when 'ENOUGH IS ENOUGH'. Let it be that way if it's going to result into impactiful and positive changes !!
 
Ni matokeo ya siasa za kidunia, hazina sababu za msingi za wananchi wa kawaida wa Afrika.

Mapinduzi haya, yanaratibiwa na mataifa yenye nguvu kiuchumi, kijeshi na kiteknolojia.

Sio mapinduzi yanaratibiwa na kusukumwa na uhitaji wa ndani ya Afrika.

Kinachoendelea kwenye wimbi hili la sasa ni regime change na sio philosophical reforms. Falsafa inabaki ile ile, watu serikalini ndio wanaobadilika.

Mfano: Kitendo cha Marekani kulipua bomba la Urusi kutoka Urusi- Ulaya (Nord-stream) ndio sababu Kuu ya Mapinduzi ya Niger. Usiniulize kwa namna gani, chekecha kichwa utapa jawabu.

Kwasasa, Hakuna mapinduzi yatakayo ratibiwa na wananchi wa kawaida (Afrika) wenyewe yatakayofanikiwa bila kuhusisha maslahi ya mataifa yaliyoendelea kiuchumi, kijeshi na kiteknolojia.

Kwasasa wamiliki wa uchumi, jeshi na teknolojia wa ulimwengu wameshagawana vitalu vya kuvuna kama ilivyokuwa kipindi cha ukoloni mkongwe.

Hivyo, sio rahisi kwa wananchi wa kawaida kuanzisha na kufanikiwa kufanya mapinduzi.
 
Haya mambo yameanza tena kurudi hapa Afrika hivi sababu ni kitu gani? Mbona huko majuu hatuyasikii au kuyaona yakitokea?
kwa sababu ya wizi,uzandiki,ukandamizaji,kurithisha watoto vyeo na akili za viongozi wengi kwa sasa hazijavaa suruale kwa kukaza,bali zimevaa mlegezo kama maniga wa USA!!!.......................!!!!
 
Ni matokeo ya siasa za kidunia, hazina sababu za msingi za wananchi wa kawaida wa Afrika.

Mapinduzi haya, yanaratibiwa na mataifa yenye nguvu kiuchumi, kijeshi na kiteknolojia.

Sio mapinduzi yanaratibiwa na kusukumwa na uhitaji wa ndani ya Afrika.

Kinachoendelea kwenye wimbi hili la sasa ni regime change na sio philosophical reforms. Falsafa inabaki ile ile, watu serikalini ndio wanaobadilika.

Mfano: Kitendo cha Marekani kulipua bomba la Urusi kutoka Urusi- Ulaya (Nord-stream) ndio sababu Kuu ya Mapinduzi ya Gabon. Usiniulize kwa namna gani, chekecha kichwa utapa jawabu.

Kwasasa, Hakuna mapinduzi yatakayo ratibiwa na wananchi wa kawaida (Afrika) wenyewe yatakayofanikiwa bila kuhusisha maslahi ya mataifa yaliyoendelea kiuchumi, kijeshi na kiteknolojia.

Kwasasa wamiliki wa uchumi, jeshi na teknolojia wa ulimwengu wameshagawana vitalu vya kuvuna kama ilivyokuwa kipindi cha ukoloni mkongwe.

Hivyo, sio rahisi kwa wananchi wa kawaida kuanzisha na kufanikiwa kufanya mapinduzi.
Hapo nimekuelewa Vizuri sana
 
Fikiri kama ingelikuwq ni niger watu wanauza bandari wanauza ngorongoro na wamasai wote wanauzwa unafikiri jeshi linaweza kukaa kimya tu
 
Back
Top Bottom