Kwanini mchango wa harusi ni muhimu

mayenga

JF-Expert Member
Sep 6, 2009
4,118
1,966
Wadau,

Hapa kumekuwepo na mada chungu nzima,zikilalamikia michango ya harusi isiyokoma.Miongoni mwa watu ambao wamekuwa hawapendezwi na uwepo wa miichango mingi Ni Mimi mwenyewe.Lakini baada ya kutafakari kwa makini,nimegundua,wale wenye kuoa au kuolewa wanahitaji michango mingi zaidi na kuungwa mkono kwa sababu zifuatazo➗
1.Sababu ya kuwa Ni vema kuchangia mtoto wa Fulani aende shule,siyo hoja kwani unapozaa lazima iwe Una uhakika wa kutunza na kusomesha.

2.Katika maisha ya binadamu Kuna sherehe,au matukio matatu muhimu,ambayo Ni kuzaliwa,kuoa au kuolewa na kufa.Kati ya matukio hayo Ni tukio moja Tu ambalo Ni ndoa,ambapo mtu anakuwa anajitambua.

3.Ndoa Ni kiashiria cha kujenga familia mpya na uumbaji.Hivyo kuwaunga mkono wahusika kufikia azima hiyo Ni muhimu.

4.Siyo vibaya kumsaidia mtu kufikia ndoto zake na furaha yake.

Nk nk
 
Michango iko too much sometimes tunalazimika kubadilisha namba za simu every 3 months,mtu hata akikuzoea kidogo tu siku ya pili anakuja na kadi damn it I don't believe it
 
michango ni muhimu lakin ya siku hizi inazidi kipimo. Mchango wa harusi ni nusu ya kiwango cha chini cha mshahara!
 
Michango iko too much sometimes tunalazimika kubadilisha namba za simu every 3 months,mtu hata akikuzoea kidogo tu siku ya pili anakuja na kadi damn it I don't believe it

nawe mpelekee
 
Hii kitu inaboa sana..unakuta mtu anakutumia sms mara nyng ili 2 utoe,,,wakat huohuo nawe una yako unayahangaikia..
 
Mimi sasa hivi nimeanza kuikaushia maana toka nimechangia pamoja na kwamba na mimi nilichangiwa ungekuta nimewekeza bonge la mradi
 
mfano my friend kitchen party minimum 80000 bado nguo,zawadi binafs na usafiri chanika hadi makongo
 
Starehe yako wewe unawapa tabu wengine, nimechangia sana hii michango lakini huwezi kuikwepa maana atatokea mtu wako wa karibu na huna jinsi.
Kikubwa usiComplicate mambo jiandae kiasi chako kwa shughuli usitake iwe baab kubwa halafu unategemea michango ya watu!!

Sent from my iPad Air using JamiiForums mobile app
 
Wadau,

Hapa kumekuwepo na mada chungu nzima,zikilalamikia michango ya harusi isiyokoma.Miongoni mwa watu ambao wamekuwa hawapendezwi na uwepo wa miichango mingi Ni Mimi mwenyewe.Lakini baada ya kutafakari kwa makini,nimegundua,wale wenye kuoa au kuolewa wanahitaji michango mingi zaidi na kuungwa mkono kwa sababu zifuatazo➗
1.Sababu ya kuwa Ni vema kuchangia mtoto wa Fulani aende shule,siyo hoja kwani unapozaa lazima iwe Una uhakika wa kutunza na kusomesha.

2.Katika maisha ya binadamu Kuna sherehe,au matukio matatu muhimu,ambayo Ni kuzaliwa,kuoa au kuolewa na kufa.Kati ya matukio hayo Ni tukio moja Tu ambalo Ni ndoa,ambapo mtu anakuwa anajitambua.

3.Ndoa Ni kiashiria cha kujenga familia mpya na uumbaji.Hivyo kuwaunga mkono wahusika kufikia azima hiyo Ni muhimu.

4.Siyo vibaya kumsaidia mtu kufikia ndoto zake na furaha yake.

Nk nk

Kwenda kanisani na kurudi nyumbani na kuendelea na ishu zenu kunahitaji michango?
 
Kwanini hiyo system tusi iweke katika mambo yenye umuhimu?

Sent from my iPad Air using JamiiForums mobile app

Muhimu kama yapi mana hata harusi ni muhimu kwa watu wenyewe wanatakaje mambo yao binafsi hizo huduma nyingne sijui shule ni another case
 
Back
Top Bottom