Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,972
- 46,738
Eneo la Mashariki ya kati ni kama eneo lenye laana fulani hivi ya vurugu. Tangu nimeanza kupata akili za kufuatilia habari sijawahi kusikiliza taarifa ya habari katika redio au TV bila kusikia kuna watu Mashariki ya wakati wamezinguana.
Yani huwa hakuna kutulia, ukiachilia mbali mgogoro wa Israel na Palestina wa kudumu utasikia Iran anazinguana na Saudia, Qatar wanataka kuzichapa na Saudia, Kuna magaidi wamelipua Iraq, Maandamano ya kuwaondoa watawala, Qatar kapigwa blocked, watu wanapora meli baharini n.k
Kila pande ukigeuka ni michakato na dili za amani!
Vita vya Urusi na Ukraine vitaisha na amani ikapatikana huku Mashariki ya kati watu bado wakiwa wanashikana mashati tu, Africa japo haina amani ila vita ambavyo mara nyingi na vya ndani ya nchi huwa vinapiganwa vinaisha amani inapatikana kama ni nchi kugawanyika zinagawanyika maisha yanaendela ila sio huko Mashariki ya kati.
Ni kwa nini Mashariki ya kati hilo eneo siku zote liko kishari, kwenye tension na watu wanaishi ngumi mkononi?