Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 18,546
- 34,438
Tanzania yote kuanzia kwa wenyeviti wa vitongoji, wenyeviti wa vijiji/Mitaa, madiwani, wabunge na Rais, kwa asilimia tisini na tisa nukta tisa tisa (99.99) wanatokana na Chama cha Mapinduzi.
Kwa ivo unaposikia CAG anaposema fedha zinaibiwa kwenye taasisi za umma ujue hapo anamaanisha wanaosimamia taasisi hizo ndiyo wanaoiba fedha hizo ama wanashirikiana na wezi hao wa fedha na mali za Umma.
Kwa kuwa serikali za mitaa na serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania zinasimamiwa na CCM, kwa maana nyingine wanaoiba mali za umma ama ni CCM ama CCM inashirikiana na wezi hao au CCM inafaidika na wizi huo, ama CCM haina uwezo wa kupambana na wizi huo wa mali za Umma.
Lakini mtu unaweza kujiuliza ni kwa nini wana CCM na CCM yao ambayo imejilimbikizia mali za umma BADO wanakwiba mali za umma!?
Kila wizi mkubwa unaohusisha fedha nyingi za umma huwezi kosa wana CCM ndani mwake na hukuti mwana CHADEMA hata mmoja. Sote tunakumbuka zile fedha za Tegeta Escrow zilivyochotwa na nani waliohusika kama si wana CCM?
Mpaka leo hatujaambiwa ni kina nani walibeba hela toka kwenye Benki ya Stanbic zikiwa kwenye mifuko ya sandarusi (Visalfeti). Kama wabebaji wa zile fedha wasingekuwa ni wana CCM leo hii wangekuwa washatajwa kitambo sana.
CCM ridhikeni basi kwa mlichotupora kwa kuzionea huruma mali za Umma.