passion_amo1
JF-Expert Member
- Dec 3, 2023
- 1,650
- 3,344
Wakuu Heshima mbele.
Mimi binafsi kwanza niseme ni mtu ambaye napenda sana kusoma historia tofauti tofauti. Nimekuwa nikivutiwa na mzee wangu Mohamed Said katika maandiko yake mengi, mzee Mohamed saidi ni mtu ambaye mara nyingi ameweza kuielezea historia Ya Tanganyika tangu harakati za uhuru zinapoanza mwanzoni kabisa, mzee Mohamed ameweza kuelezea ni kwa namna gani wazee Wa mwanzoni kabisa wa TANU ambao wengi wakiwa ni waislamu na wakaweza kumpokea mwalimu kwa upendo wote.
Mzee Mohamed Said mimi ni mtu ambaye napenda sana unachoandika. Lakini mbali na hilo watu wengi wamekuwa wakimshutumu mbali na kipaji na talanta kubwa aliyonayo ya kuandika, historia zake mara nyingi huwa zinaambatana na udini ( ZEALOTISM).
Mfano; katika moja ya komenti zake nitamnukuu hapa chini
Serikali ya awamu ya tano ilipoingia madarakani Mwaka (2015), Rais alifanya uteuzi wa Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Wilaya na Wakurugenzi mbalimbali. Uteuzi wake ulikuwa kama ifuatavyo:
Mawaziri na Manaibu: 30.
Waislamu 10, sawa na asilimia 33%.
Wakristo 20, sawa na asilimia 67%.
Makatibu Wakuu na Manaibu: 50.
Waislamu 10, sawa na asilimia 20%.
Wakristo 40, sawa na asilimia 80%.
Wakuu wa Mikoa na Wilaya: 166.
Waislamu 41, sawa na asilimia 25%.
Wakristo 125, sawa na asilimia 75%.
Makatibu Tawala wa Mikoa na Wilaya: 163.
Waislamu 24, sawa na asilimia 15%.
Wakristo 139, sawa na asilimia 85%.
Wakurugenzi mbalimbali: 249.
Waislamu 45, sawa na asilimia 18%.
Wakristo 204, sawa na asilimia 82%.
Manaibu Kamishna wa Polisi: 25.
Waislamu 5, sawa na asilimia 20%.
Wakristo 20, sawa na asilimia 80%.
Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi: 33
Waislamu 7, sawa na asilimia 21%.
Wakristo 26, sawa na asilimia 79%.
Jumla Kuu ya Uteuzi:
Waislamu asilimia 20%.
Wakristo asilimia 80%.
Hio ni moja ya komenti aliyoiandika mzee wangu Mohamed kuhusu uwiano kati ya waislamu Na wakristo. Na akaendelea chini kwa kusema kwamba:
Uteuzi huo umekuwa kama Sera kwa teuzi zinazoendelea ndani ya miaka yote mitano. Vilevile kama Mwongozo kwa wateule wenye mamlaka ya kuteuwa. Mwelekeo huo unakinzana na Katiba ya nchi ibara ya 13(4)(5), inayokataza ubaguzi wa aina zote. Kwa hakika Taifa halihitaji kiongozi wa nchi akiwa Muislamu basi ateuwe idadi kubwa ya Waislamu wenzake katika nafasi mbalimbali za uongozi wa nchi au akiwa Mkristo atumie uongozi wake kuteua idadi kubwa ya Wakristo wenzake katika uongozi nchini. Au akiwa Mzanaki ateuwe idadi kubwa ya Wazanaki wenzake katika nafasi mbalimbali za uongozi na mfano wa hayo.
Kama takwimu hizi ni za kweli mzee wangu Mohamed Said unafikiri ni nini kinasababisha kuendelea kuwepo kwa Mizani kutoku-balance?
Katika kitabu cha Kwa heri ukoloni kwa heri uhuru. Umetuonyesha ni jinsi gani makubaliano Baina ya waziri mkuu wa Kenya Ndg. Jommo kenyata na waziri mkuu wa Zanzibar Ndg. Mohamed shamte hayakufanikiwa na kupelekea kunyanga’nywa Kwa waislamu Taasisi ya (MIOME) mombasa institute of muslims education.
Mzee wangu Mohamed si mtu mwenye nia mbaya akijaribu kueleza kwa namna gani historia ya TANU haikuwa sawa kwa kiasi fulani, hivyo anajaribu kutufumbua macho zaidi. Lakini ni kama vile waislamu bado ni watu ambao kwa maandishi yake hakuna uwiano sawa na wakristo.
Mzee wangu Mohamed Said mimi naomba kufahamu kutoka kwako mbali na yote , ni kipi kifanyike ili kutengeneza uwiano sawa baina ya waislamu na wakristo katika Ngazi zote za nchi yetu? Haswa katika kipindi hichi tulichonacho elimu inatolewa kwa usawa bila kujali dini zetu.
NB. This is not intended to divisive or inflammatory only for learning purpose.