Kiswahili ni lugha ya kutengenezwa na binadamu, tatizo la BAKITA wapo tu kupokea mshahra mwisho wa mwezi, nadhani wameamini hata lugha zetu za ASILI ni 'USHENZI!'. Neno hilo lingeingizwa katika kiswahili 'badala ya kiingereza au kiarabu' lugha hii ingekuwa ya KIBANTU zaidi.Ulanzi
Ulanzi ni kinywaji kinachotokana na mmea ambao huota kwa wingi sehemu moja na hukua sana kwenda juu. Mimea hii ikiwa bado michanga hukatwa juu na ikishakatwa hutoa maji na kitu mithili ya povu hujaa juu ya pale palipokatwa. Maji hayo yanayotoka hukingwa kwenye kitu kiitwacho mbeta: halina kiswahili sahihi. Maji hayo yanayotoka ni matamu sana na tena yana uwezo wa kulewesha.Historia yake.
Inasemekana ulanzi uligunduliwa na mnyama mdogo aitwaye panya ambaye kwa mara ya kwanza walingata ule mmea mchanga wa ulanzi na maji yakaanza kutoka. Kila siku panya walionekana kupenda kulamba ile sehemu walioingata. Binadamu, baada ya kugundua hilo, walifuatilia na wakajaribu kulamba na wao, ndipo walipogundua kuwa yale maji yaliyotoka ni matamu.
Basi wakakata ile mimea michanga ya mianzi na kuona maji mengi yakitoka na kitu mithili ya povu juu yake.
Baadaye wakatumia mianzi iliyokomaa kwa kutengenezea kitu cha kukingia yale maji yanayotoka. Zinaitwa mbetaMaelezo
Ulanzi ni kinywaji cha asili kinachopendwa sana na watu wa mikoa ya Iringa, Mbeya na Songea, Kanda za Juu ya nchi ya Tanzania.
Ni kinywaji cha asili ambacho hakitengenezwi bali kinatokana na mti unaoitwa mwanzi.
Ulanzi unagemwa mara tatu kwa siku:
¨ Asubuhi: hugema na kutoa ulanzi kutoka kwenye vile vyombo vya kukingia (mbeta). Ulanzi huu wa asubuhi daima ni mtamu na togwa sana.
¨ Mchana huenda kugema kusudi kuweza kutoa sehemu iliyokauka ili ulanzi uendelee kutoka.
¨ Jioni: hugemwa tena na kutoa ulanzi uliomo kwenye vyombo vya kukingia. Ulanzi huu wa jioni ni mkali kidogo kwa sababu unakuwa umewakiwa na jua.
Ili kupata ulanzi ulio mzuri, wagemaji huchanganya ulanzi wa asubuhi na wa jioni ili uwe bora zaidi na kwa hiyo upendwe na wengi zaidi.
Utomvu:
Ni kitu kama uji unaotuama juu ya ile sehemu iliyokatwa kwenye kitindi kichanga kwa ajili ya kutoa ulanzi.
Kitindi
Ni mti ule unaotoa ulanzi. Kitindi ni umoja, vikiwa vingi huitwa vitindi na daima huwa vingi ili kupata vitindi vichanga vingi. Kitindi kikiwa kimoja huwezi kugema ulanzi kwa sababu kitindi kichanga hakiwezi kupatikana.
Hugemwa lini?
Ulanzi huu hugemwa kwa kipindi, kwa sehemu zilizo nyingi hasa kipindi cha kifuku (masika) ulanzi huwa mwingi sana na unazidi kupungua kadiri kipindi cha masika kinavyoisha. Lakini kuna baadhi ya sehemu ambazo zina baridi sana na hali ya ubichi kwa mwaka mzima, kwa mfano katika mbuga ya Kitulo, wilaya ya Makete (Tanzania).
Hunyweka kwa siku ngapi?
Ulanzi hunyweka kwa siku moja kimsingi hapo huwa mtamu wa ladha safi. Lakini ukishalala, ulanzi hupoteza ubora wake na hivi hauwi mtamu sana. Lakini ukichanganya na uliogemwa siku hiyo, hurudi katika hali njema tena, ingawa siyo safi sana.
aisee nimekumbuka idete kwenye mapera na ulanzi,lupalama B, na ipamba kwa manesi...those time are gone now....ulanzi uliwafanya wazungu wasahau wine wahamie kwenye ulanzi...kwa waliokuwepo tosa wanamkumbuka Mr. Simon na Mr. Jonathan? (kama sijakosea) hawa jamaa walikuwa wakiwa zamu tu then wakakukamata na kosa wanaomba jiti kwa ajili ya ulanzi kama adhabu.hahaaa watu wa tosa, malangali, njoss na wengineo wanamiss sana hii kitu.
aisee nimekumbuka idete kwenye mapera na ulanzi,lupalama B, na ipamba kwa manesi...those time are gone now....ulanzi uliwafanya wazungu wasahau wine wahamie kwenye ulanzi...kwa waliokuwepo tosa wanamkumbuka Mr. Simon na Mr. Jonathan? (kama sijakosea) hawa jamaa walikuwa wakiwa zamu tu then wakakukamata na kosa wanaomba jiti kwa ajili ya ulanzi kama adhabu.
mkuu kilimasera nashukuru kwa kunikumbusha ulanzi...nshazoea mnazi xaxa....but naomba nikusahihishe kidogo. mimea ya mianzi, vitindi huwa havikui sana kwenda juu....hurefuka yapata mita tano hivi then inapinda kwenda down, na pia mbeta hazitokani na mianzi (vitindi) vya ulanzi but hutokana na mianzi mingine ambayo haitoi ulanzi bali hutumiak kwa kutengenezea mbeta na bidhaa zingine kama vitanda, nyungo, vikapu nk.
ulanzi uliokomaa sana unaitwa kilama, huu ulanzi ni full spirit kwani ukimwagia kwenye majani yanaungua,na ukiunywa bila kuchanganya na togwa afya yako ni hatihati.
Mi mpenzi wa mkangafu na mdindifu
duh mdindifuna ule unaofukiwa chini unaitwa mdindifu ve mwagito
Aah vemdimi pede ulikuwulasiPede ve kelwike, vigusa kwiya de pa mwani ipa?
Twevanyandolo twatwinywa umkangafu sio itogwa!
Pe twinywa na ilidondo likwima nige lisaka umung'inetu tuhunyunile
wataalam wa lugha tunaita mabosoUtomvu:
Ulanzi