Kwa ulimwengu huu wa sasa Fani ya Procurement bado inafundishwa vyuoni kwa sababu gani?

The Evil Genius

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
5,543
17,573
Baadhi ya vyuo Duniani vimekuwa vikifanya mabadiliko ya mitaala na kufuta ama kuachana na fani ambazo haziendani na wakati.

Bado najiuliza, kwa Dunia ya sasa fani ya Procurement inafundishwa vyuoni kwa sababu gani? Ni fani ambayo haina umuhimu wowote kwa karne hii ya 21.

Mtoto akisoma Procurement basi umuhimu wake ni aajiriwe Serikalini zaidi ya hapo fani haina umuhimu wowote,na haina msaada wowote kwa mhitimu. kwanini iendelee kufunishwa vyuoni?

Hii fani ilipaswa kuwa sehemu ya course za watu wanaosoma finance/accounts lakini sio kuwa independent course.

Wakati tunafanya mabadiliko ya mitaala ya elimu, tusisahau ya vyuo vikuu. Vyuo wao wanachotaka ni hela tu kwa kuanzisha fani sizizo na maana yoyote ambazo hazina msaada kwa wahitimu.

Fani ya Procurement inapaswa kufutwa. Mzee Kishimba aliwahi kuuliza, mtu anasoma fani ya manunuzi ananunua nini?
 
Makampuni makubwa Kama haya duniani yanajua umuhimu wa procurement and logistics management, wewe kichaa mmoja tu ndo unataka ifutwe be ashamed
Screenshot_20221015-153751.jpg
 
Mbona wanauhitaji sana mkuu. Mtu wa store anayecheza na stock ya store ni muhimu sana eneo lolote ambapo kuna store kama hotelini, mgahawa, gereji, hospital, popote pale ambapo kuna store.
Mkuu, graduate wa procurement anawezaje kujiajiri akimaliza chuo? Hayo uliyoandika hapo juu ya stores za hospital na hotelini hata mhitimu wa kidato cha sita anaweza kufanya.
 
Mkuu, graduate wa procurement anawezaje kujiajiri akimaliza chuo? Hayo uliyoandika hapo juu ya stores za hospital na hotelini hata mhitimu wa kidato cha sita anaweza kufanya.
Huujui umuhimu wa procurement Sababu hauhusiki nayo, kawaulize ma supplier wakubwa dunia watakuambia umuhimu wa procurement ni Nini

By the hamna mradi unaeza fanyika bila kuhusisa kitengo cha procurement
 
Makampuni makubwa Kama haya duniani yanajua umuhimu wa procurement and logistics management, wewe kichaa mmoja tu ndo unataka ifutwe be ashamedView attachment 2387926
Nadhani kuna vitu huelewi kwamba Procurement na logistics ni vitu 2 tofauti.

Procurement is different from logistics.

Simply put, procurement is the buying or purchasing of goods or services. Logistics is the movement, storage, and operations around the utilization of purchased goods and services for whatever business the company is in.

Hapo naamini nimekusaidia kuelewa kidogo.
 
Hamna namna unaweza itenga procurement and logistics
 
Huujui umuhimu wa procurement Sababu hauhusiki nayo, kawaulize ma supplier wakubwa dunia watakuambia umuhimu wa procurement ni Nini

By the hamna mradi unaeza fanyika bila kuhusisa kitengo cha procurement
Mkuu, mimi niliwahi kufanya kazi katika construction industry kwa muda fulani. Nilichoshuhudia kwa muda wote huo ni kwamba, watu wa kidato cha nne na sio ndio wanafanya hizo kazi za manunuzi na sio graduates. Kwa mazingira ya Tanzania hiyo kozi ipunguze udahili wa wanafunzi.
 
Back
Top Bottom