Kwa rushwa wanazokula wafanyakazi wa nchi hii wasiongezewe mishahara kabisa

Arovera

JF-Expert Member
Nov 19, 2013
11,082
28,874
Ukweli uko hivo.

Anzia mahakamani, polisi, hospital na idara nyingine kote wanajilia rushwa kama wametumwa. Sasa hawa watu hawafai kuongezewa mishahara maana wanazoiba ni nyingi mno.

Wafanyakazi waingie makubaliano na serikali wakiacha rushwa ndio waongezewe mishahara na marupurupu mengine.

Tofauti na hapo wasiongezewe chochote kabisa.
 
Kada ya ualimu ndio kada isiyo na rushwa na ndio kada iliyo barikiwa kisha zingine ndo zitafatia badae
 
Ifuatayo ni orodha ya kada zinazokula rushwa, walimu hawapo kwenye orodha hii
 
Umeonesha upeo mdogo sana kwenye kujenga hii hoja yako. Maana hiyo serikali unayotaka iingie makubaliano na wafanyakazi, ndiyo inaongoza kwa vitendo vya rushwa.

Ndani ya hii nchi, ni wafanyakazi wachache sana wanaonufaika na hivyo vitendo vya rushwa. Ila ukija kwenye majority, hali ya maisha yao ni tete.
 
Msingi wa maada yangu ni kuinua hasira ili watumishi wapate ari na molari ya kudai haki zao, kwanza nakuunga mkono kua wanufaika wa rushwa ni wachache, kati ya watumishi laki sita labda wa serikali ni laki moja ndio hufikiwa na rushwa wengine hali ni mbaya
 
Rushwa sio kipato halali, poa si wafanyakazi wote wanakula rushwa ni kikundi cha wachache so hoja yako bado haina base
 
Umeonesha upeo mdogo sana kwenye kujenga hii hoja yako. Maana hiyo serikali unayotaka iingie makubaliano na wafanyakazi, ndiyo inaongoza kwa vitendo vya rushwa.

Ndani ya hii nchi, ni wafanyakazi wachache sana wanaonufaika na hivyo vitendo vya rushwa. Ila ukija kwenye majority, hali ya maisha yao ni tete.
Nadhani sasa kwenye ile molari ya kudai haki kada wasizolipwa malipo ya ziada, mawasiliano na ama usafiri wataanza kusema na kufikiriwa, mambo ni mengi Kwa mtazamo lakini nitakua naanzisha maada za kuudhi ili wapate ari ya kudai stahiki zao
 
Kwani serikali haina Sheria dhidi ya rushwa? Kwanini serikali isitumie hizo Sheria kupambana na watumishi unaosema wanakula rushwa? Wafanyakazi wanakula rushwa while wanasiasa wanafanya ufisadi. Ngoma droo, wananchi ndio nyasi mnaumia.
 
Ukweli uko hivo
Anzia mahakamani, polisi, hospital na idara nyingine kote wanajilia rushwa kama wametumwa,
Sasa hawa watu hawafai kuongezewa mishahara maana wanazoiba ni nyingi mno.
Wafanyakazi waingie makubaliano na serikali wakiacha rushwa ndio waongezewe mishahara na marupurupu mengine.
Tofauti na hapo wasiongezewe chochote kabisa.
Siyo kila mtu anakula rushwa.
Kada ya ualimu ndio kada isiyo na rushwa na ndio kada iliyo barikiwa kisha zingine ndo zitafatia badae
Nyie ndo hamfai kabisa, mnachangisha michango kwa wanafunzi, mara tusheni, mara mitihani etc.
 
Back
Top Bottom