Kwa mtaji wa milioni 12, nifungue hardware, nafaka au phone and accessories?

Teacher, nenda na biashara ya simu na vifaa vyake. Halafu unaongezea ndani yake na huduma za kifedha. Hakika utanishukuru kwa huu ushauri.

Na uzuri umekiri mwenyewe machimbo yote ya hivyo vifaa pale Kariakoo unayafahamu. Kwa hii biashara ni rahisi kwako kuisimamia.

Achana na biashara kichaa ya mazao, na pia hiyo ya hardware ambayo kuna wateja wanataka wapelekewe bure mpaka site, hata mfuko mmoja tu wa saruji!
Shukrani mkuu
 
Yeah Kuna mtu alinambia hii, mfano debe la maharage vijijini ni 2000 unamwambia wakala Kila debe unampa 500, Sasa ni speed yake kutafuta then Kila weekend unaenda kuchukua mzigo.
Vijijini ukiwa unamuwekea hata kwa gunia buku 5, mtu anakupambania sana yaani, unaweza hata kuwa na bodyguard kwa hio hela. Mawakala ndo kila kitu
 
Teacher, nenda na biashara ya simu na vifaa vyake. Halafu unaongezea ndani yake na huduma za kifedha. Hakika utanishukuru kwa huu ushauri.

Na uzuri umekiri mwenyewe machimbo yote ya hivyo vifaa pale Kariakoo unayafahamu. Kwa hii biashara ni rahisi kwako kuisimamia.

Achana na biashara kichaa ya mazao, na pia hiyo ya hardware ambayo kuna wateja wanataka wapelekewe bure mpaka site, hata mfuko mmoja tu wa saruji!
Biashara ya vifaa vya simu inataka usimamizi especially kama akiongeza na uwakala, alafu kwa hio capital bado ni ndogo kufanya uwakala akapata hela inayoeleweka. Hapa nazungumzia experience kabisa. Nafaka zina hela mzee, hio hela anai double chap sana. Maana gunia zinakuja na vipimo kama ni mahindi ni gunia za kg 128 na inajulikana bei zake.
 
Watu wakigoma wanasifika kwa ujanja ujanja wa Elimu Dunia,wakija mjini huku tunaona sifa zao, hustle,hela zao za moto,wewe umeenda kwao l,haitakua rahisi,but inawezekana,..

Usifikiri mtu wa dar au Mwanza atakupa idea itakayo work out kigoma,,wewe mwenyewe jipe muda tembea mji wote,usome kwa jicho la MTAFUTAJI,andika fursa tano tu ambazo umeziona Kigoma,andika mchanganuo, pick the best one,,

Mimi Kigoma nimefika,mji huo mgumu,jaribu kuuza HUDUMA,sio Merchandise
 
Kosa lako ni kutaka mafanikio kupitia biashara lakini kazi hutaki kuacha, nakuhakikishia Mimi kuwa utumishi wa umma na kipato kikubwa ni mbingu na ardhi na mchawi muda na usimamizi kwa sababu unataka ukabidhi watu walifanyie kazi itakula kwako na huwezi kuwa mtumishi wakati huohuo kuwa mfanyabiashara angalau ungekuwa DC, DED, RC etc lakini kazi ya ualimu halafu unataka kutusua you should not be serious na kitakacho kuumiza ni uoga vinginevyo hiyo hela itapotea na hutaelewa imepoteaje kama unataka kufanya biashara chukua maamuzi ya kufa umesimama otherwise endelea kuishi umepiga magoti
Walau aombe liziko ya miaka miwili akomae na biashara ndo acheki namna ya kumweka mtu
 
Hapo nashauri fungua 👉 phone's accessories....
Hii nahakika haitokuwa na competition kubwa kwa sababu kuu ifuatayo
👉Wafanyabiashara wengi wa mikoani huwa hawana connection ya moja kwa moja Dar (ambako vitu hupatikana kwa bei rafiki)
Wengi hupitia changamoto ya kukosa watu waaminifu kuwatumia mzigo bila janja janja...

Kwahyo kama wewe unaconnection nzuri ya kutoa mzigo Dar,,,, lazima uwakimbize

USHUHUDA: Kuna mwaka flani huko nyuma nilienda mwanza.... Katika moja mbili tatu nikapata wazo la kuagiza mzigo wa handbag Dar, product ya 5000 nilikuwa nauza 15000
Wafanyabiashara nilowakuta pale kila siku wimbo wao ulikuwa niwaunganishe ninakochukulia mzigo

(Hapo ndipo nikagundua ukiweza kuiconnect Dar na mikoa ya mbali Kuna pesa asee🚶🚶
 
Back
Top Bottom