Habari zenu Wakuu,
Kwa hizi siasa zinavyoendelea nchini sidhani kama raia wanaojaa kwenye mikutano ya kiasiasa wanakuwa wanaenda kweli kusikiliza sera, hasa wale wanaojaza wasanii kibao utafikiri wanafanya tamasha.
Kila mtu sasa hivi ni chawa, viongozi ni chawa ili kubakia kwenye nafasi zao na wananchi wanakuwa chawa kwa kufanya lolote ili kupata nafasi ya kula sehemu ya mema ya nchi.
Ndio tumefikia huku? Kiongozi unaona sifa kusifiwa, unajifanya hupendi na kukemea lakini unaacha viendelee, wanaosifia ndio wanapata nafasi wakati wanaokukosoa wanakula joto ya jiwe au hawapati nafasi za kuongoza huku kila mtu akiona uwezo wao mkubwa wa kufanya maamuzi!
Ina maana viongozi wameishiwa sera na mipango ya kuiuza kwa wananchi ili wawakubali? Kuna uwezekano wa viongozi hao kutoboa bila kutumia ushawishi wa wasanii wanaombatana nao?
Mna maoni gani kweny hili wakuu?
CC johnthebaptist Lucas Mwashambwa Mshana Jr Erythrocyte