SoC02 Kutoka Geita mpaka Wuhan - Stori ya kweli

Stories of Change - 2022 Competition

Trump Jr

Member
Jan 19, 2017
26
35
Mwaka 2014 February majira ya baridi kali yakiwa yanamalizikia Jiji Wuhan China ndipo mwandishi wako nilifika Uchinani baada ya kupitia changamoto mbalimbali.

Ilikuwa ni safari ya miaka sita ya masomo katika Jiji la Wuhan, Jiji lenye uchumi mkubwa katika Central China, Wanafunzi wa kigeni na wenyeji wamezoea kuliita Jiji hili kama "Academic City" kwa sababu ya kuwa na idadi kubwa ya vyuo vikuu ambavyo kwa idadi kubwa hupokea wanafunzi kutoka mataifa mbali mbali hasa Africa.

Kuna habari nyingi sana kutoka China, lakini leo nataka nikujuze msomaji wangu kuhusu mwanzo wa urafiki wangu na kijana wa kichina mpaka tukapanga safari ya kuja Tanzania na kutembelea mikoa kadhaa.

Mwanzo wa urafiki wetu ilikuwa ni katika viwanja vya mazoezi ndani ya chuo nilichokuwa nasoma, kama kawaida yangu huwa napenda kufanya mazoezi kila jioni baada ya masomo. Bila kujua kinachoendelea, kumbe alikuja kijana wa kichina mwenye siha njema aliponifuata kwa shauku kubwa sana akitaka kuzungumza na mimi, aliongea kiingereza cha kuungaunga, nilimwelewa na mimi nilimtoa hofu kwa kumwambia nafahamu kuongea kichina “我会中文” maana tayari nilikuwa nimekwisha kaa China kwa zaidi ya miaka miwili.

Rafiki huyu alishangaa sana kuona naweza kuzungumza kichina, hii ikachagiza urafiki wetu, kumbuka nilikuwa kwenye moja ya viwanja vya mazoezi ndani ya chuo lakini chenye hadhi sawa na "Lupaso" The Benjamin Mkapa Stadium. Baada ya mazoezi tulipata kunena mawili matatu, alivutiwa na usakataji wangu kabumbu, alisifia na kunipa jina la "Yaya Toure" mchezaji wa zamani wa Barcelona na Manchester City kutoka Taifa la Ivory Coast, japokuwa yeye ni shabiki wa Chelsea kama mimi na nimfuatiliaji wa ligi kuu Uingereza (EPL)

Maisha ndani ya Uchina yakaendelea kama kawaida, mara nyingi ratiba zetu za Wikiendi tulipanga pamoja, tulicheza mpira pamoja na pia nilimfundisha baadhi ya vyakula vya kiafrika nilivyokuwa nampikia ili apate stamina, alipenda Ugali na Chips Zege.

MIPANGO YA SAFARI KUJA TANZANIA.

Mapema sana mwaka 2019 majira ya joto tulipanga ratiba ya kuja Africa - Tanzania, alikuwa na shauku kubwa na maswali ya mara kwa mara juu ya usalama katika maeneo yetu kwani ilikuwa ni safari yake ya kwanza nje ya nchi. Alikuwa akiwaambia rafiki zake wa kichina kwamba sasa nakwenda Africa - Tanzania.
Tulikwenda kwa wazazi wake na wao wakatoa baraka za kusafiri pamoja na kijana wao huku wakitutaka tuwe makini na tusiwe wagomvi na mtu yeyote safarini.

Wiki kadhaa kabla ya safari kulitokea machafuko Africa Magharibi pamoja na ile habari ya wachina kukamatwa nchini Kenya, haya matukio ilikuwa ni habari kubwa sana kwake, alikuwa akitumia muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii kufuatilia habari za Africa hasa Africa Mashariki, nilifanya kazi kubwa ya kumuondoa hofu, nilimwambia uharifu upo Dunia nzima, waharifu wapo kila nchi lakini serikali zetu zipo kazini kupambana na kila aina ya uharifu, nilimwambia kiwango cha uharifu katika nchi yetu Tanzania ni mdogo sana kulinfanisha na nchi zingine Africa, aliniamini kwani hata yeye alikuwa akijilidhisha kupitia data mbali mbali kwenye mitandao.

AIRPORT JNIA TERMINAL II.

Safari ilikuwa ndefu ikichukua takribani saa 18, kwani tulipanda ndege za shirika la ndege Ethiopia Airlines hivyo tulipita Jijini Addis Ababa kubadilisha ndege na kushuka Dar es Salaam majira ya saa kumi na moja jioni, tulipokelewa na joto kali na changamoto ya foleni kwenye kukaguliwa na kusubiri mizigo yetu, kumbuka tumetoka katika Jiji lenye uchumi mkubwa, Jiji la tano kwa utajiri China, likiwa na Airport hadhi ya nyota tano, "The rest is history"

Rafiki yangu alipenda namna tunavyoishi Tanzania, tulitembea mikoa kadhaa, alipenda vyakula vyetu hasa vile vya Zanzibar, alikuwa akiniambia ona nimenenepa kwa muda mfupi tu, tulikwenda mijini na vijijini na habari hii ni ndefu pia.

LENGO LA KUANDIKA HABARI HII.

Pamoja na mambo mengi tuliyoongea na kuyaishi nchini Tanzania, rafiki yangu alinidokeza kwamba nyie ni matajiri sana lakini kwanini huwa mnakwenda China na nchi zingine kuomba misaada? Swali hili lilinipa wakati mgumu kidogo, rafiki yangu huyu ni mdadisi kweli kweli na huwa akiandika kila kitu cha muhimu, nilianza kuvuta picha tokea siku tunafika Airport JNIA maana alikwenda msalani pia, aliona alichokiona, barabara zetu, usafiri wetu, na mambo mengine kedekede.

Rafiki yangu aliniambia ameona magari ya bei kubwa sana barabarani, aliniuliza kwanini nchi ambayo inaibukia kiuchumi inunue magari kama yale maana kipindi China inajenga uchumi wake ilikuwa ni haramu kuona magari kama yale, kizazi cha sasa nchini China ndiyo kinaweza kumiliki magari kama yale, ndugu msomaji wewe ungejibu vipi?

Binafsi nilimwambia baadhi ya magari haya ni ya watu wachache wenye uwezo na mengine mengi ni ya viongozi wa serikalini, aliniambia kwanini serikali itumie gharama kubwa hivi kwenye luxury na siyo kuwekeza kule vijijini ili kila sehemu pawe na huduma za muhimu, nilimwambia kila sehemu itafikiwa na maendeleo, kazi ya kuleta maendeleo siyo ya siku moja.

Sijui kama aliridhika na majibu yangu lakini niliendelea kumuona akibaki na maswali mengi kichwani, tulimaliza ziara zetu kwa kutembelea kanda zote walau mkoa mmoja au miwili, aliahidi akirudi tena Tanzania tutakwenda Ziwa Tanganyika.

MWISHO.

Rafiki yangu alitangulia kurejea kwao China baadae nikafuatia, tulikutana tena Wuhan tukaendelea na maisha na masomo mpaka nilipohitimu shahada yangu ya kwanza, tumekuwa marafiki mpaka sasa.
 
Nmejifunza kitu
 
Ninalikumbuka jiji la Wuhan eneo la kati ya China. Si mbali sana na three gorges hydropower station kinacho zalisha umeme wa zaidi ya 22,000MW
 
Ulifanya kosa kumdanganya , ungemwambia ukweli kuwa nchi yetu Kuna mchwa mafisadi wanaoiba na kurudisha nyuma maendeleo, akija kugundua ukweli atakudharau sana.
 
Stori nzuri ila umeinyima nyama.. ilistahili mwendelezo!
 
Back
Top Bottom