Kusafiri nje ya nchi kwa viongozi wa kisiasa na hata wale makinda wa kisiasa ni jambo jema

winnerian

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
336
530
Wengi wanahoji kwanini Rais SSH anasafiri sana nje! Jibu ambalo linahitaji mtazamo mpana sana ni kwamba KULE NJE ANAKUWA "EXPOSED" NA MAZINGIRA YA KIMAENDELEO na namna dunia inavyosonga mbele kwa kasi. Kwa mtazamo huu utagundua kila safari inamuongezea uchu wa kutaka kuiona Tanzania inajitahidi kufikia ile kasi ya maendeleo ambazo nchi nyingine zimeshaifikia.

Piga picha wewe kama wewe uwe kila siku unafanya safari zako kutoka kijijini kwenu kule ndanindani kabisa kwenda tena ndani zaidi kwa bibi na babu kuwasalimu na kufanya mizunguko mingine isiyokuwa muhimu. Imagine fikra zako zitakavyobaki mgando kutokana na kutojifunza chochote kutoka kwenye mazingira ambayo hayakujengi kimtizamo wala fikra. Wenzako wanaokimbilia mijini na majiji watakupiku parefu sana kimaendeleo.

Mh. Rais ni ushauri wangu uendelee na safari za nje na pia utoe mwanya na kwa mawaziri pamoja na wale wote wanaoweza kwenda huko nje kutuletea mawazo mapya ya kutufanya tupate maendeleo kwa haraka.

Kukaa tu hapa ndani na kuzunguka wilayani kutafuta kesi ya nani kaibiwa kuku wake sisi kama taifa kwa ujumla hatutapata manufaa yeyote yale na badala yake tutazalisha viongozi mgando na wenye mtazamo hasi na very very primitive.
 
Exposure na experience ni muhimu kuliko 'knowledge'. Ili kuwa kwenye nafasi ya kufanikisha mambo makubwa inapaswa kuwa na vyote vitatu kwa umuhimu wake.

1. Exposure
2. Experience
3. Knowledge
4. Wisdom
5. Kuzungukwa na watu wenye 1-4 hapo juu.
 
Umeelezea vizuri sana,tunamuunga mkono asilimia mia.Katika familia,wapo wenzetu waliishia kijijini,hawakuwahi kutoka hata nje ya Kijiji,ukifika waliko wako na mawazo ya miaka 1840,,kila unachowaelezea na kuwaonyesha picha,hawaamini kama dunia iko hivyo,kwenye picha,wanazoziona.
 
Exposure na experience ni muhimu kuliko 'knowledge'. Ili kuwa kwenye nafasi ya kufanikisha mambo makubwa inapaswa kuwa na vyote vitatu kwa umuhimu wake.

1. Exposure
2. Experience
3. Knowledge
4. Wisdom
5. Kuzungukwa na watu wenye 1-4 hapo juu.
Exactly ndio maana nikashauri awaruhusu pia na mawaziri na wengine ikiwezekana
 
Wewe umetumwa nini, the pandemic is not corona but our infantuation with Samia. Eti kale ya maji, Bara Bara etc ni kodi yetu hiyo nyinyi wapumbafu! Samia Hana hela. She is egotistical President
 
Hakuna nchi imeendelea kwa kujifungia.

Hayo maendeleo ya China, Vietnam, India etc yote yametokana na uwekezaji kutoka nje ya nchi, FDI ni kitu muhimu kupita kiasi.
 
Wewe umetumwa nini, the pandemic is not corona but our infantuation with Samia. Eti kale ya maji, Bara Bara etc ni kodi yetu hiyo nyinyi wapumbafu! Samia Hana hela. She is egotistical President.
Stop emotional instability and attack the agenda with much more reasoning atmosphere
 
Ambaye alikuwa hataki kusafiri alikuwa anaogopa vitu viwili;

(1) Kwa vile alikuwa amewekewa defibrillator kwenye kifua KUONGEZA kasi ya mapigo ya moyo, ilikuwa ni hatari kwake kusafiri na ndege safari ndefu. Ndiyo maana akabakia kuwa Rais wa kuzurura Msamvu, Sekenke, Kahama na Chato. Usidanganywe kwamba Magufuli eti alikuwa anabana matumizi, HAPANA

(2) English ilikuwa ni tatizo kubwa kwake. Unapotoka nchi iliyotawaliwa na Mwingereza na unadai una PhD halafu unasema "people used to die in ze rake" lazima utaonekana kituko.

Muacheni Samia mwenye Afya inamruhusu na English anapiga kisawasawa aendelee kusafiri vile anavyodhani inaleta tija kwa nchi yetu
 
Makamba bwana
 
JK alitumia Muda mwingi sana kuruka angani alisaidia nini nchi?
1645941908773.png

Miaka yote ya Magufuli hakuwahi kufikia FDI record ya JK...
 
Vitaje alivyovifanya
1.
2
Daraja la Kigamboni
2. Daraja La Kilombero
3. Daraja la Umoja
4. Daraja la Maragarasi
5. Chuo Kikuu cha Dodoma
6. Hospitali ya Mloganzila
7. JNIA terminal III
8. DART(Mwendo kasi)
9. Sekondari za Kata nchi nzima kila kata ina shule.
10. Mradi mkubwa wa maji wa Ziwa Victoria
11. Songwe Airport
12. Kigoma Airport
13. Tabora Airport
14. Umeme wa REA
15. Benjamin Mkapa hospital Dodoma
16. Chuo kikuu cha Nelson Mandela Arusha
17. Dangote industry
18. Bomba la gesi Mtwara Dar
19. Kinyerezi I&II
20. Hospitali ya Moyo
21. MOI
22. Nchi nzima kuunganishwa kwa barabara za lami(zaidi km 14000 zilijengwa nchi nzima)
23. Umeme kwa makao makuu ya wilaya
24. Kuvusha Umeme Zanzibar
25. Ujenzi wa Mkongo wa taifa wa mawasiliano(leo tunajimwambafai na internet matunda ya JK)
26. JNICC Conference center(Ukumbi wa kisasa)
27. Hata CCM wenyewe aliwajengea ukumbi wa kisasa Dodoma.
28. Nyongeza ya mishahara kwa watumishi kila mwezi julai
29. Ajira kila mwaka
30. Annual Increment ilikuwa haki ya Mtumishi.
32. Diplomasia ya kimataifa ilikuwa juu katika ukanda wa maziwa makuu.
33. Demokrasia iliyopevuka
34. Aliwagomea CCM na kuwaambia hoja za kisiasa hujibiwa kisiasa, sio kwa kipigo cha polisi.
 
M

Vyote ulivyovitaja vilikuwa ni upigaji mkubwa na wizi mkubwa kwa kuanzia hilo daraja la kigamboni.

Chuo kikuu cha Dodoma ulikuwa upigaji mkubwa haramu africa.
 
Alishindwa kukutana kodi moja kwa moja. Jifunze mfumo wa Control number ulioanzishwa na JPM utajifunza kitu.

Jifunze kurudisha uteuzi wa wakurungezi wa Halmashauri kupitia ikulu utajifunza kitu.
Jifunze kuhusu kuanzishwa kwa TARURA utajifunza kitu kuhusu madiwani na fedha Za Barabara
Jifunze kuhusu SGR utajifunza kitu.
Jifunze kuhusu bwawa la umeme la Julius nyerere utagundua kitu ukifananisha na Kinyerezi one.
Jifunze kuhusu utumbuaji utajifunza kitu
 
Bahati mbaya sana kutokana na culture na tabia zetu watanzania za kutojua tunachokitaka hatujawahi kuwa na raisi aliekamilika kwetu.
Hatujui kama hatujui... ndio changamoto kubwa. Speed ya JK ingeendelezwa na Magu tungekuwa mbali zaidi, endeleeni kuvutia wageni na uwekezaji, huku ukipambana na ufisadi.... mwenzetu akasahau ya muhimu akaleta stupid nationalism.
 
Unafiki tu mbona kwa jiwe mlisema safari za nje hazina tija. Mlisema mabalozi walioko huko wanatosha.

Wameninyima viza tu ningeenda North Atlantic Terrorists Organization (NATO).

Sent from my SM-A022F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom