Ahmed Ally: Si jambo jema hata kidogo Serikali kutoa Posho ya 1.2M pamoja na Usafiri kwa Mashabiki wa Yanga, Mpira ni Starehe

Heparin

Senior Member
Sep 24, 2021
150
564
1000020299.jpg

Baadhi ya Mashabiki wa Simba waliojilipia nauli zao kusafiri kwenda kuipa support timu yao Nchini Misri

Kila shabiki amejilipia Dola 1200 sawa na Milioni 3,126,000.

Hili swala la Serikali kusafirisha Mashabiki nitatoa maoni yangu nikimalizana na Al Ahly, Sasa hivi akili inawaza namna ya kufuzu Nusu Fainali, Ila msimamo wangu ni kwamba si jambo jema hata kidogo.

Kwa Mashabiki mpira ni starehe hivyo Serikali haiwezi kugharamia watu kwenda kustarehe.

Tena bora ingekua imetoa usafiri tu. Lakini wametoa Posho Dola 500 kila kichwa sawa na Milioni 1,200,000 kwa ufupi hawa Mashabiki wamenuniliwa na wanalipwa kuishangilia timu yao.

Na hao sio Mashabiki wa kawaida ni Machawa wanaotetea maslahi ya viongozi wao yaani Serikali imelipia Machawa wa watu.

Kuwalipia nauli sio kuwapenda ni kufuga tatizo ambalo baadae hatutaweza kulitatua.

Leo unalipia mashabiki wa klabu, kesho Ali Kiba ataiomba Serikali iwagharamie mashabiki wake kwenda Marekani kufanya show utamnyima?

Twaha Kiduku ataomba aende kupigana Uingereza na mashabiki wake utamnyima??

Halafu nyie Nyuma Mwiko acheni kuzuga huwezi kulipia nauli watu 48 ukajidai eti unawapenda mashabiki zenu, Wakati kwenye mechi yenu juzi Mashabiki wameumia, wamepigwa mabomu ya machozi, watu wamepata vilema, na hamjasema chochote halafu uje uzuge eti unawapenda watu wenu.

Ndugu zangu wana Simba hili swala lisiwatie unyonge na wala Serikali yetu haina nia ya kufanya ubaguzi.

Sisi tuendelee na utamaduni wetu kujisimamia tukipata msaada tutachukua lakini katu tusilemae kusubiri dezo.

We are Simba Sisi ni Wakubwa, Sisi ni Wafalme, Sisi tuna hadhi kubwa

Lets focus na mechi yetu ya Ijumaa.

Pia soma: Rais Samia kununua kila goli Tsh. Milioni 5 mechi za Simba, Yanga CAF
 
Yanga walionyesha uzalendo kuruhusu wananchi watanzania kuingia bure uwanjani katika mechi kubwa hivyo kuchangia kukuza soka! Pia Yanga imeshiriki fainali za CAF na kutwaa medali na kwa sasa ndiye timu inayoongoza kwa kutwaa kombe la ligi mara nyingi kuliko club yoyote! Kwa hili naona serikali iko sawa kabisa kurudisha fadhila.
 
Dollars 500* 2507 = 1253500

1253500*48 sawa na milion 60,168000 hzo Ni posho tu Bado

Nauli
600000* 48 sawa na milion. 2880000

Jumla kuu milion 88968000
Hizo Ni pesa zimekwenda kutumika nnje ya bajeti kuu
Serekali hi hiwezi kuishi kweny bajeti yake inachota pesa hazina ianvyo taka
 
Mbumbumbu Fc kwasasa ni Bora mkae kimya msubiri Maumivu yaishe ndio muongee.
Mnaongea vitu vya kipuuzi kuliko upuuzi wenyewe.
Inaongewa kuhusu kodi ya nchi kutumiwa hovyo kwa wapenda dezodezo.Wewe kalumekenge unapinga.Hili suala lilikuwa siri.Siri imefichuka.Yanga mna mdhamini anayejiita "tajiri"!Nini kimemshinda kugharamia washabiki wenu?Jambo hili Naibu Waziri Mwinyjuma ana la kujibu.
 
Back
Top Bottom