Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Muundo upi wa Muungano unafaa?

  • Serikali 1

    Votes: 81 23.3%
  • Serikali 2

    Votes: 22 6.3%
  • Serikali 3

    Votes: 241 69.5%
  • Sijui

    Votes: 3 0.9%

  • Total voters
    347
  • Poll closed .
Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 inasema kuwa maoni ya kutokuwepo kwa Muungani ni marufuku! Wewe unazungumzia "Nchi Mbili Huru" maana yake hakuna Muungano! Just imagine zile States za Marekani kila State moja iwe na kiti UN ku-represent nchi moja (USA) Sijui kwa nini suala la Muungano linawafanya watu ku-lose focus kiasi hiki!
Na hilo la ku-refer Katiba ya JMT, 1977 ni sawa kwa kuwa ndio inayotumika, au ulitaka nirejee rasimu ya Katiba Mpya? Be serious, plse!
Ni kwamba watu wanatamaa ya Uongozi. Ila kimsingi hakuna unuhimu wa kua na Serikali 3.

Kama tunataka Muungano ulio qa kweli, Serikali ni Moja ila iwe ya Majimbo ku deligate power kwa wazawa wa sehemu husika.

Serikali 3 ni kutaka kugawana Madaraka na posho tu hakuna kipya.

Niko palee nawasubiri
 
Ndugu mtanzania

Toa sababu za kitafiti, Kwa nini unasema Serikali Moja ?
MiMi naongelea kiuchumi zaidi.
Hivi hii pesa ya serikali ya tatu si ingesaidia kuwaajiri walimu kujenga maabara na karakana ili kuongeza ubora wa elimu? Kuna nini zaidi kipya zaidi ya kuongeza fursa kwa wanasiasa. Kirusi cha yote haya ni wanasiasa ambao wanajali matumbo yao baada ya kufikiria jinsi gani kuikwamua nchi ilipo wakati miaka ya 80 uchumi ulikuwa sawa na nchi kama Malaysia na Indonesia.
 
Nikama wanaforce sherehe hizi za muungano lakini hawako wazi na maendeleo, Siasa ndio zinawaumiza
 
Sababu kiuhalisia wanaopigania serikali tatu ni wanasiasa tu, wanalinda vyeo na madaraka yao. Mfano ukienda zanzibar, ukaangalia mikoa na wilaya zilivo ni usanii tu, kutoka mwenge hadi ubungo mataa tayari ni mikoa miwili na wilaya zake, zenye mamlaka kamili. Mimi kwangu ni usanii tu huu wa kulindiana chakula, na vyeo na sababu wananchi kwenye mada hii tunaamuliwa na wanasiasa/walinda vyeo bhasi tunabusruzwa tu tupiganie vyakula vyao. Hata wanaosema sejui mamlaka kamili ya Tanganyika, inakusaidia nini kama mwananchi wa kawaida?, ni vyeo tu vya watu na matamanio yao. Kwahiyo serikali iwe moja tu, na swala la muundo wa muungali lisiwe mada kubwa kuliko zote kwenye katiba mpya. Kuna mambo mengi mengine ya muhimu yanayohusu maisha na maendeleo ya watu wa kawaida.
 
Back
Top Bottom