Kupanda kwa bei ya mazao iwe fusra ya kuwekeza kwenye kilimo

chiembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
12,369
21,244
Ni wazi Sasa kwamba,utajiri uko shambani, kupaa kwa bei ya mazao iwe alama ya kijani ya kutuelekeza turudi shambani, na tuwekeze katika kilimo.

Mtu amekaa mjini anasubiri mwenzake wa shamba aingie gharama kulima, halafu aje amuuzie mazao kwa bei nafuu!

Huko huko mjini, wa Kijijini wakija kupanga nyumba au kukodi gesti, gharama ziko juu. Kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake. Zamani mlizoea mkulima alime, wakati wa kuuza mnamzuia asiuze kwenye bei nzuri, matokeo yake vijijini pakajaa umasikini, watu wakakimbia kilimo. Kuanzia mwakani kilimo ndio habari ya mujini.

Tuachane na bodaboda na bajaji na umachinga.
 
Sasa wote mkienda kulima bodaboda na shuguli zingine watafanya wakina nani

Ova
 
Jidanganyeni, kilichotokea mwaka huu kinaweza kisitokee tena
 
Back
Top Bottom