- Source #1
- View Source #1
Salaam,
Nimesikia mtaani wanawake wanaambiana kuwa Kunywa maji ya Baridi wakati wa Ujauzito husababisha kupata mtoto mwenye matatizo ya kifua. Nimeogopa kidogo maana mdogo wangu ana mimba na anapenda sana kunywa maji ya baridi.
JamiiCheck tusaidieni kuhakiki hii.
Nimesikia mtaani wanawake wanaambiana kuwa Kunywa maji ya Baridi wakati wa Ujauzito husababisha kupata mtoto mwenye matatizo ya kifua. Nimeogopa kidogo maana mdogo wangu ana mimba na anapenda sana kunywa maji ya baridi.
JamiiCheck tusaidieni kuhakiki hii.
- Tunachokijua
- Ujauzito ni hali ya mtu mwanamke kuwa na mtoto tumboni anayekua kwa muda hadi kuja kuzaliwa(mimba). Hali hiyo kwa kawaida inadumu wiki 38 (miezi tisa hivi) ambapo mimba inazidi kukua na kukomaa ndani ya tumbo la uzazi la mama yake hadi wakati wa huyo kujifungua.
Maji ni kimiminika ambacho ni kiini cha uhai wowote duniani na pia kiini cha utamaduni wa binadamu. Hakuna mtu anayeweza kuishi bila maji kwa sababu asilimia 75 za mwili wa mwanadamu ni maji.
Wakati wa hali ya ujauzito baadhi ya wajawazito huvutiwa zaidi na unywaji wa maji ya baridi sana, hata hivyo hukutana na upinzani kutoka kwa baadhi ya watu kuwazuia kunywa kwa kuwaambia kuwa watoto waliobeba watazaliwa wakiwa na madhara kama magonjwa ya kifua.
Je, ni kweli Kunywa maji ya Baridi wakati wa Ujauzito husababisha kupata mtoto mwenye matatizo ya kifua?
Wakati wa ujauzito, mtoto anakua mahali salama kwenye tumbo la uzazi la mama na hutunzwa kwa usalama kila mwezi anavyoendelea kukua kwa miezi yote mpaka kuzaliwa, hivyo ili awe na afya kila aina ya virutubisho huchukuliwa kupitia chakula, virutubisho humfikia mtoto kwa urahisi kupitia plasenta. Mwili wa Mama wenye afya una uhusiano wa moja kwa moja na mtoto, kwa hiyo ni muhimu kupata chakula kizuri chenye virutubisho muhimu kipindi chote.
Kwa mujibu wa Daktari Bingwa wa Uzazi na Magonjwa ya Wanawake katika Hospitali ya Mtaalamu wa Irrua(The Lead Obstetrician and Gynaecologist at the Irrua Specialist Teaching Hospital), Jimbo la Edo, Dk Joseph Okoeguale, kupitia Punch Newspapers anasema hakuna madhara kwa mtoto ambaye hajazaliwa ambaye mama yake hunywa maji baridi wakati wa ujauzito
Kunywa maji ya baridi hakuwezi kumuathiri mtoto aliyeko tumboni, anaeleza iwapo mama akinywa maji ya baridi anakuwa kanywa kwa ajili yake tu kwani chochote mama anachokula au kunywa ni virutubisho pekee ndivyo huchukuliwa kwenda kwa mtoto kupitia plasenta kwani tumbo la mama la chakula lipo tofauti na tumbo la uzazi la mtoto ambalo tumbo la mtoto huwa limezungukwa na maji ambayo mtoto hukua humo.
Hakuna uhusiano kati ya kunywa maji baridi na kusababisha baridi kwa watoto ambao hawajazaliwa. Hakuna njia ambayo mtoto atakuwa na mafua au matatizo ya kifua baada ya kuzaliwa ikiwa mama hunywa maji baridi wakati wa ujauzito. Hii ni kwa sababu mwanamke anapokuwa mjamzito, mtoto hutenganishwa na mama yake. Mtoto yuko katika tumbo tofauti na analopokelea mama maji au chakula, mtoto yuko tumboni na pia kuna majimaji yaliomzunguka, mawasiliano kati ya mama na mtoto ni kupitia placenta.