Kuna watu wana miaka 30 na bado wapo nyumbani kwa wazazi, nimelia sana

Haki vile!watu Wana hustler Hadi sio poa yaani lakini mambo bado magumu,,,hakuna haja kuwadharau ambao hawajatoboa tuombeane,tutiane Moyo,inatosha!
Yaaah maisha bwana ndio yalivyo, hakuna kupumzika mpaka unaingia kaburini
 
Miaka 30 ni mingi sana kukaa hapa duniani sio tu kukaa nyumbani, inabidi uwe umesha leta impact.

Kuna watu kabla ya hiyo miaka walishafanya makubwa sana hadi sasa bado wanakumbukwa kwenye historia ya Dunia.

Unamjua Alexander the Great, aliyoyafanya yote hadi kutawala almost Dunia nzima Aliya fanya kabla ya kufikia miaka 30 na alikufa akiwa 30'S, ila hadi saivi anakumbukwa na hawezi kusahaulika kwenye historia ya Dunia ingawa aliishi B.C huko.

Huo ni mfano mmoja tu ila ukiwa na miaka 30 inabidi uwe umeshafanya mambo makubwa tuu, hata kufa tayari, kama kina kanumba etc.

Fanya kitu leta impact amsha, kwani wewe ulikuja Duniani ku enjoy tuu?

Muda ni mchache sana, kama ulitaka kukaa milele si ungekua mlima, au hata uwe kobe uishi miaka 200+! Binadamu aliumbwa akapewa akili ili aje kuleta impact kwenye Dunia au wewe utashabikia tu Simba na Yanga, "Stop existing start living."

Kwa wataoniuliza mimi nimefanyaje na nina miaka ngapi mimi nina miaka 12!
Kuna mambo mengi ya kufikiria kwa kijana wa umri wa kuondoka nyumbani.

Kwa namna yeyote ile kuondoka nyumbani kunapaswa kuzingatia afya ya wazazi wenyewe.
Ikiwa wazazi wanajiweza hasa kiafya na walao kumudu maisha ya kika siku basi hata miaka 19 unaweza kutoka nyumbani kwa ajili ya kwenda kutafuta maisha na changamoto zingine kwa mustakabali wa maisha yako, familia na wazazi.
Lakini kama wazazi wana changamoto kubwa ya kiafya mfano uzee sana, uwezo mdogo wa kujihudumia, ulemavu na magonjwa yanayoyohitaji uangalizi wa karibu basi hakuna haja ya kufanya hivyo badala yake tumia muda wako kupambania maisha ukiwa hapohapo nyumbani ili kutoa usaidizi wa karibu kwa wazazi wako.
 
Labda hiyo miaka thelathini uwe una ulemavu mmoja au mwingne kinyume na hapo itakuwa ni uvivu mkubwa wa kiakili na kimwili hivyo sio sahihi kuishi na wazazi miaka yote hiyo
 
Shida ipo wapi sasa si naishi kwetu bro siishi kwenu,tena wapo wanapika chapati nizigonge na chai baadaye niingie kijiwe pale kwa chande kucheza draft na kuisema serikali,majira ya saa moja usiku nirudi kugonga msosi na kulala
 
Moja ya mambo huwa yamewashinda kuyaelewa watu ni kufananisha Umri na mafanikio.

Miaka 30 unaweza ukawa hauna kitu chochote unachomiliki ,ikiwemo ,kazi, elimu, familia , n.k

Ila miaka 31 ukajikuta Una kila kitu.

Hapa duniani huwa hakuna umri wa kufanya jambo Fulani Ila huwa kuna wakati na majira ya kufanya jambo Fulani.

Jambo la muhimu ambalo kijana anabidi kuwa nalo ni kuwa sober 24/7

Umri huwa haumfanyi MTU afanikiwe wala asifanikiwe

Unaweza msoma hata founder wa KFC katoboa Ana miaka 65+yrs
Ndio unaweza amka ukashinda mkeka au Biko ghafra tukakusahau
 
Miaka 30 ni mingi sana kukaa hapa duniani sio tu kukaa nyumbani, inabidi uwe umesha leta impact.
.........

Kwa wataoniuliza mimi nimefanyaje na nina miaka ngapi mimi nina miaka 12!
Umeruhusiwaje kujiunga na JF kwa muri huo?
Moderator siku hizi masharti yamebadilishwa? Siyo miaka 18+ tena?
 
Miaka 30 ni mingi sana kukaa hapa duniani sio tu kukaa nyumbani, inabidi uwe umesha leta impact.

Kuna watu kabla ya hiyo miaka walishafanya makubwa sana hadi sasa bado wanakumbukwa kwenye historia ya Dunia.

Unamjua Alexander the Great, aliyoyafanya yote hadi kutawala almost Dunia nzima Aliya fanya kabla ya kufikia miaka 30 na alikufa akiwa 30'S, ila hadi saivi anakumbukwa na hawezi kusahaulika kwenye historia ya Dunia ingawa aliishi B.C huko.

Huo ni mfano mmoja tu ila ukiwa na miaka 30 inabidi uwe umeshafanya mambo makubwa tuu, hata kufa tayari, kama kina kanumba etc.

Fanya kitu leta impact amsha, kwani wewe ulikuja Duniani ku enjoy tuu?

Muda ni mchache sana, kama ulitaka kukaa milele si ungekua mlima, au hata uwe kobe uishi miaka 200+! Binadamu aliumbwa akapewa akili ili aje kuleta impact kwenye Dunia au wewe utashabikia tu Simba na Yanga, "Stop existing start living."

Kwa wataoniuliza mimi nimefanyaje na nina miaka ngapi mimi nina miaka 12!
Unataka nihame niende wapi ???
 
Back
Top Bottom